Na Juma Mohamed
Ripoti iliyotolewa kuhusu tenda ya kuhodhi michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 na mwaka 2022 imeelezwa huenda ikasabisha wanaoshutumiwa kufunguliwa mashtaka.
Mwanasheria kutoka nchini Marekani, Michael Garcia alitoa ripoti yake mwezi huu, lakini Fifa imesema yaliyomo kwenye ripoti hiyo hayatatolewa hadharani
Kamati ya Qatar iliyokuwa ikiwania tenda kuhodhi michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 inakabiliwa na shutuma kuwa ilitoa rushwa kupatiwa nafasi hiyo,baada ya Gazeti moja kuripoti mwezi juni kuwa aliyekuwa makamu wa rais wa fifa Mohamed bin Hammam alitoa rushwa ya pauni milioni tatu ili kupata tenda hiyo.madai ambayo Qatar imeyakanusha.
Uamuzi baada ya kutoka kwa ripoti hiyo utatolewa mwakani.
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment