Sunday, May 13, 2012

MUNGU IBARIKI SIMBA SC LEO


Kikosi cha Simba
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC leo wana kazi moja tu ya kumalizia kazi waliyoifanya kwa kiasi kikubwa Dar es Salaam, wiki mbili zilizopita.
Simba leo itakuwa uwanjani Sudan kumenyana na Al Ahly Shendi ya huko katika mechi ya pili ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Simba iliondoka jijini Jumanne kuelekea Sudan kwa ajili ya mechi hiyo ambapo hata hivyo hawakupata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao hali ilioufanya uongozi wa klabu
hiyo kuazimia kupeleka malalamiko (CAF).
Simba leo inahitaji ushindi au kama kufungwa isiwe zaidi ya mabao 3-0 ili isonge mbele hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Habari kutoka Sudan zinasema pamoja na vituko walivyofanyiwa na wenyeji, lakini kikosi cha Simba kiko imara kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa katika mji wa Shendi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga Simba imefanyiwa vitendo ambavyo si vya kiuanamichezo ikiwa ni pamoja na kusafirishwa umbali mrefu, kupewa chakula usiku sana pamoja na kulazwa kwenye hosteli badala ya hoteli nzuri kama walivyofanyiwa wao
walipofika nchini.
Kamwaga alisema wachezaji wako kwenye hali nzuri na kocha Milovan Circovick ameahidi kuibuka na ushindi.
“Kila kitu chetu kwa upande wa benchi la ufundi kiko sawa, pamoja na vurugu zao lakini tunaamini dakika 90 uwanjani ndio zitaongea,” alisema Kamwaga.
“Wachezaji wako kwenye ari kubwa pamoja na mizengwe ya hapa na pale, kwani hawakukatishwa tamaa badala yake walifanya mazoezi wenyewe pamoja na kocha kuwapa
mapumziko… wachezaji wanasema lengo lao ni kuvuka raundi inayofuata na watavuka hata wakiwafanyiwa vituko,”alisema Kamwaga.


VIKOSI VYA LEO:
SIMBA SC:
Kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kuwa; Juma Kaseja. Shomari Kapombe, Amir Maftah, Victor Costa, Kelvin Yondan, Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman, Patrick Mafisango, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi, wakati kwenye benchi watakuwapo Ally Mustafa
‘Barthez’, Obadia Mungusa, Juma Jabu, Derrick Walullya na Salum Machaku.

Al AHYL SHANDY:
Abdulrahma Ali, Elnour Altigani, Isaac Seun Malik, Saddam Abu Talib, Fareed Mohamed/Orwah Ibrahim dk 83, Zakaria Nasu, Razak Yakubu, Faris Abdallah, Hamopuda Bashir/Mogabid Farouq dk63, Nadir Eltaveb na Bashiro Ubamba.

Mungu ibariki Simba. Ibariki Tanzania. Amiiin.
 

SAMATTA, MAZEMBE WATINGA NANE BORA AFRIKA


Sixième quart consécutif pour Mazembe !
Sinkala



TOUT Puissant Mazembe imefuzu kuingia Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa mara ya sita mfululizo baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji El Merreikh kwenye Uwanja wa Omdurman, Khartoum jana, Mazembe, yenye mshambuliaji mwingine Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu, lakini ‘anasugua mwanzo mwsiho’, ilitangulia kupata bao kupitia kwa Nathan Sinkala.
Mazembe imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga bao moja.
Merreikh ilisawazisha kupitia kwa mchezaji wake Mganda, Mike MUTYABA dakika ya 61.
Kama kawaida, mshambuliajio chipukizi wa Tanzania, Mbwana Ally samatta alikuwa mwiba mchungu kwenye safu ya ulinzi ya Merreikh na hata bao la jana lina mchango wake.
Sasa ni wakati wa Samatta kujiuza zaidi kupitia mechi sita atakazocheza kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa- na kutokana na ndoto za Mazembe kuchukua ubingwa, kuna uwezekano kinda huyo wa Tanzania mwishoni mwa mwaka akaweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.


GONGA CHINI KILA PICHA UIONE KWA UKUBWA HALISI Al Merreikh Vs TP Mazembe

UNAYOPASWA KUJUA KABLA YA MAN CITY V QPR LEO

Aguero


VIKOSI VYA LEO:


MANCHESTER CITY


Hart
Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy Yaya Toure, Barry
Nasri, Silva
Aguero, Tevez
QPR

KennyOnuoha, Ferdinand, Hill, Taiwo
Mackie, Barton, Derry, Taarabt
Zamora, Cisse


IKIWA haina mchezaji majeruhi au anayetumikia adhabu, kocha Roberto Mancini hana cha kuhofia akiwa kikosi kamili katika mechi ya mwisho ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, dhidi ya QPR Uwanja wa Ethiad leo.
Kwa sababu hiyo, hatutarajii mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City ikitarajiwa kushusha kikosi kile kile kilichozifunga Manchester United na Newcastle katika mechi mbili zilizopita.
Kwa QPR, wote Shaun Derry anayesumbuliwa na maumivu ya mguu na Akos Buzsaky nyama za paja, wako shakani kucheza, ingawa kocha though Mark Hughes anaweza 'kuwatoa muhanga' ili kuimarisha safu yake ya kiungo katika mchezo wa leo mgumu wanaotakiwa kushinda wabaki Ligi Kuu.
Samba Diakite anayesumbuliwa na virusi, dhahiri ataukosa mchezo huo, wakati Alejandro Faurlin ataendelea kuwamo kikosini licha ya maumivu ya mguu yanayomkabili. Djibril Cisse, aliyefunga bao muhimu pekee la ushindi dakika za mwishoni dhidi ya Stoke City katika mchezo uliopita ugenini, anaweza kuwamo kwenye kikosi cha kwanza.


JE, WAJUA?

  • <!--[if !supportLists]-->1. <!--[endif]-->Manchester City wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa, kwani hata Manchester United wakiifunga Sunderland, wao wakawafunga QPR kipigo kiduchu, wanajivunia wastani wa mabao tisa zaidi walioyonayo hadi sasa dhidi ya wapinzani wao hao.

    <!--[if !supportLists]-->2. <!--[endif]-->Kikosi cha Roberto Mancini, kimeshinda mechi zao 17 za nyumbani hadi sasa, na matokeo mbaya Etihad hadi sasa ni sare ya 3-3 na Sunderland, Machi 31.

    <!--[if !supportLists]-->3. <!--[endif]-->Mshambuliaji wa City, Sergio Aguero amefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu msimu huu (22) ambayo ni mabao manne zaidi katika idadi ya jumla ya mabao ya QPR waliyofunga msimu huu.

    <!--[if !supportLists]-->4. <!--[endif]-->Wenyeji wameshinda mechi zao zote tano zilizopita, wakitisa nyavu za wapinzani mara 15 ndani ya mechi hizo na zao kutikiswa mara moja tu.

    <!--[if !supportLists]-->5. <!--[endif]-->QPR wamefungwa mechi 10 zilizopita kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Stoke City katika mechi iliyopita.
    <!--[if !supportLists]-->6. <!--[endif]-->Pointi tatu zitaihakikishia QPR. Sare pia itawasaidia kunusurika kwa wastani mzuri wa mabao - lakini kikosi cha Mark Hughes kikifungwa na Bolton ikaifunga Stoke, wageni watarejea Championship.

    <!--[if !supportLists]-->7. <!--[endif]-->Tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Lazio, Januari, Djibril Cisse (pichani juu kulia) amekuwa akifunga mabao sambamba na kupigwa kadi nyekundu, hadi sasa akiwa amefunga mabao matano na kupewa kadi mbili nyekundu.

    <!--[if !supportLists]-->8. <!--[endif]-->Kocha wa QPR, Hughes aliiongoza City kwa miezi 18 kati ya mwaka 2008 na 2009 kabla ya kupigwa chini na nafasi yake kupewa Mancini.

    <!--[if !supportLists]-->9. <!--[endif]-->Man City wana kawaida ya kuuanza mchezo mtaratibu, huku asilimia nane tu ya mabao yao ndiyo yamepatikana katika dakika 20 za mwanzo kwenye Ligi Kuu, wakati QPR asilimia 25 ya mabao yao ni ya mapema..

    <!--[if !supportLists]-->10. <!--[endif]-->Yaya Toure alifunga bao la ushindi katika ushindi wa 3-2 wa City mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Loftus Road,Novemba 5, mwaka jana

No comments: