Tuesday, April 24, 2012
SIKU SABA BAADA YA CHELSEA KUPIGA SHUTI MOJA NA KUPATA GOLI HUKU BARCA WAKIPIGA MASHUTI 24 BILA GOLI - TIMU HIZI MBILI ZINARUDAIANA LEO NOU CAMP - NANI KUTINGA FAINALI
Siku saba baada ya takwimu za shuti moja bao moja
kwa Chelsea na mashuti 24 bila mabao kwa Barcelona kwenye uwanja wa Stamford
Bridge, timu hizi zinarudiana kwenye uwanja wa Nou Camp.
Barcelona wamekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo huku nyota wake Lionel Messi akisindwa kung'aa kwenye kwenye mechi zote mbili.
Chelsea walipoifunga Barca mapema wiki iliyopita wengi waliona kuwa timu hii toka London imepanda baiskeli ya miti na Barcelona ingeshinda kiwepesi mchezo wa marudiano.
Hata hivyo kipigo cha kwenye El Classico kimewaweka
Barca kwenye hali tofauti ya kisaikolojia ambayo inaweza kuwa sababu ya aidha
kushinda au kufungwa kwenye mchezo wa marudiano.
Ukirudi nyuma na kutazama sababu ambazo zinaweza kuwa zimeipelekea Barca kufungwa michezo yote miwili na kuzichanganya kwa pamoja hapa ndio unapoweza kugundua hali ngumu waliyo nayo Barca hii leo.
Ukirudi nyuma na kutazama sababu ambazo zinaweza kuwa zimeipelekea Barca kufungwa michezo yote miwili na kuzichanganya kwa pamoja hapa ndio unapoweza kugundua hali ngumu waliyo nayo Barca hii leo.
Kwenye mechi ya jumatano iliyopita mfumo waliotumia Chelsea na bahati kwa pamoja viliwasaidia vijana wa Di Matteo. Mfumo aliotumia siku hiyo ulikuwa rahisi, kuta mbili za wachezaji wanne kila moja nyuma ya mpira na kujaribu kupunguza nafasi ya Barca kufaidi kumiliki mpira kuanzia katikati mwa uwanja kuelekea liliko lango la Chelsea.
Pamoja na hilo , Di Matteo aliwaelekeza viungo Raul
Meireles na John Obi Mikel kuhakikisha wanakufa na Lionel Messi ,Xavi na Andres
Iniesta huku Ramires akifanya kazi ya kuua mashambulizi ya upande wa kulia aliko
Mbrazil mwenzie Dani Alves.
Mbinu hizi zilifaulu kwa kusaidiwa na ari
waliyokuwa nayo Chelsea kisaikolojia pamoja na bahati iliyokuwa upande wao kwani
ukiachilia mbali jinsi Chelsea walivyoshinda huwezi kusahau mara ambazo Barca
waligongesha mwamba na mara ambazo Petr Cech alifanya kazi ya ziada kuokoa au
mabeki kina Ashley Cole wakiondosha hatari langoni mwao.
Kwenye mchezo dhidi ya Real , Barca waligharimiwa sana na kuwakosa watu mbadala wanaoweza kufanya kazi ya ufungaji zaidi ya Lionel Messi.
Huwezi kuacha kufikiri kuwa nafasi mbili alizopata
Christian Tello na kushindwa kuzitumia zingekuwa zimetumiwa vyema na mtu kama
Pedro au David Villa . Pengo la David Villa limeonekana sana kwenye El Classico
na kuna kila uwezekano kuwa endapo Chelsea watafuzu basi pengo hilo litaonekana
kwenye mchezo huo pia.
Pamoja na hayo Real walikuwa na aina ya uzoefu na
uwez wa kutumia nafasi chache za kufunga walizozipata jambo ambalo si timu
nyingi zinazocheza na Barca zinafanya. Ukiwaangalia Barcelona wenyewe kama
Barcelona kuna baadhi ya viashiria mbalimbali ambavyo vilionyesha kuwa hawako
mchezoni siku ya jumamosi.
Lionel Messi hana kawaida ya kuwa mlalamishi lakini
alilalama kwa waamuzi kuliko mchezaji yoyote siku ile na hata Xavi na wengineo
walikuwa wanaonekana kupagawa jambo ambalo linakufanya uhisi kuwa ile hali ya
woga ambayo timu pinzani inakuwa nazo ikicheza dhidi ya Barca inakuwa nayo
imehamia kwa Barcelona wenyewe.
Safu ya ulinzi nayo imekuwa tatizo kubwa . Carles Puyol anastahili kubeba lawama kwenye mabao yote matatu ambayo Barca imeruhusu kwenye michezo miwili iliyopita na endapo atacheza tena huenda Di Matteo akawaelekeza wachezaji wake kupeleka presha kwenye upande wake.
Hata hivyo Barcelona wanabaki kuwa timu yenye uwezo hata pale ambapo wanapitia kwenye kipindi kigumu kama livyokuwa kwenye msimu huu na quality yao pekee ambayo dhahiri shahiri ni bora kuliko ya Chelsea inaweza kutosha kugeuza matokeo.
Kikubwa kitakachoamua mchezo ni hali ya kisaikolojia ya wahezaji a Barcelona.
Wanapaswa kuacha yaliyotokea kubaki huko nyuma
yaliko na ku-deal na mchezo wa leo kama wa leo . Endapo wataruhusu kuingiwa na
hali ya woga kwa maana wanaweza kufungika kirahisi.
Kwa hali ya kawaida Barcelona ni washindi na hiki
ni kitu ambacho wahezaji wanaingia nacho uwanjani kwa kuwa wana "winning
mentality" . Ila hiyo hiyo mentality inaweza kuondoka na swali ambalo kila mmoja
anajiuliza ni kama hiyo winning mentality ipo baada ya michezo miwili migumu
ambayo Blaugurana wamefungwa?
Chelsea wana nafasi finyu ya kupata ushindi kwenye mchezo wa leo na nafasi pekee kubwa waliyo nayo ya kusonga mbele ni kutafuta bao la ugenini huku wakilinda kwa nidhamu kama waliyolinda nyo kwenye mchezo wa Stamford Bridge.
Tetesi toka kwenye magazeti ya Hispania kwa masaa 24 yaliyopita zimekuwa zikisema kuwa Lionel Messi hayuko kwenye physique nzuri , pengine michezo imekuwa mingi mfululizo pengine kama ilivyo kwa kila binadamu wachezaji wa Barcelona wamechoka baada ya kuwa na msimu ambao mambo yamekuwa magumu kwao?
Haya ni maswali ambayo majibu yake yatapatikana ndani ya masaa machache yajayo.
Monday, April 23, 2012
CHELSEA KULAMBA £10 MILLIONI WAKIWATOA BARCA NA KUCHUKUA UBINGWA WA ULAYA.
Wachezaji wa Chelsea wamehaidiwa na bosi wao
Roman Abramovich kupata bonasi ya £10 million ikiwa watafanikiwa kuifunga Barca,
kisha kwenda fainali na kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa ulaya
katika historia ya timu hiyo.
According to gazeti la The Sun la Uingereza ikiwa Chelsea watafanikiwa kuchukua kombe hilo watapewa kiasi hicho cha fedha huku manager wao wa muda Roberto Di Matteo nae hatoondoka mikono mitupu.
Kila mchezaji wa kikosi cha wachezaji 25 atapokea kiasi cha £350,000 ikiwa watafanikiwa kubeba kombe la ulaya pale Allianz Arena mwezi ujao.
Roberto Di Matteo ambayo bado hajapokea ongezeko la mshahara ukiachana na 1.2millionaliyokuwa akilipwa kwa mwaka kama kocha namba 2 nyuma ya Villas Boas.
Bonasi yake itajadiliwa katika kikao cha baina yake na mmiliki wa The Blues.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kiungo huyo wa zamani wa klabu atavuta mkwanja unaofikiwa paundi 500,000 kama shukrani kwa kugeuza msimu wa Chelsea - japokuwa bado hajapewa uhakika wa kupewa kazi ya moja kwa moja kama kocha mkuu.
Di Matteo amefungwa mechi moja tu tangu amrithi Villas Boas huku akiwa aemcheza mechi 14.

UKWELI NA UTHIBITISHO KWAMBA BARCELONA BILA MESSI HAKUNA KITU.
Katika mechi mbili za
hivi karibuni za Barcelona, mchawi wa soka wa sasa ulimwenguni Lionel Messi
hakufanikiwa kufnga goli - na Barcelona wakafungwa mfululizo na Chelsea na Real
Madrid. Lakini hawezi kufanya mabo yote peke yake.
Kiukweli tuache ubishi pembeni Muaregentina huyu ndio roho ya Barcelona, na mfano mzuri ni huu katika katika mechi nne ambazo Barcelona wamefungwa msimu huu Messi hakufunga kabisa ndani ya mechi na pia katika mechi 21 ambazo Lionel hakufunga matokeo hajawahi kuwa mazuri kwa Catalans.
Angalia ukweli huu.

WHEN MESSI HAS
FAILED TO SCORE IN
2011-12
|
RIVAL | COMPETITION | DATE | RESULT |
Real Sociedad | La Liga | Sep 10 |
2-2 |
AC Milan | Champions League | Sep 13 |
2-2 |
Valencia | La Liga | Sep 21 |
2-2 |
Sporting | La Liga | Oct 2 |
1-0 |
Viktoria Plzen | Champions League | Oct 19 |
2-0 |
Sevilla | La Liga | Oct 22 |
0-0 |
Granada | La Liga | Oct 25 |
1-0 |
Getafe | La Liga | Nov 26 |
0-1 |
Real Madrid | La Liga | Dec 10 | 3-1 |
Al Sadd | Club World Cup | Dec 15 | 4-0 |
Espanyol | La Liga | Jan 8 | 1-1 |
Osasuna | Copa del Rey | Jan 12 | 2-1 |
Real Madrid | Copa del Rey | Jan 18 | 2-1 |
Real Madrid | Copa del Rey | Jan 25 | 2-2 |
Villarreal | La Liga | Jan 28 | 0-0 |
Valencia | Copa del Rey | Feb 1 | 1-1 |
Valencia | Copa del Rey | Feb 8 | 2-0 |
Osasuna | La Liga | Feb 11 | 2-3 |
AC Milan | Champions League | April 3 | 0-0 |
Chelsea | Champions League | April 18 | 0-1 |
Real Madrid | La Liga | April 21 | 1-2 |
KIMENUKA YANGA: KIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI SEIF AHMED AJIUZULU
Kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya
yaliyopelekea timu ya Yanga kupoteza ubingwa wake, hatimaye leo kiongozi na
mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Yanga - Seif Ahmed ametangaza
kujiuzulu.
Seif ambaye amehusika na usajili wa wachezaji wengi wa Yanga msimu huu amesema ameona bora ajiuzulu ili kupisha kiongozi mwingine ambaye ataoangeza ufanisi na kuisadia Yanga iweze kurudisha makali yake na kuuchukua tena ubingwa wake wa ligi kuu msimu uajo.
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu.

ITS ALMOST DONE..... SIMBA YAKARIBIA BINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012
WEKUNDU wa Msimbazi,
Simba SC jioni hii wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya
kuifunga Moro United ya Morogoro maba 3-0 na mechi ya wapinzani wao katika mbio
za ubingwa, Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ikivunjika timu hizo zikiwa
zimefungana 1-1, Uwanja wa Azam, Chamazi.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' na Felix Mumba Sunzu Jr.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' na Felix Mumba Sunzu Jr.
Simba sasa imetimiza
pointi 59, ambazo kutokana na matokeo ya leo ya sare ya 1-1 kati ya azam na
Mtibwa, haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Lakini kujiweka salama, Simba
itahitaji japo polnti moja katika mechi zake tatu
zilizobaki.
Mchezo
kati ya Azam na Mtibwa ulivunjika wakati beki Salum Swedi amekwishaifungia bao
Mtibwa na Mrisho Khalfan Ngassa ameifungia Azam FC. Mtibwa waligomea mechi hiyo
wakipinga Azam kupewa penalti. Sasa Kamati ya Ligi Kuu itakutana kesho na kutoa
uamuzi, lakini kuna uwezekano mkubwa Mtibwa ikatozwa faini na wapinzani wao
kupewa ushindi.
Nafasi | Timu | MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Simba SC | 25 | 18 | 5 | 2 | 42 | 12 | 30 | 59 | |
2 | Azam | 23 | 15 | 5 | 3 | 34 | 11 | 23 | 50 | |
3 | Young Africans | 24 | 15 | 4 | 5 | 38 | 21 | 17 | 49 | |
4 | Mtibwa Sugar | 23 | 10 | 5 | 8 | 31 | 25 | 6 | 35 | |
5 | Coastal Union | 24 | 10 | 2 | 12 | 24 | 29 | -5 | 32 | |
6 | Kagera Sugar | 24 | 7 | 10 | 7 | 25 | 25 | 0 | 31 | |
7 | JKT Ruvu | 24 | 7 | 10 | 7 | 25 | 30 | -5 | 31 | |
8 | Ruvu Shooting | 24 | 7 | 9 | 8 | 20 | 19 | 1 | 30 | |
9 | JKT Oljoro | 23 | 7 | 8 | 8 | 16 | 20 | -4 | 29 | |
10 | Toto African | 24 | 5 | 11 | 8 | 23 | 27 | -4 | 26 | |
11 | African Lyon | 24 | 5 | 8 | 11 | 20 | 29 | -9 | 23 | |
12 | Villa Squad | 24 | 6 | 5 | 13 | 26 | 43 | -17 | 23 | |
13 | Moro United | 25 | 3 | 10 | 12 | 27 | 44 | -17 | 19 | |
14 | Polisi Dodoma | 25 | 3 | 8 | 14 | 18 | 34 | -16 | 17 |
MAGOLI 34 NA JINSI ALIVYOBADILISHA MSIMU WA ARSENAL: TATHIMINI YA MCHEZAJI BORA WA ENGLAND VAN PERSIE KUTOKA AUGUST 2011 - APRIL 2012
AUGUST |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
4(0) 1/1/2 2 6.25 |
Van Persie, na Arsenal in general, walianza msimu taratibu. Baada ya sare
tasa katika mechi ya ufunguzi., baadae mdachi huyo akafunga goli muhimu la
kusawazisha dhidi ya Udinese katika mechi ya play off ya champions league kabla
ya kufunga goli la pili katika mechi ya aibu kwa upande wao waliyofungwa 8-2
naManchester United.
SEPTEMBER SEPTEMBER |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
4(0) 1/1/2 2 6.25 |
Arsenal waliendelea kucheza ovyo mwezi wote wa septmber, ushindi mwembamba
dhidi ya Swansea na droo ngumu dhidi ya Dortmund zikifuatiwa na kufungwa na
Blackburn huku Van Persie akifanikiwa kufunga goli 1 katika mechi dhidi ya
wajerumani. Mambo yalianza kwenda vizuri baada ya kufunga goli mbili
zilizoisadia Arsenal kushinda 3-0 dhidi Bolton.
OCTOBER |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
5(0) 4/0/1 7 7.50 |
NOVEMBER |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
4(1) 3/2/0 5 7.50 |
DECEMBER |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
6(0) 4/1/1 4 7.08 |
JANUARY |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
4(0) 1/0/3 4 6.75 |
FEBRUARY |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
6(0) 3/1/2 4 6.75 |
MARCH |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
6(0) 5/0/1 4 6.75 |
APRIL |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
4(0) 2/1/1 1 6.7 |
JUMLA YA TATHIMINI YOTE YA MIEZI 10
SEASON'S TOTAL THUS FAR | |
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE) GAMES WON/DRAWN/LOST GOALS SCORED AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING |
43(2) 26/7/12 34 6.94 |
No comments:
Post a Comment