Thursday, July 12, 2012

BAADA YA PODOLSKI KUINGIA KWENYE MUZIKI SASA NI ZAMU YA THOMAS ROSICKY


MASIKINI HAIKUHUSU HII: KUANGALIA MAZOEZI YA RONALDO NA WENZIE WA REAL MADRID NI SHILINGI 600,000

Ikiwa unaishi nchini Marekani na ukapenda kuwaona Real Madrid, then kuna taarifa nzuri na mbaya kwa ajili yako.

Taarifa nzuri ni kwamba mabingwa hao wa Spain watakuwa wakifanya mazoezi kwenye sehemu ya wazi kwa wale ambao wangependelea kuwaona: habari mbaya ni kwamba itabidi uichimbue sana mifuko yako kuweza kulipia kuwaona Ronaldo na wenzie wakifanya mazoezi. Gharama za tiketi kuwaona Madrid zimepanda mpaka kufikia €311 kwa kipindi cha saa moja na nusu kuweza kumshuhudia Mourinho akitoa maelekezo huko Los Angeles mwezi August tarehe 4.

Tiketi ya bei rahisi itagharimu kiasi cha €69, lakini tiketi ya gharama zaidi itakayokuwa ikihusisha kupata breakfast pamoja na kuweza kukutana na wachezaji na kuongea nao itarudi na kufikia €311 ambayo ni sawa na kiasi kisichopungua 650,000 za kibongo.

Na kama utapenda kuangalia mazoezi na kwenda kuangalia mechi ya kirafiki dhidi ya LA Galaxy, then itabidi uongeze €448

GOLI LA SIKU


Munir Zakaria afutiwa cheo chake na ZFA

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimemuengua Munir Zakaria kuwa Ofisa Habari na msemaji wake, pamoja na kumteua Suleiman Mahmoud Jabir, kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Abdallah Juma Mohammed kuwa Mwanasheria wa chama hicho. Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa kamati tendaji ya chama hicho uliofanyika juzi kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View, chini ya Mwenyekiti Amani Ibrahim Makungu ambaye ni Rais wa ZFA Taifa

Rais wa Chama Cha Soka (ZFA) Amani Ibrahim Makungu (katikati) akizungumza na Afisa Habari Munir Zakaria (kulia) na Rais aliyestaafu Ali Fereji Tamim kushoto)
.
Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Kassim Haji Salum, ameliambia gazeti hili kuwa, kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, msemaji wa mambo mbalimbali yanayokihusu ni Rais kwa kushauriana na Katibu Mkuu.
“Kwa mujibu wa katiba yetu, Rais ana nafasi nne za kufanya uteuzi wa watu wa kumsaidia kazi, lakini pia ndani ya katiba hiyo, hakuna nafasi ya Ofisa Habari, na kazi ya kukisemea ni ya Rais kwa kushirikiana na Katibu Mkuu”, alifafanua.
Hata hivyo, alisema Zakaria anabakia kuwa mjumbe wa kawaida wa kamati tendaji, hadi hapo itakapoamuliwa vyenginevyo.
“Hivi sasa, tunafanya kazi zetu kikatiba zaidi, na kufutwa kwa nafasi ya Ofisa Habari ni miongoni mwa utekelezaji wa katiba hiyo”, alisema.
Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa ZFA ilichukizwa na kauli ya Zakaria aliyoitoa katika vyombo vya habari, kwamba iwapo klabu za Simba na Azam FC zitaingia fainali ya mashindano ya Kombe la Urafiki, mchezo huo utahamishiwa jijini Dar es Salaaam, kauli iliyozusha malalamiko kutoka kwa mashabiki wengi wa soka wa Zanzibar.
Kwa upande mwengine, alizitaja kazi zitakazomuwajibikia Mkurugenzi wa Ufundi, kuwa ni kupanga programu za maendeleo ya mchezo wa soka kwa ajili ya timu za madaraja yote, kuanzia ngazi ya watoto hadi wachezaji wakubwa.
Aidha, Mkurugenzi huyo atakuwa na wajibu wa kuandaa mipango ya mafunzo (mtaala) kwa walimu wa soka, waamuzi pamoja na viongozi wa klabu mbalimbali.
Katibu huyo ameeleza kuwa, kazi zote zinazohusiana na mambo ya kisheria, sasa zitashughulikiwa na Mwanasheria aliyeteuliwa, Abdallah Juma Mohammed.

No comments: