Tuesday, May 15, 2012

DI MATTEO KUWAPANGA PAMOJA DROGBA NA TORRES JUMAMOSI NA BAYERN MUNICH


EPL - Chelsea v Newcastle United, Didier Drogba, Fernando Torres and Frank Lampard
Drogba kushoto, Torres na Lampard kulia

Getty Images
KOCHA wa Chelsea, Roberto Di Matteo anaweza kuwapanga pamoja katika safu ya ushambuliaji Fernando Torres na Didier Drogba wacheze pasha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi wiki hii, baada ya kuwajaribu wawili hao katika mechi na Blackburn Rovers mwishoni mwa wiki.

Wapachika mabao hao wawili, hawajawahi kuanza pamoja chini ya Mtaliano huyo katika kipindi chake cha miezi miwili ya kuwa kazini na kocha huyo wa zamani wa West Brom amesema atawaweka pamoja Jumamosi dhidi ya Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena.
"Nimejaribu vitu vichache ili kuwa mtazamo mpya na kuona itafanyaje kazi. Wakati wote ni ngumu, kwa sababu ni wazi itakuwa nafasi tofauti," alisema. "Lakini nimekuwa nikijaribu kubadilisha vitu vichache."
Wawili hao wote wamejaribu kuzinduka mwishoni mwa msimu na wote wamefunga mabao muhimu katika mechi ngumu, Drogba alifunga kwenye fainali ya Kombe la FA wakati Torres alifunga bao la dakika za mwishoni Uwanja wa Camp Nou lililoipeleka The Blues fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Huku viungo Ramires na Raul Meireles ikifahamika wataikosa mechi hiyo, Di Matteo anaweza kabisa kuimarisha kikosi chake kuwa mpanga Drogba na Torres mbele.

GARY NEVILLE AINGIA THREE LIONS NA KIKOSI CHAKE


Gary Neville England
Goal.com
BEKI wa zamani wa Manchester United, Gary Neville ametajwa kama Msaidizi wa kocha Roy Hodgson katika kikosi cha England leo mchana, akisaini mkataba wa miaka minne na FA.Baada ya mwaka uliopita kufanya kazi kama mchambuzi wa TV ya Sky Sportstangu astaafu soka mwaka 2011, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37, amelamba dume kuingia kwenye benchi la ufundi la Three Lions.
Sign up with bet365 for a free bet up to £200
Uteuzi huo unakuja siku chache tangu ateue kikosi chake kwanza cha Three Lions, wakati akifanya kazi yake ya uchambuzi kwenye TV katika mchezo kati ya Liverpool na Tottenham Jumatatu, ulioisha kwa sare ya bila kufujngana.
Katika kikosi hicho, ameteua wachezaji watatu tu wa timu yake, wakiwemo Phil Jones na Chris Smalling ambao kwa sasa ni majeruhi katika safu ya ulinzi na mchezaji mwenzake wa zamani wa United, Rooney akiongoza kikosi.
Tazama kikosi kamili cha Neville hapo juu.

AJISHINDIA PIKIPIKI VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO YA SBL

Meneja wa bia ya Serengeti Premeum Lager, Allan Chonjo akimkabidhi kadi ya usajili wa pikipiki kwa mshindi wa Vumbua hazina chini ya kizibo Ibrahim Kimambo
Mshindi wa pikipiki katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti, Ibrahim Kimambo akiwasha pikipiki



BALOTELLI APUUZA PATI LA TIMU, ATOKA KIVYAKE NA MASELA WAKE


Mario Balotelli
Mchezaji wa timu? ... Mario Balotelli akiwa na mdogo wake Enoch, kushoto, na mshkaji wao
t: EAMONN & JAMES CLARKE
Published: Today at 12:53

MARIO Balotelli alipuuza pati la Manchester City kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu England na kuamua kutoka kivyake usiku wa jana.

Mtaliano huyo alikataa kwenda pati la chakula cha usiku kilichoandaliwa maalum kwa pamoja na timu na kufanya mtoko kivyake na mdogo wake Enoch.
Kiwa amevaa kofia flat, mshambuliaji huyo alikwenda kwenye klabu la Kitaliano, San Carlo wakati wachezaji wenzake na kocha walienda kusherehekea ushindi wao unaokuja baada ya miaka 44 Hilton Hotel.
Hii si mara ya kwanza kwa Mario kupuuza sherehe za klabu baada ya ushindi mkubwa.

Mei mwaka jana alipuuzia sherehe za City baada ya kutwaa Kombe la FA.
Roberto Mancini
Kocha wa City, Roberto Mancini kushoto
BIGPICTURESPHOTO.COM
Pia alishindwa kutokea kwenye sherehe za tuzo za msimu za klabu hiyo, zilizoambatana na chakula cha usiku, japo alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Gareth Barry and his wife Louise
Party ... Gareth Barry na mkewe Louise

David Silva


Mchezaji tegemeo ... David Silva
XPOSUREPHOTOS.COM

Micah Richards
Micah Richards
XPOSUREPHOTOS.COM

Vincent Kompany and his wife Carla
Vincent na mkewe Carla
EAMONN & JAMES CLARKE

Liam Gallagher and Ricky Hatton with Vincent Kompany
Mashabiki maarufu City... Liam Gallagher na Ricky Hatton wakiwa na Vincent Kompany
steve allen




Mario Balotelli
Kachaa... Balotelli akimpuuza shabiki wa kike anayejipendekeza

No comments: