Wednesday, September 24, 2014

KIONGERA NJE KWA WIKI 8, KUIKOSA YANGA

Paul Raphael Kiongera



Na Juma Mohamed

Straika wa Simba raia wa nchini Kenya Paul Raphael Kiongera, ataukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi watani wao wa jadi Yanga utakaofanyika Oktoba 12 katika Uwanja wa Taifa Dar Es salaam, baada ya kuumia katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Coastal Union uliomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2.
Kiongera alipata jeraha hilo la goti baada ya kugongana na golikipa wa Coastal Union Shabani Kado, na kulazimika kutoka nje dakika ya 88 baada ya kucheza kwa dakika 21 pekee, baada ya kuingia katika dakika ya 67.

Ripoti zinasema straika huyo atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki 6 hadi 8 kabla ya kuanza mazoezi, kwa maana hiyo ataukosa mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Oktoba 12.
Amejiunga na orodha ya wachezaji majeruhi wa Simba ambao ni Issa Rashidi na Haroun Chanongo, lakini kuna habari njema pia kwa wanamsimbazi kutokana na kurejea kwa kiungo wao mahiri Jonas Mkude.

Simba wamepiga kambi visiwani Zanzibar, kujiandaa na mchezo wao unaofuata wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Moro, utakaopigwa Septemba 27 mwaka huu.
 
SOURCE: GOAL.COM

No comments: