Thursday, September 18, 2014

LAMBERT AMWAGA WINO VILLA PARK

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02234/paul-lambert_2234921b.jpg
Paul Lambert

 Na Juma Mohamed

Meneja wa Aston Villa Paul Lambert ametia saini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamuweka Villa Park hadi Juni 2018, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilitangaza Jumatano.

Lambert, 45, alichukua hatamu Villa mwaka 2012 na ameongoza klabu hiyo ya Midlands kuwa katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Uingereza baada ya mechi nne msimu huu mpya.

“Nimejitolea kuhakikisha tunaendelea kuunda klabu hii hadi ifikie pale tunapotaka,” Lambert alisema kwa mujibu wa nukuu katika akaunti rasmi ya Twitter ya Villa.

"Hii ni klabu kubwa, kalbu nzuri sana ya soka, Tunaweza kuangalia siku za usoni tukiwa na matumaini na hamu ya kufana msimu huu, na misimu itakayofuata.”

Lambert, aliyekuwa kiungo wa kati wa kimataifa wa Scotland wakati wa uchezaji wake, alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Borussia Dortmund mwaka 1997 na akaanza ukufunzi baada ya kustaafu 2005.

Baada ya kukaa Livingston, Wycombe Wanderers, Colchester United na Norwich City, alijiunga na Villa Juni 2012 baada ya Alex McLeish kufutwa.

Villa walimaliza katika nafasi ya 15 misimu ya kwanza miwili ya Lambert kuwa kwenye usukani, na kuponyoka kushushwa ngazi kwa alama tano nyakati zote mbili.

Lakini wameanza vyema msimu huu, na walishinda 1-0 wakiwa Liverpool Jumamosi kwenye mechi yao ya majuzi zaidi.

 

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: