Thursday, March 26, 2015

FAHAMU, ONGEA, SIKILIZWA (FOS II) SASA NI TANDAHIMBA







Mweka hazina wa MRENGO, Mustafa Kwiyunga, akizungumza na wadau wa Warsha wilayani Tandahimba
               
          Mradi wa Fahamu, Ongea, Sikilizwa (FOS II) uliozinduliwa Jumapili iliyopita wilayani Newala, sasa ni zamu ya Tandahimba ambapo jana iliendeshwa warsha ya siku moja kwa wadau wa maendeleo, lengo kuu la mradi huo ni kutoa mchango kwa serikali za mitaa zilizo wazi katika uchaguzi mkuu ujao, ambapo wananchi hususani makundi yaliyo pembezoni, ya wanawake na vijana watashiriki kama wapiga kura, kuwa wagombea na waangalizi wa uchaguzi.
Mustafa Kwiyunga

   Warsha ya kutathimini fursa na changamoto zinazowakumba vijana katika kujiletea maendeleo ngazi ya jamii iliendelea hapo jana katika wilaya ya Tanadahimba ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo walijitokeza kwa wingi katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la polisi wilayani humo.
Wadau wa Warsha, wilayani Tandahimba








No comments: