Van Persie

Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

MAN UNITED WANAMTAKA VAN PERSIE

KLABU ya Manchester United imeamua kuungana na mahasimu wao, Manchester City katika kuwania saini ya Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28-mkataba wake Emirates unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.
KLABU ya Juventus imejitoa kwenye mbio za kuwania saini ya Van Persie, ikihofia haitaweza kushindana kwa dau na Manchester City na sasa wanahamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Napoli, Edison Cavani.
Athletic Bilbao striker Fernando Llorente
Llorente.
Manchester City inajiandaa kubomoa benki na kutumia kiasi cha pauni Milioni 28.7 ili kumnasa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27 kutoka Athletic Bilbao, Fernando Llorente.
MCHEZAJI anayewani na Chelsea na Everton, Oscar Cardozo ameambiwa anaweza kuondoka Benfica. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, pia anazivutia klabu za CSKA Moscow na Rubin Kazan.
KIUNGO wa Montpellier na Morocco, Younes Belhanda mwenye umri wa miaka 22, amepuuza tetesi za kutakiwa na Arsenal na Liverpool kwa kusema kwamba anataka kubaki kwa vinara hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa msimu ujao.
KIUNGO wa Borussia Dortmund, Shinji Kagawa amesema alifanya mazungumzo na kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson. "Alikuwa ana vitu vizuri vya kuniambia," alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan, mwenye umri wa miaka 23.
KLABU ya Fulham imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Huddersfield na Scotland, Jordan Rhodes, ikimpata kwa dau la pauni Milioni 3.5 nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, ikizipiku Norwich, Aston Villa na West Ham.

DESCHAMPS, AVB, KLOPP KUMRITHI DALGLISH LIVERPOOL...

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas, kocha wa Borussia Dortmund, Juergen Klopp na wa Marseille, Didier Deschamps ni miongoni mwa walimu waliomo kwenye orodha ya makocha wanaotakiwa kurithi mikoba ya Kenny Dalglish Liverpool.
BEKI Rio Ferdinand hamemtupia lawama kocha wake wa Manchester United, Alex Ferguson kwa amechangia kutemwa kwake katika kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachocheza fainali za Euros, baadfa ya Mscotland huyo kuulizwa kama beki huyo mwenye umri wa miaka 33 kama anaweza kucheza mechi za kimataifa.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Emmanuel Adebayor amesema chaguo lake la kwanza msimu ujao ni kuendelea kuichezea Tottenham, ambako amekuwa akicheza kwa mkopo msimu mzima. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, pia ana ofa ya kwenda kukipiga Marekani na Urusi.