Thursday, September 18, 2014

UINGEREZA WAANZA KAMPENI YA KUWAONDOA NYOTA WA KIGENI


Na Juma Mohamed 

                                            
Shirikisho la kandanda nchini Uingereza, FA, limeanzisha mpango unaonuia kupunguza wachezaji wa kigeni wanaocheza waocheza soka nchini humo, kwa kiasi kinachoweza kufika asilimia 50.

Watawala hao wa soka Uingereza wametoa orodha ya mabadiliko kwa muundo wa sasa katika harakati za kuongeza idadi na ubora wa vipaji asili katika nchi hiyo.

Orodha hiyo imewasilishwa kwa ligi ya Premier, ligi ya daraja la kwanza na muungano wa wachezaji na mameneja na nia yao ni kuanza kuitekeleza kabla ya mwanzo wa musimu wa 2015-16.
FA wanaamini kuwa mpango huo utawezesha taifa lao kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: