Thursday, September 18, 2014

KIBARUA CHA SOLSKJAER KINAELEKEA KUOTA NYASI

http://e1.365dm.com/14/01/768x432/Ole-Gunnar-Solskjaer-Cardiff-press-conference_3060500.jpg?20140102135041

Ole Gunnar Solskjaer





 Na Juma Mohamed

 

Meneja wa Cardiff City Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kuiacha klabu hiyo baada ya kuwa kwenye usukani miezi tisa.

Solskjaer, 41, alifanya mashauriano na mwenyekiti Mehmet Dalman Jumatano.

Tangazo kuhusu mustakabali wa raia huyo wa Norway linatarajiwa kutolewa Alhamisi, huku maelezo kuhusu kuondoka kwake yakiendelea kukamilishwa.

Klabu hiyo, ijulikanayo kwa utani kama Bluebirds (Ndege wa Bluu), imo katika nafasi ya 17 katika ligi ya daraja la pili baada ya kushindwa mechi mbili kati ya saba walizocheza, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwao nyumbani 1-0 na Middlesbrough Jumanne na pia kucharazwa 4-2 na Norwich.

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: