Wednesday, September 24, 2014

FERGUSON AITWA KWENYE MCHEZO WA GOFU...

Sir Alex Ferguson


Na Juma Mohamed

Nahodha wa kikosi cha Ulaya kitakachowania kombe kuu la gofu, Ryder Cup, juma hili kwenye klabu ya mchezo huo, Gleneagles, Paul McGinley, amemualika mwalimu gwiji mstaafu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, kupatia kikosi chake hotuba ya kuwahamasisha.
Nahodha huyo alinuia kuweka mpango huo faraghani lakini siri ilifuchuka  wakati mwalimu huyo shupavu alipoonekana Gleneagles kabla ya zoezi la kwanza rasmi la kikosi cha Ulaya Jumanne asubuhi.
“Tumepatana mara kadhaa miezi iliyopita kufuatia mkutano wetu wa kwanza miaka 15 na tukashiriki pamoja chakula cha mchana. Tulipanga ahudhurie hafla ya chakula cha jioni cha kikosi chetu na kuwahutubia ili waweze kupata motisha kupambana na Marekani.
“Hayo hayatachukua mwelekeo wa mwalimu mkuu darasani na wanafunzi ila litakuwa zoezi la kuchangamsha. Yeye ni shabiki mkubwa wa gofu na anafahamu Rory (Mclloroy) vizuri kwani Rory (mchezaji gofu nambari moja duniani) ni shabiki sugu wa Manchester United,” McGinley alisema.

Kualika makocha shupavu kuhotubia vikosi vya Ryder Cup si jambo geni kwani miaka miwili iliyopita Medinah, nahodha wa Ulaya, Jose Maria Olazabal, alimleta mwalimu wa sasa wa Bayern Munich, Pep Guardiola, ambaye wakati huo alikuwa kinara wa Barcelona.

SOURCE: SUPER SPORT

No comments: