Tuesday, May 15, 2012

MANCINI AMUOMBA RADHI FERGUSON


Carlos Tevez

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amemuomba radhi kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa kitendo ch mshambuliaji wake, Carlos Tevez kubeba bango la R.I.P. Fergie katika kusherehekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England jana.

WENGER, CEO ARSENAL WAMUITA FARAGHA VAN PERSIE


Arsenal striker Robin van Persie
14 May 2012Last updated at 22:21 GMT

MSHAMBULIAJI Robin van Persie wa Arsenal, kesho anatarajiwa kuwa na kikao kizito na kocha wa klabu yake, Arsene Wenger na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis kuzungumzia mustakabli wake kwa Washika Bunduki hao.

Majadiliano hayo, yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Wenger, kuanzia saa 4:00 kwa saa za Uingereza.
Uamujzi wa mwisho utachukuliwa kabla ya kutajwa kwa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi Alhamisi, kinachotarajiwa kushiriki Euro 2012 na Van Persie anatarajiwa kuwamo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake, amemaliza msimu na mabao 41 katika mechi 53 za klabu na nchi yake.
Akiwa amefunga mabao 37 katika 48 za Arsenal na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa mabao yake 30 kwenye mechi 38, Van Persie sasa amegeuka lulu na klabu nyingi kubwa Ulaya zinataka kumsajili

MAN CITY YATANGAZA OFA RASMI KWA VAN PERSIE


Van Persie

Gossip logo
14 May 2012Last updated at 23:00 GMT

Tetesi J'nne Magazeti ya Ulaya

MAN CITY HAITANII KWA VAN PERSIE, INAMTAKA KWELI...

MABINGWA wapya wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wako kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie kwa dau la pauni Milioni 25, wakimuahidi mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.
BAHATI iliyoje kwa Arsenal, mchezaji wao mpya, Lukas Podolski amesema kwamba atakuwa akicheza washambuliaji watatu katika nafasi moja katika kikosi cha washika Bunduki wa London msimu ujao.
Robin van Persie
Van Persie aliigharimu Arsenal pauni Milioni 2.75, akitokea Feyenoord ya Uholanzi mwaka 2004
KLABU ya Manchester United imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski, baada ya mazungumzo yake na klabu yake juu ya mkataba mpya kufa. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland, mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 30 msimu huu.
KIUNGO wa Lille, Eden Hazard amesema kwamba atajiunga na klabu ya Manchester msimu huu. Hata hivyo, Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 21 hakusema itakuwa ipi kati ya City au United.
KLABU za Chelsea na Liverpool zinaelekea kumkosa kiungo wa Sao Paolo ya Brazil, Lucas Moura, kutokana na Inter Milan kuonekana wameingia kwa gia kubwa zaidi katika vita ya kuwania saini ya kinda huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 19.
KLABU ya West Brom inabangua bongo kama imsajili moja kwa moja, kipa Ben Foster anayewadakia kwa mkopo au la. Mchezaji huyo Bora wa Mwaka wa The Baggies, anatarajiwa kurejea timu ya Daraja la Kwanza, Birmingham msimu huu.

DALGLISH OUT LIVERPOOL

KOCHA wa Liverpool, Kenny Dalglish amekwenda Boston kupambana kupigania ajira yake, kufuatia tetesi kwamba kocha wa Wigan, Roberto Martinez anaweza kuchukua nafasi yake Anfield.
Roberto Martinez
Martinez
Martinez nimtu anayetakiwa, na Aston Villa inaaminika kumuweka Mspanyola huyo na kocha wa Norwich, Paul Lambert katika orodha ya makocha inaowataka kurithi mikoba ya Alex McLeish iliyemfukuza.
MARADONA
GWIJI wa Argentina, Diego Maradona amesema alifurahia taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, ambalo walilitwaa Manchester City, akisema; "Kwa moyo wangu wote". Bao la ushindi la City dhidi ya QPR, lilifungwa mkwewe, Sergio Aguero aliyemuolea binti yake.

 

HIZI NDIZO SERA ZA BIN ZUBEIRY, MIGOGORO HAIPEWI NAFASI


Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika Kombe la Challenge na mkewe, mama Salma, ambalo timu ya Bara ilitwaa mwaka juzi. Kwa staili ya migogoro ni ndoto za alinacha kutarajiwa mafanikio kama haya tena nchini. Migogoro ni kitu kinachomkera hadi rais wetu, aliye mstari wa mbele katika kusapoti michezo nchini, kiasi kwamba katika siku za karibuni anaonekana kama anaanza kujitoa taratibu. Tuamua sasa kuitenga migogoro ili tuinue soka yetu, au tuendelee kuibeba ili tudumaze kandanda yetu.

NIKIWA mwandishi wa muda mrefu, niliyelelewa katika misingi na maadili ya kitaaluma, napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba, sitoi kipaumbele kwa habari za migogoro kwenye blog yangu.
Nasikitika, sitakuwa naandika habari yoyote ya mgogoro- nikiamini kabisa wakati umefika Watanzania tunapaswa kubadilika na kuachana na desturi hiyo, badala yake kufikiria namna ya kujiletea maendeleo.
Lazima tukubali kukabiliana na changamoto- kwa kufuata misingi ya sheria na katiba- badala ya kuweka mbele vurugu na uvunjaji wa sheria.
Kwa sababu hiyo, tunaanzia na huu mgogoro wa Yanga unaoendelea hivi sasa, BIN ZUBEIRY haitaupa nafasi. Sera kubwa ya BIN ZUBEIRY ni kuandika habari za maendeleo, kuelimisha na kuburudisha wasomaji wake.
Siwezi kuingilia uhuru wa blogs nyingine- au magazeti hata Radio na Televisheni, lakini kwangu narejea kwenye mafundisho na uzoefu nilioupitia chini ya magwiji wa taaluma ya Habari nchini, nikiwa mfanyakazi wa kampuni ya Habari Corporation (sasa Neww Habari) tangu 1998 hadi nilipoacha kazi Mei 1, mwaka huuu.
Nasema, BIN ZUBEIRY ni kwa habari za maendeleo, na si migogoro. Asanteni. Mungu ibariki Tanzania, bariki sekta yetu ya michezo, iwe na amani mafanikio. Amin.

YONDAN, NIZAR KHALFAN WATUA YANGA

Kelvin Yondan

Nizar Khalfan
KLABU ya Yanga imefanikiwa kunasa sahihi ya beki wa Simba Kelvin Yondan, kwa ajili ya
kuichezea timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Gazeti la Habari Leo limeandika kwamba, habari za uhakika zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka ndani ya Yanga, zilidai kwamba Yondan amesaini mkataba wa miaka miwili.
“Tayari tumeishasajili wachezaji wawili ambao ni Nizar Khalfan mwaka mmoja na Yondan, bado wengine watatu wakiwemo wa kigeni,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza kwamba mlinda mlango namba moja Yaw Berko, naye ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na wameondoka jana na mshambuliaji Keneth Asamoah kwenda kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko.
Gazeti hili lilimtafuta Salum Rupia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga kuelezea suala la usajili wa Yondan lakini hakupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuita
bila majibu.
Aidha, alipotafutwa Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga, alisema kwamba hahusiki na mambo ya usajili, mambo yote ya usajili aulizwe Rupia.
“Nisingependa kuzungumzia mambo ya usajili, mambo ya usajili muulizeni Rupia ndiye anajua,” alisema Nchunga.
Hata hivyo Nchunga kwa sasa yuko kwenye shinikizo ambapo wanachama wa klabu hiyo wanamtaka ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kuiendesha klabu hiyo.
Yondani hakupatikana kuzungumzia, hilo kwa kuwa amesafiri na timu yake ya Simba Sudan na wanatarajiwa kurejea leo.
Kwa muda mrefu Yanga walikuwa wakimsaka Yondan bila mafanikio. Mchezaji huyo ameshawahi kuingia kwenye mgogoro wa mara kwa mara na mashabiki na viongozi wa Simba
wakidai kuwa ni mamluki wa watani wao hao wa jadi.

VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA


Ruud van Nistelrooy
ALL OVER ... Ruud van Nistelrooy has quit
Published: 14th May 2012

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy amestaafu soka.

Van Nistelrooy mwenye umri wa miaka 35, amekuwa katika wakati mgumu tangu amejiunga na Malaga akitokea Hamburg msimu uliopita, akifunga mabao matano tu katika mechi 32.
Licha ya ukame wake wa mabao, ameisaidia klabu hiyo ya Hispania kumaliza ndani ya Top-Four ya La Liga kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao na kufuzu kucheza Ligit ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi, alisema: “Jana ilikuwa siku yangu ya mwisho katika soka ya kulipwa. Nilitaka kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini ni wakati wa kuondoka.
“Nimefikia kwenye kiwango cha mwisho cha ubora na siwezi kucheza kwa kiwango kinachotakiwa. Siwezi kuagwa vizuri zaidi ya hivi,"alisema.
Van Nistelrooy alianzia soka nyumbani kwao na klabu ya Den Bosch kabla hajahamia Heerenveen na PSV Eindhoven, ambako alijijengea jina.
Baada ya kutwaa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu Uholanzi, Eredivisie Golden katika misimu ya 1998/99 and 1999/2000, alichukuliwa kwa bei mbaya na vigogo wa Old Trafford.
United ilimsajili Van Nistelrooy bila ya kujali kama alikuwa majeruhi wakati huo, akisumbuliwa na maumivu ya goti aliloumia mazoezini.
Van Nistelrooy alilipa fadhila kwa kolcha huyo Mscotland, kwa kumfungia mabao 150 katika mechi 219 ndani ya misimu mitano ya kuitumikia Manchester na kuipa taji msimu wa 2002/03.
Baadaye aliuzwa Real Madrid mwaka 2006, ambako alifunga mabao 53 katika misimu miwili, akiiwezesha Real kutwaa mataji mawili mfululizo ya La Liga.
Lakini akaumia tena na akaukosa karibu msimu wote wa 2008/09 na kuzidiwa kete na akina Raul, Gonzalo Higuain na Karim Benzema katika msimu uliofuata.
Alitimkia Hamburg ya Ujerumani alikocheza miezi 18 kabla ya kurejea Hispania kuchezea Malaga.
Van Nistelrooy pia amefunga mabao 35 katika mechi 70 za timu ya taifa ya Uholanzi— ikiwemo aliyofunga kwenye Euro 2004, Kombe la Dunia 2006 na Euro 2008 — na mfungaji bora wa pili kihistoria katika Ligi ya Mabingwa, akiwa ametikisa mabao 54 katika mechi 81.
Mechi yake ya mwisho ilikuwa kati ya timu yake, Malaga ambayo walishinda 1-0 dhidi ya Sporting Gijon.

SCHOLES ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED


Paul Scholes
PLAYING ON ... Paul Scholes
Last Updated: 15th May 2012

PAUL SCHOLES ataendelea kuichezea Manchester United msimu ujao.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 37, amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuendelea kukipiga Trafford.
Kocha wa Old Trafford, Alex Ferguson amesema: “Imefanyika. Anabaki.”
Ferguson alikuwa ana wasiwasi msimu uliopita ungekuwa wa mwisho kwa Scholes akiwa na jezi ya United na atakuwa na wasiwasi iwapo, iwapo atateuliwa kwenye kikosi cha Roy Hodgson kwa ajili ya Euro 2012, kwani amekwishapendekezwa.
Pamoja na hayo, kocha wa United anashawishika kuamini kiungo huyo atakuwa na moto ule ule msimu ujao katika kukibeba kikosi cha Mashetani Wekundu kwenye harakati za kurejesha taji.


MAN CITY WAMWAGIKA MITAA YA MANCHESTER, LILIKUWA BONGE LA PATI LEO


HAVING A BALL ... Man City celebrate their title with an open-top bus parade through Manchester
MAN CITY KATIKA PICHA TOFAUTI WAKISHANGILIA UBINGWA WAO
Published: Today at 19:04

MAN CITY walisherehekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England waliotwaa jana kwa kutembea mitaani na basi lao kubwa la wazi jioni ya leo katika Jiji la Manchester.

Mashabiki walimwagika mitaani kuwapongeza mashujaa wao huku wakipigiwa wimbo waThe Beatles, Hey Jude.
Vijana wa Roberto Mancini, walitwaa taji hilo kiaina yake wakipata mabao mawili dakjika za majeruhi na kushinda 3-2 dhidi ya QPR katika siku ya mwisho ya msimu.
TIME TO PARTY ... the celebrations in front of the clock tower

Wapinzani wao, Man Utd walifikiri wametwaa ubingwa baada ya kuifunga Sunderland 1-0 kwenye Uwanja wa Stadium of Light, wakati huo City wakiwa nyuma kwa 2-1 kabla ya mambo kubadilika.
IN GOOD KOMPANY ... captain Vincent lifts the Premier League trophy aloft
Nahodha Vincent akiwa ameinua Kombe
Lakini mpira wa kichwa uliopigwa na Edin Dzeko aliyetokea benchi uliisawazishia City dakika ya 92 kabla ya Sergio Aguero kufunga la ushindi sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho.
SHADY CHARACTER ... goalkeeper Joe Hart (left) gives the fans a wave
Kipa Joe Hart (kushoto) akipungia mashabiki
Lilikuwa taji la kwanza kwa City, ndani ya miaka 44 – tangu watwae la mwisho mwaka 1968.
CITY SLICKERS ... the players enjoy the glorious scenes

JUST CHAMPION ... City boss Roberto Mancini (left) and Kompany
Kocha Roberto Mancini (kushoto) na Kompany
STOPPING TRAFFIC ... a fan sits on a traffic light to join in the party

No comments: