Sunday, May 20, 2012

KUINUNUA MAN UNITED INABIDI UJIPANGE: PAMOJA NA KUKOSA KOMBE LOLOTE MSIMU HUU - YATAJWA KAMA TIMU YENYE THAMANI KUBWA KULIKO ZOTE



THE BRAND FINANCE FOOTBALL TOP 25 FOR 2012
2012 RANK 2011 RANK CLUB LEAGUE BRAND VALUE CHANGE IN VALUE
1 1 Man Utd England €672.9m 29 %
2
4 Bayern Germany €617.9m 59 %
3 2 Real Madrid Spain €471.7m -7 %
4 3 Barcelona Spain €455.9m -8 %
5 5 Chelsea England €312.9m 27 %
6 6 Arsenal England €305m 29 %
7 9 Liverpool England €288.5m 47 %
8 11 Man City England €237.4m 77 %
9 7 Milan Italy €229.5m 7 %
10 12 Schalke Germany €209.1m 97 %
11 15 Dortmund Germany €178.4m 81 %
12 14 Tottenham England €176.8m 77 %
13 8 Inter Italy €169m -18 %
14 23 Ajax Netherlands €144.6m 150 %
15 17 Marseille France €132.1m 41 %
16 10 Juventus Italy €125.8m -13 %
17 13 Hamburg Germany €120.3m 14 %
18 16 Lyon France €94.3m -1 %
19 25 Aston Villa England €68.4m 27 %
20 NEW Newcastle England €67.6m 115 %
21 18 Roma Italy €66.8m -16 %
22 24 Napoli Italy €66.8m 22 %
23 27 Everton England €62.1m 28 %
24 NEW Corinthians Brazil €60.5m NEW
25 22 Bordeaux France €59.7m -2 %

RAISI WA MASHABIKI WA CHELSEA TANZANIA ALIKUWEPO MUNICH KUISAPOTI THE BLUES


Wale waliosema football is madness hawakukosea kabisa. Soka ni mchezo ambayo unateka hisia kubwa za mwanadamu yoyote anayefuatilia mchezo huu, mfano hai ni Bwana Makulilo, mtanzania halisi anayeishi jijini Dar es Salaam.

Bwana Makulilo ambaye hujiita Raisi wa mashabiki wa Chelsea Tanzania, alifunga safari ya takribani siku mbili kutoka Bongo mpaka Munich Ujerumani kwa ajili ya kuisapoti timu yake ya The Blues katika mchezo bila kujali umbali wala gharama atakazoziingia kwa safari hiyo.
Watu wanapenda mpira bwana.

KUTOKA MUNICH: JEZI YA BASTIAN SCHWEINSTEIGER NDIO INAOONGOZA KWA KUNUNULIWA HAPA UJERUMANI.

Je umeshawahi kujiuliza na jezi ya mchezaji gani wa kibongo ndio inayoongoza kwa mauzo kwenye soko la jezi(hata kama feki)? Sidhani kama unaweza kupata majibu sahihi kutokana na mfumo uliopo.

Basi nikiwa hapa Ujerumani jijini Munich wakati nikiudhuria fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich, nililifanya kiutafiti kidogo kwenye maduka ya kuuza vifaa vya michezo kwa mfano jezi, na kwa hakika nilifanikiwa kupata majibu yafuatayo juu ya jezi za wachezaji gani maarufu hasa wa Bayern Munich ndio zinazoongoza kwa kununuliwa.


Jezi namba 31 mgongoni inayovaliwa na mchezaji wa mwisho wa Bayern Munich kukosa penati Bastian Schweinstieger (jina lake lina maana ya mpanda nguruwe) ndio inayoshika namba moja kwa mauzo ya jezi, huku namba mbili ikishikwa na jezi ya Frank Ribery, tatu Mario Gomez, Arjen Robben jezi yake inashika nafasi ya tano huku nafasi ya tano kwa mauzo ikishikiliwa na Olger Badstuger.


RIPOTI KUTOKA MUNICH: KABLA YA MCHEZO WA FAINALI YA UEFA - MASHABIKI WA BAYERN WALIVYOKUWA NA UHAKIKA WA USHINDI




HAPA MASHABIKI WA BAYERN MUNICH WAKIIIMBA WIMBO MAALUM WA KLABU HIYO



NIKICHEZA NA KUIMBA WIMBO BAYERN MUNICH

WANAUME WA EUROPA CHELSEA WAREJEA LONDON





BAADA YA CHELSEA KUBEBA UBINGWA: MWANAMUZIKI J.COLE NAE AJITOKEZA KAMA MSHABIKI WA THE BLUES

J.COLE KWENYE POZI BAADA YA MECHI YA CHELSEA NA BAYERN MUNICH KUISHA.

HARUNA MOSHI BOBAN NA MUSSA MGOSI WAWAKILISHA WACHEZAJI WA KIBONGO KWENYE MSIBA WA MAFISANGO

Leo hii yamefanyika mazishi ya mchezaji wa Simba Patrick Mafisango huko nchini Kongo - katika mazishi hayo wachezaji Haruna Moshi Boban wa Simba pamoja na Mussa Hassan Mgosi walikuwepo na kushiriki kikamilifu katika zoezi. Hapa juu kwenye picha Mussa Mgosi na Boban wakiwa na watoto wa marehemu Mafisango.
Hapa ndipo ulipo msiba wa Mafisango kwenye uwanja ambao marehemu alianza kucheza soka alipokuwa mdogo.

Umati wa watu uliodhuria

Boban na Mgosi wakiongea na baadhi ya wafiwa.


TWIGA STARS WAPIGWA 5-2 NA BANYANA BANYANA


TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini, Banyana Banyana, jioni hii imeitandiika Tanzania, Twiga Stars mabao 5-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa Twiga Stars inayonolewa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya wanaume, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, baada ya wiki iliyopita kufungwa 4-1 na Zimbabwe kwenye Uwanja huo huo katika mchezo wa kirafriki pia.
Aidha, haya ni matunda ya programu mbovu ya maandalizi ya timu hiyo hivi sasa, ambayo mara kwa mara imekuwa ikicheza mechi za kirafiki na timu ya waigizaji, badala ya kuwekeza kwenye maandalizi thabiti ya kuijenga timu.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Banyana yalitupiwa nyavuni na Portia Modise dakika ya 23 na 46, Sanah Mollo dakika ya 73 na 79 na Jamine van Wyk dakika ya 86, wakati ya Twiga yalifungwa na Fatuma Bashir dakika ya 67 na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika ya 77.


JANA NIKIWA KWENYE TRNI KUELEKEA ALLIANZ ARENA


SIKU YA MWISHO YA MAFISANGO JUU YA ARDHI - HARUNA MOSHI AZUILIWA UWANJA WA NDEGE

Michael Momburi, Kinshasa
SAFARI ya mwisho ya kiungo wa Simba, Patrick Mafisango kuonekana duniani, inakamilishwa leo wakati sanduku lenye mwili wake litakapoteremshwa kaburini baadaye jioni.

Mafisango alifariki alfajii ya Alhamisi iliyopita baada ya gai lake kuacha njia na kuingia mtaroni. Alikuwa akitoka Maisha Club kurudi nyumbani.

Kiungo huyo aliyeacha mke na watoto watatu, aliagwa juzi kwenye Viwanja vya Klabu ya Sigara, Chang'ombe Dar es Salaam.

Msafara wa uliosindikiza mwili wa Mafisango ulitua jijini hapa jana saa 6.10 mchana na kulakiwana mashabiki wengi wa kike huku askari wa usalama ndani ya Uwanja wa Ndege wahapa wakishindwa kujizuia na kumwaga machozi.

Mafisango atazikwa leo kwenye makaburi ya Kinkole yaliyoko karibu na Uwanja wa Ndege wa Kinshasa.

Baada ya mwili wa mchezaji huyo kutua, askari wa uhamiaji pamoja na wahudumu wa afya wanaokagua kadi za chanjo kwa wasafiri ndani ya uwanja wa ndege walianza kuuliza kwamba ni nani huyo lakini walipoelezwa bado hawakuelewa kwa vile mchezaji huyo hakuwahi kutamba na timu yoyote ya Kinshasa. Kiungo wa DC Motema Pembe, Mussa Hassan Mgosi alikuwa miongoni mwa waombolezaji.

Mkuu wa msafara wa Simba, Itang'are alipotoa nakala za magazeti ya Tanzania na kuwaonyesha waliacha kazi zao na kuuzingira mwili huo huku wanawake wakishindwa kujizuia nakuanza kumwaga machozi kwa jinsi walivyoona gari lake lilivyochakaa baada ya ajali hiyo.

Askari hao walitumia takribani dakika 10 kuangalia jeneza la mchezaji huyo huku wengine wakikimbia ofisi zao na kwenda kuliangalia na walisaidia kulitoa nje kuwakabidhi ndugu ingawa walizuia kabisa kupiga picha eneo la uwanja.

Licha ya barabara nyingi kuwa chakavu kwenda Lemba nje ya kidogo ya jiji alikokuwa akiishi marehemu, mwili wake ulibebwa kwa gari ndogo ukiongozwa na ving’ora ingawa msafara huo uliingiliwa na 'daladala'. Msafara mzima ulikuwa na magari manane.

Nyumbani kwa marehemu, kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakimlilia mchezaji huyo wa Rwanda na ilitumia karibu saa nzima kuwatuliza kabla ya Mzee Kinesi kumkabidhi baba mlezi wa Mafisango, Papaa Pierre mwili wa mchezaji huyo kisha kumwelezea tukio zima la ajali na hali ilivyokuwa Tanzania. Pierre alishindwa kujizuia na kuanza kulia kwa sauti ya juu.

Mwili huo wa mchezaji huyo ambaye hapa anafahamika kwa jina la Patrick Tabu Ete ambayo ndiyo majina halisi ya wazazi wake, haukukaa sana nyumbani hapo kutokana na nafasi kuwa ndogo na waliuhamishia kwenye Uwanja wa mpira wa Terrain ambao Mafisango alianzia kucheza soka ili kutoa nafasi ya mashabiki kumuaga zoezi linaloendelea hadi leo mchana.

Ingawa anaonekana si maarufu sana jijini hapa kama ilivyo Lubumbashi na Rwanda, mchezaji huyo picha zake zilikuwa zimebandikwa kwenye magari mbalimbali ya vijana na hadi jana jioni hakuna mke wake aliyekuwa amewasili wala mtoto.

Pierre alisema; “Msibahuu unauma sana, hakuna jinsi ninavyoweza kuelezea lakini nashukuru Wanasimbana Tanzania kwa kumpa heshima stahili mwanangu, hii ni kazi ya Mungu, tumpumzishe aende kwa amani.”

Ujumbe wa Shirikisho la Soka la Rwanda, Ferwafa pamoja na familia na wageni mbalimbali mashuhuri walitarajiwa kuwasili usiku wa kuamkia leo kwa shughuli hiyo.

Katika hatua nyingine, nguo za Mafisango zimeyeyuka kiaina huku Haruna Moshi ‘Boban’ akionja joto ya jiwe kwenye Uwanja wa Ndege wa hapa.

Ndugu wa Mafisango waliokuwa wakiishi naye jijini Dar es Salaam walidai kupakia nguo hizo kwenye ndege na walipofika Kinshasa hazikuonekana huku wahudumu wakidai zitakuwa zimesahaulika Nairobi.

“Sisi tuliziweka sehemu ya mizigo lakini tunashangaa hapa hazionekani wanasema labda zimebaki Nairobi, kule ndani ya begi lake vilikuwa vitu vyake vyote mpaka zile nguo alizopatia ajali yaani sijui itakuwaje,” ndugu mmoja alimueleza Papaa Pierre ambaye ni baba mlezi wa Mafisango.

Lakini wahudumu wa ndege iliyosafirisha mizigo hiyo wameahidi kwamba leo Jumapili huenda nguo hizo zikapatikana kama kweli zilikwama Nairobi.

Wakati huo huo, Haruna Moshi aliyesindikiza mwili wa marehemu, alizuiwa kwa zaidi ya nusu saa na maofisa wa uhamiaji ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kinshasa kwa madai kuwa pasi yake ya kusafiria si halali.

Maafisa hao walikuwa wakidai pasi hiyo ya dharura anayotumia Boban hairuhusu kuingia nchini Congo bali kwenye nchi za Afrika Mashariki lakini baadaye wakalainika na kumruhusu.

“Huyu anarudi Dar es Salaam hawezi kuingia Congo na hii karatasi nyie ondokeni, huyu gari lile pale anarudi nalo mpeni kila kilicho chake,”alisema Afisa mmoja akimwambia mkuu wa msafara wa Simba Mzee Kinesi.

Lakini baadaye maafisa hao walipoona picha za Boban kwenye magazeti ya Tanzania yaliyoripoti ajali ya Mafisango walilainika na kuamua kumruhusu Boban aingie ingawa alishachanganyikiwa na kutaka kulia huku akigoma kwenda licha ya kwamba askari hao haswa wa kiume walimsukuma mara kadhaa.

“Sasa mimi niende wapi wakati ubalozi wenu umenipa visa na kuniruhusu nije kuwawakilisha wachezaji wenzangu kwenye mazishi ya ndugu yetu,”alisikika Boban akimwambia askari mmoja.

Hata hivyo baadhiya askari walisikika waziwazi wakiomba kitu kidogo ili wamuachie Boban apite kwani alisahau hata karatasi yake ya chanjo jijini Dar es Salaam.

Saturday, May 19, 2012

FAHARI YA AFRICA: DIDIER DROGBAAAAAAAAAA - APIGA GOLI NA KUIPA CHELSEA UBINGWA WA KWANZA WA ULAYA

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji lake la kwanza la michuano ya klabu bingwa ya Ulaya tangu kuanzishwa kwake. Chelsea wamekuwa mabingwa baada ya kuwafunga Bayern Munich katika mchezo wa fainali kwa mikwaju ya penati 4-3. Kwa maana hiyo Chelsea ndio inakuwa klabu ya kwanza kutoka katika jiji la London kubeba kombe la UEFA Champions league.

Shujaa wa Chelsea Didier Drogba - fahari ya Afrika




Baada ya kutumia zaidi ya paundi billioni moja kwa matumizi ya kununua wachezaji pamoja na kuwalipa mishahara na matumizi mengine tangu kuinunua klabu ya Chelsea - hatimaye leo mmiliki wa The Blues Roman Abramovich ametimiza ndoto yake ya kubeba taji la ulaya.

BAYERN YENYE SAFU KALI YA USHAMBULIAJI NA BEKI MBOVU DHIDI YA CHELSEA YENYE PENGO KUBWA LA RAMIRES: FAINALI ISIYOAMULIKA KIRAHISI

Ni fainali ambayo inatawaliwa na hadithi ya timu zote mbili kuwakosa wachezaji muhimu, Chelsea ikiwakosa wanne na Munich ikiwakosa watatu.
Ni fainali inayofanyika kwenye uwanja wa nyumbani wa timu inayoshiriki mchezo wa fainali jambo ambalo linatokea kwa mara ya kwanza kwneye kizazi hiki .
Bayern Munich moja kwa moja wanaingia kwenye mchezo kama timu yenye nafasi kubwa ya kushinda . Ukiangalia baadhi ya factor nyingi za ushindi ziko upande wao. Ukiangalia wachezaji watakaowakosa ni tofauti na wale watakaokosekana na Chelsea. Munich itawakosa Luis Gustavo, David Alaba na Olger Badstubber.
Moja ya matatizo makubwa ya Bayern Munich ni kwenye defense na hii ni kwa sababu tofauti na ilivyo Chelsea na timu nyingine toka England ambazo huanza kujengwa tangu nyuma kwenye defense, Bayern Munich ni timu ambayo imeanza kujengwa kwenye safu ya ushambuliaji ambako ndio hasa ilipo nguvu yake kuu.
Mario Gomez akisaidiwa na kina Toni Kroos,Thomas Mueller, Arjen Robben , Franck Ribery na Bastian Schweisteiger wote wamekuwa msaada mkubwa kwa Bayern wakati ikiwa inashambulia na ndio maana wakati mwingine mapungufu ya Bayern kwenye defense yanashindwa kuonekana.
Hata hivyo defense ya Bayern Munich ambayo imekuwa kwenye wakati mgumu mara nyingi imekuwa ikisaidiwa na wachezaji watakaokosekana leo ambao ni Alaba, Badstubber na Gustavo .
Kukosekana kwa wachezaji hawa kutailazimu Bayern pengine kuwatumia Anatoly Tymoschuk ambaye ni midfielder mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kati , Philip Lahm huenda atatumika kwenye mojawapo kati ya pande mbili za safu ya ulinzi kwa maana ya kushoto au kulia huku Bastian Schweinsteiger akilazimika kushuka chini kucheza kama kiungo mkabaji .
Bayern ni timu ambayo ina mabao mengi ndani yake huku Mario Gomez akiwa katikati ya mipango yote ya ufungaji . Ukitazama takwimu za msimu huu a ligi ya mabingwa zinaonyesha kuwa Bayern Munich ni moja ya timu tatu zilizofunga mabao mengi tangu hatua ya makundi hadi kufika fainali .
Ukiitazama Chelsea ambayo itacheza leo ndio unapata taswira halisi ya jinsi walivyo kwenye wakati mgumu wakicheza na Bayern. Pengo la Ramires ni kubwa pengine kuliko mapengo ya wachezaji wote watakaokosekana kwenye line up ya Chelsea leo. Ukitazama kazi aliyoifanya ya kupunguza threat ya Dani Alves kwenye mchezo wa nusu fainali halafu jiulize umuhimu gani angekuwa nao kwa kumzuia mmojawapo kati ya Arjen Robben na Franck Ribery.
Ukiachilia mbali kazi ya kukaba Ramires ametokea kurekebisha sehemu muhimu ya mchezo wake ambayo ni ufungaji wa mabao muhimu kama alivyofanya kwenye nusu fainali dhidi ya Barca na hata kwenye fainali ya kombe la FA .
Branislav Ivanovic naye atakuwa pengo kubwa sana kwa Chelsea. Ivanovic ni beki mwenye umuhimu wa aina yake kwa Chelsea hasa ukizingatia kuwa Terry hatakuwepo na Gary Cahill na David Luiz hawana match fitnesss . Bahati mbaya naye ni mchezaji mwingine anayeingia kwenye orodha ya watu watakaokosekana hii leo . Ukabaji wake wenye nidhamu ya ufundi hali wa jukumu la beki pamoja na mabao yake muhimu ambayo hufunga akipanda ni jambo ambalo linafanya kukosekana kwake kuwe mazingira magumu kwa Chelsea .
Raul Meireles ni jina lingine ambalo Chelsea italikosa, Meireles ni kiungo ambaye hutimiza jukumu analopangiwa na kocha na hulifanya kwa asilimia mia moja hamsini . Work Rate yake ni kubwa, na ana uwezo wa ziada ambao kocha yoyote huhitaji kwenye timu .
Wachezaji hawa watatu wanaifanya kazi ya Chelsea kuwa ngumu kwa kuwa wametokea kuwa misingi muhimu ya kikosi cha Chelsea chini ya Roberto Di Matteo ambapo timu hii imekuwa ikishinda mechi nyingi kwa kufanya kazi na kutumia nafasi chache ambazo zinapatikana .
Moja ya mambo ambayo yataamua mchezo wa fainali kwa Chelsea ni mfumo watakaotumia. Endapo wataamua kupaki basi kwa staili waliyoifanya dhidi ya Barca watadhurika kwa hakika kwa kuwa Bayern Munich ni timu ambayo haina matatizo ya kiufundi ambayo yanaonekana kuidhuru Barca . Bayern tofauti na Barca ina mpango mbadala pale mpango wake wa msingi unaposhindikana . Ukipaki basi Bayern wanao wachezaji ambao watawatumia kwa kupiga mashuti ya mbali kama Schweisteiger, Kroos, Lahm na Thomas Mueller . Ukiamua kuwaelekeza mabeki au viungo wawili dhidi kucheza kwa kumkaba mmojawapo kati ya Robben na Ribbery Bayern watatumia shimo litakalobaki katikati ya uwanja kukudhuru na kama Chelsea watakuwa wakiokoa kwa kuwapa Bayern Umiliki wa mpira kwenye set pieces pia watadhurika kwa kuwa Bayern wanafunga kupitia ste pieces kwa kuwa wanae aina ya mshambuliaji ambaye Barcelona walimkosa ambaye ni Mario Gomez na hata Chelsea wakiridhika na kutafuta sare ili wajaribu bahati ya kwenye penati historia inaonyesha kuwa timu za ujerumani ni hatari sana kwenye penati kama walivyotambua Real Madrid kwenye nusu fainali.
Hata hivyo Chelsea wamekuwa wakicheza vizuri wakiwa under pressure hasa kutokana na kuridhika kuwa under dog kwenye michezo kadhaa msimu huu.
Rudi kwenye mechi ya Barcelona na utagundua hilo. Haya yote hayamaanishi kuwa Chelsea hawana nafasi kwani bado wanae Didier Drogba ambaye ni mshambuliaji wa mechi kubwa . Wanaye Fernando Torres ambaye anabaki kuwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuziona nyavu .
Itakuwa fainali ngumu na isiyoamulika kirahisi , dakika 90 zitaamua bingwa wa ulaya msimu .

ZANTEL MDHAMINI MPYA WA BONGO STAR SEARCH


Makamu wa Rais wa Kampuni ya Etisalat, Ahmed Mokhles akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampuni yao kudhamini shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, kulia kwake ni mkurugenzi wa Benchmark Productions iyoandaa shindano hilo, Rita Poulsen.
Shindano la BSS mwaka huu litajulikana kama ‘Epiq Bongo Star Search’ ambapo mshindi atanyakua shilingi milioni 50,pamoja na zawadi nyingine kutoka Zantel, sambamba na mkataba wa kurekodi ili aweze kuendeleza kipaji chake baada ya shindano hilo. Aidha, mchakato wa mwaka huu utawahusisha washiriki kutoka mikoa nane tofauti ikiwemo Zanzibar, Lindi, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam ambapo mchakato utaanza mwezi Juni.

IKIWA BAYERN WATABEBA KOMBE LEO HAPA NDIPO WATAKAPOSHEREHEKEA UBINGWA WAO



HII NI SEHEMU YA KUOMBA MATAMANIO YAKO YAKAMILIKE

MTANZANIA MULUMBU:CHELSEA WANA NAFASI KUBWA YA KUBEBA KOMBE LEO -ATOA USHAURI KWA WABONGO


Leo nimekutana mtanzania bwana Mulumbu ambaye nimepiga nae story tofauti kuelekea mechi ya leo usiku.


Shafih: Unauzungumziaje mchezo wa leo usiku kati ya Bayern vs Chelsea?



Mulumbu: Mchezo utakuwa mgumu sana lakini naipa nafasi Chelsea kwa sababu Bayern wana tataizo la defense, wanawakosa mabeki wao muhimu kama akina Alaba ambao wana uzoefu kiasi, pia waliopo kama replacement bado hawana uzoefu wa kupambana na deadly strikers kama Didier Drogba na Fernando Torres.



Shaffih: Chelsea nao watawakosa wachezaji wao muhimu kama John Terry, Ramirez na Meireles, huoni kama na wenyewe wana pengo kubwa?

Mulumbu: Utofauti kati ya Bayern na Chelsea kwa wachezaji, ni kwamba atleast kwa Chelsea wabadala kama wa akina Terry wana uzoefu, mtu kama Essien kila mtu anafahamu uwezo wake na uzoefu, David Luiz na Gary Cahil wamecheza kwenye level ya juu kwa muda mrefu sasa. Halfu kitu kingine Chelsea wataingia kwenye mchezo wakiwa wana presha ndogo sana ukiwafananisha na Bayern, hivyo hiyo ni advantage nyingine kwao.

Shaffih: Tangu nifike hapa nimegundua kwamba mashabiki wengi wa hapa wanaonekana kutoisapoti Bayern. Hii ni kwanini?

Mulumbu: Hapa Munich mashabiki wamegawanyika kutokana na timu zilizopo hapa, kama ilivyo nyumbani pale Dar es Salaam Uyanga na Usimba, na hapa kuna timu mbili kubwa Bayern na TSV 1860 Munich - hivyo kwa mtazamo mashabiki wengi wa hapa ni wa timu ya TSV 1860 na ndio maana unaona hali hiyo.


Shaffih: Unazungumziaje soka la nyumbani na ushauri kwa watanzania.

BAADA YA TIKETI KUISHA - UWANJA WA ZAMANI WA BAYERN WAFUNGULIWA NA KWA AJILI YA KUONYESHA MPIRA KWENYE BIG SCREENS


Pamoja na tiketi za bei chini kabisa kuuzwa kwa EURO 2000 tena ukiwa unakaa kwenye siti za nyuma ya goli, leo hii mamlaka ya jiji la Munich wameufungua uwanja wa Olympia Stadium uliokuwa ukitumiwa na Bayern Munich kabla ya kuhamia Allianz Arena, kwa ajili ya matumizi ya kuonyeshea mpira wa leo katika uwanja huo.




Olympia leo pametengenezwa kwa kuwekwa TV screens kubwa ambazo mashabiki zaidi ya 60,000 watakaa na kuangalia mtanange kati ya Chelsea na Bayern Munich. Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba kwenye uwanja huo pia napo pameshajaa na tiketi zote zimeshauzwa.

KUTOKA MUNICH: POMBE NDIO KINYWAJI KINACHOONGOZWA KUTUMIKA HAPA

Katika siku mbili nilizokaa hapa Munich nimegundua watu hapa hasa mashabiki wa soka wanapenda sana kunywa pombe.
Pombe ndio kinywaji wanachopenda sana watu wa hapa, mitaani mpaka viwanjani utawakuta watu wameshikilia maglassi ya pombe.

REDONDO NA CHUJI WAZUNGUMZIA PATRICK MAFISANGO

Kiungo wa Azam, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema kifo cha Patrick Mafisango ni pigo kubwa kwake kutokana ndiye alimtaka aondoke Maisha Club ili akalale muda mfupi kabla ya kifo chake.

Redondo aliyekuwa na marehemu Mafisango kwenye ukumbi wa Maisha Club hadi saa 7 usiku ambako Mafisango alimtaka aondoke kwa madai kuwa muda ulikuwa umekwisha.

Akizungumza kwa shida kutokana na kuelemewa na uzito wa msiba huo alisema haelewi ni nini kimetokea na kwa nini alimfukuza pengine wangekuwa wote kwenye safari ya kurudi.

"Tulikuwa wote hadi mwisho kwenye ukumbi wa maisha klabu, lakini ilipofika muda ya saa saba nane kasorobo Mafisango alinifukuza na kunichukulia taxi nirudi nyumbani na kuniaambia muda umeisha yeye atarudi na jamaa zake ambao alikuwa nao akiwemo mtoto wa dada yake,"alisema na kuongeza

"Nilikubali nikaondoka cha kushangaza napata taarifa alfajiri kuwa Mafisango amefariki Mungu amefanya kazi yake kumchukua, lakini mimi imeniathiri kutokana na mambo mengi niliyoongea nae"alisema na kushindwa kuendelea kuongea.

ATHUMANI IDD CHUJI

"Unafahamu wapo wachezaji wengi wa kigeni wanaocheza soka nchini na waliowahi kucheza soka nchini na kuondoka, lakini sikuwahi akuona mchezaji wa kigeni aliyekuwa akipendwa na wachezaji kama yeye,"alisema Chuji.

Alisema," Mafisango alipendwa na wachezaji wa timu tofauti za Ligi Kuu hasa walipokutana naye nje ya uwanja, alikuwa anapenda kuishi maisha ya kawaida tu na wachezaji wengi walikuwa wakimchukulia kama Mtanzania ila lafudhi yake tu.

PICHA: TIKETI ZINATAFUTWA KWA TAABU HAPA MUNICH

EURO 2000 - NI ZAIDI YA MILLIONI 3 ZA KIBONGO. MZUNGU YUPO TAYARI KUTOA KWA AJILI YA KUINGIA ALLIANZ ARENA.

Friday, May 18, 2012

NIMEKUTANA NA WAKONGO HAPA: WATHIBITISHA TIKETI KUUZWA EURO 1500-2500 LEO HII

Kama ambavyo niliripoti muda mfupi uliopita kuhusu upatikanaji wa tiketi kwa ajili ya kuangalia fainali ya champions league zilivyo ghali na shida kupatikana - jioni hii nikiwa kwenye matembezi yangu nimekutana na jamaa wawili raia wa Kongo ambao wamekuja hapa Munich kwa madhumuni ya kuangalia mtanange wa kesho kati ya Chelsea na Bayern Munich. Wakongo hawa wamenithibitishia kwamba ni kweli leo kuna baadhi ya sehemu ambazo ni chache sana zimebakiwa na tiketi lakini wanauza kwa EURO 1500 -2500 ambazo ni tiketi za hadhi ya juu.



KUTOKA MUNICH: IJUE KIUNDANI HISTORIA NA MAANA YA TIMU YA BAYERN MUNICH

HAPA NDIPO PATAKAPOAMUA BINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE 2012 - ALLIANZ ARENA - IJUE HISTORIA YAKE.

Allianz Arena ni uwanja wa kuchezea soka uliopo kusini mwa Munich, Bavaria - Ujerumani. Huu ni uwanja unaotumiwa na timu mbili za mji wa Munich FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen kuchezea mechi zao za nyumbani kuanzia msimu wa 2005-06. Timu mbili zote zilikuwa zikicheza mechi zao za nyumbani kwenye uwanja wa Munich Olympic tangu mwaka 1972. Allianz Arena ni uwanja wa tatu kwa ukubwa nchini Ujerumani nyuma ya Signal Iduna Park mjini Dortmund na Olympiastadion mjini Berlin. Uwanja huu ulifunguliwa mwaka 2005, mwezi Mei 30. Ulijengwa kwa na gharama zisipungua Euro million 340 na kampuni ya Allianz ambayo wana haki ya kutumia jina lao kwenye uwanja huo kwa miaka 30. Uwanja una uwezo wa kuingiza watu 69,901.

RIPOTI KUTOKA MUNICH: HAPA NDIPO WALIPOFIKIA CHELSEA

BAYERN MUNICH WANATENGENEZA FEDHA NYINGI SANA KWA MAUZO YA JEZI

FAINALI YA MABINGWA WA ULAYA: TIKETI ZAPANDA MPAKA EURO 1500 -2500 ZA KIBONGO NA BADO ZAKOSEKANA

Football is business.......
Wakati jana nafika hapa Munich tiketi za mchezo wa fainali ambazo kwa jana tu zilikuwa zikipatikana kwa taabu, leo zimepanda bei maradufu kutoka Euro 1500 kwa jana mpaka EURO 2500 leo hii.

Katika hali ya kushangaza pia tiketi hizo za EURO 2500 ambazo kwa haraka haraka ni kama shilingi millioni 4 za kitanzania, nazo zimeisha hivyo kusababisha uongozi wa jiji la Munich pamoja UEFA kuchagua sehemu maalum ambazo zimetengenezwa na kuwekwa Big screens.


Sehemu hizo pia nazo zimejaa na kuwa sold out kwa maana tiketi zote nazo zimeisha. Kwenye mabaa na pub nyingine nyingi hapa Munich ambazo huonyesha mipira napo kumekuwa sold out. Ni watu wengi inaonekana watakosa nafasi ya kuangalia mechi hii uwanjani.
Huyu mzungu ni mmarekani ambaye amesafiri kutoka Califonia kuja kuangalia fainali lakini amekosa tiketi.

Kwa mfano nikiwa kwenye matembezi yangu leo nilikutana na Jamaa mmoja raia wa Marekani ambaye ambaye amesafiri kutoka Califonia mpaka Munich lakini maskini ya mungu amekosa tiketi.


Kiukweli mpaka sasa kila sehemu ni Champions league final ndio kitu kinachotawala. Nimejifunza namna wenzetu wanavyoandaa matukio ya kuyafanyia promotions ya kutosha na ndio maana ni vigumu kwa matukio yao kufeli na mwisho ndio maana wanakuwa wanafanya biashara kubwa na kuwa matajiri.

KUTOKA MUNICH: MTANZANIA DJ MAX AMBAYE NI SHABIKI WA KUTUPWA WA BAYERN MUNICH

DJ Max mtanzania ambaye anaishi Munich. Huyu ndio mwenyeji wangu ambaye ananisaida kunitembeza mjini hapa na kuelekeza juu ya vitu tofauti kuhusu mechi hii pamoja na mambo mengine.

Hapa tukiwa wote nje ya jengo la hoteli waliyofikia klabu ya Chelsea wakati huu wakiwa hapa kwa ajili ya mechi ya fainali ya Champions league. Hii ni hoteli ya hadhi ya juu sana hapa Munich, Bayerischer Hof ni hotel ambayo huwa wanakaa mastaa wakubwa duniani wanapofika katika mji wa Munich.

JAY JAY OKOCHA AWAPA NAFASI BAYERN HUKU KAREMBEU AKITOA NAFASI KWA CHELSEA

Nikiwa na Jay Jay Okocha ambaye amesema kwa hali anavyooiona ni dhahiri anawapa nafasi Bayern Munich kuchukua ubingwa wa ulaya.

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa Christian Karembeu yeye ameniambia Chelsea kesho watabeba kombe.

MASIKINI BOBAN: KIFO CHA MAFISANGO KIMEMUUMIZA MNO - WALIKUWA MARAFIKI WAKUBWA SANA.

Haruna Moshi Boban akiwa mwenye huzuni mkubwa leo wakati wa kuaga mwili wa Mafisango. Pole Boban mwenyezi mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. (Picha kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/)
Pamoja na kuwa ni wengi tumeumizwa na msiba wa aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba Patrick Mafisango Mutesa, lakini ni dhahiri wachezaji wenzie wa Simba wameumizwa zaidi hasa rafiki yake kipenzi Haruna Moshi Boban.
Haruna Moshi Boban akiwa na huzuni tele leo hii wakati wa kumuaga Patrick Mafisango.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba kwa takribani masaa 24 tangu kifo cha Mafisango kitokee Haruna Moshi ambaye wengi wetu tunamjua kama kama nunda na mtu mwenye aibu sana lakini kufuatia msiba huu wa Mafisango, Boban amekuwa mtu mwenye huzuni sana kiasi cha kushindwa hata kula.
Emmanuel Okwi akiaga mwili wa Patrick Mafisango.
"Kiukweli msiba wa mwenzetu umetumuumiza sana, lakini Haruna umemuuma zaidi kwa kuwa Mafisango ndio alikuwa rafiki yake mkubwa kuliko wachezaji wote ndani ya Simba. Mafisango na Boban pale Simba walikuwa kama mapacha, yaani muda wote hata tukiwa kambini utawakuta pamoja. Kwa mfano hata tukiwa tumeenda safari kwa ajili ya mechi mara zote wenyewe walikuwa wakilala pamoja, kiukweli walikuwa wakipendana sana na ndioa maana haishangazi kumuona Boban kwenye hali ile." - alikaririwa akisema Emmanuel Okwi kupitia mawasiliano ya mtandao wa BBM.

No comments: