Thursday, September 18, 2014

GUARDIOLA: MAN UTD HAWANA JEURI YA KUNIBOMOLEA KIKOSI CHANGU

 http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/e/e5/Guardiola_2010.jpg

 Na Juma Mohamed

Kocha mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola amezua majibizano makali baada ya kudai kuwa Manchester United hawana pesa za kutosha kuwashawishi wachezaji wake kutoka Allianz Arena.

Manchester united imetumia takriban pauni milioni 150 kuwanunua wachezaji akiwemo mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi nchini Uingereza Angel Di Maria kutoka Real Madrid.

Maria aliigharimu United takriban pauni milioni 59.7 alipotua Old Trafford.

Sasa Guardiola akizungumza na wanahabari alisema kuwa hana hofu ya kuwapoteza wachezaji wake kwenda Old Trafford. "hawana pesa .

'Samahani hawana hela hawa,'' kocha huyo alinukuliwa akisema .

Guardiola, alikuwa akizungumza kabla ya mabingwa hao wa Bundesliga kuchuana dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester City .

''Niliwaona wakitumia pesa nyingi tu lakini unajua hawa wachezaji wenyewe wameamua kusalia hapa tu ''

Guardiola, aliwahi kuwa chini ya Louis van Gaal' alipokuwa Barcelona kabla ya wawili hao kutengana Pep alipoondoka kuchukua wadhfa wake mpya kama kocha

 

SOURCE: BBC

No comments: