Thursday, March 26, 2015

OFISI ZA CUF ZATEKETEA KWA MOTO

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim  Seif  Sharif Hamad amechukizwa na kitendo cha kuchomwa moto ofisi za chama cha CUF katika  jimbo la Dimani visiwani Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kujionea ofisi hizo zilizoteketea kabisa kwa moto, tukio lilifanywa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Malim Seif alisema hali hiyo inasikitisha na ina lengo la kuchafua hali ya amani na utulivu iliyopo visiwani Zanzibar kwa sasa.
Aliongeza kwa kulitaka jeshi la Polisi visiwani Zanzibar, kufanya uchunguzi wa kina ili kuwajua watu walio husika kuchoma moto ofisi za chama hicho  katika jimbo la Dimani  wilaya ya Magharibi Unguja.
Katika tukio hilo inadaiwa watu wasio fahamika walifika katika ofisi hizo usiku majira ya saa nane wakiwa kwenye gari ambapo walitoa matairi na kuyaingiza ndani ya ofisi na  kisha  kuilipua ofisi hiyo.
Kufuatia jengo hilo kuungua limesababisha hasara ya takribani milioni 135.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea Ofisi ya (CUF) jimbo la Dimani kuangalia uharibifu uliofanywa baada ya ofisi hiyo kuchomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuni. Picha na Salmin Said, OMKR

SOURCE: TIMES FM

No comments: