Thursday, September 18, 2014

OTTMAR HITZFELD AHOFIA MTAFARUKU KUIBUKA BAYERN

Ottmar Hitzfeld

                       




















Na Juma Mohamed

Kocha wa zamani wa miamba wa Ujerumani Bayern Munich, Ottmar Hitzfeld, ametabiri mtafaruku baina ya wachezaji utazuka wakati mabingwa hao wa Bundesliga watakapokuwa wameungana na wachezaji walio majeruhi.

Akizungumza na gazeti la Bild, Hitzfeld alisema, “Kila mchezaji anakubali kukaa kwenye benchi kwa muda. Lakini hali itakuwa ya hatari baadaye msimu huu wakati  wachezaji wanaorejea baada ya kuuguza majeraha wataanza kulalamika kwa kutumiwa kama wachezaji wa ziada.”

Hitzfeld, 65, aliyeongoza Bayern kutwaa ubingwa wa Ulaya mwakani 2001 dhidi ya Valencia ya Uhispani alionya mwalimu wa sasa, Pep Guardiola kuwa, “Kunaweza tokea vita vya kindani.”
“Wakati kila mchezaji atataka kuwa katika kikosi cha kwanza, kutakuwa na shida na wengine hawatasita kuelezea kukatishwa tama,” aliongeza.

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: