Tuesday, April 24, 2012

Tuesday, April 24, 2012


ROONEY MCHEZAJI BORA MAN UNITED


TUZO YA MCHEZAJI BORA MECHI NA EVERTON:
1 - Wayne Rooney (40%)
2 - Danny Welbeck (27%)
3 - Nani (19%)
WENGINE WALIOGEMBEA:
Antonio Valencia, Michael Carrick
Na Nick Coppack

Nyota ya Wayne Rooney yatakata

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney kwa kufunga mabao mawili Jumapili amejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi kutoka ManUtd.com.
Rooney, ambaye aliwafungia Mashetani Wekundu bao la kwanza na la tatu katika sare ya 4-4 dhidi ya Everton, alijishindi asilimia 40 ya kura zilizopigwa.
Wafungaji wengine wawili wa United - Danny Welbeck na Nani - pia walidhihirisha umaarufu kwenye kura hizo, lakini alikuwa Rooney aliyejishindia tuzo hiyo ya kwenye mtandano.
Rooney sasa amefikisha mabao 33 kwenye mashindano yote msimu huu, yakiwemo 12 aliyofunga katika mechi 11 zilizopita.
Licha ya kuonekana amerudi kwa kshindo, lakini hivi karibuni alisema hafurahishwi na kiwango chake na anaendelea kupambana kupandisha uwezo wake.

ZUBEDA WA SITIMBI ALETA MPYA


MWINGIZAJI wa filamu Swahiliwood, Immaculata Aloyce, anadai kuwa ili uone maisha magumu ng�ang�ania kuigiza filamu badala ya kufanya kazi nyingine.

�Nipo sehemu nafanya kazi nyingine kabisa tofauti na uigizaji ili niendeshe maisha yangu, lakini pia naweza kusema kuwa natafuta mtaji kwa ajili ya kutengeneza filamu yangu mwenyewe, nafikiria nikifanya hivyo angalau naweza kupata fedha kidogo, tofauti na filamu ya kushirikishwa,� anasema.

Immaculata alitamba na filamu kama Ikunda, Black Mail, Born to Suffer na alishiriki katika wimbo wa Prof. Jay wa 'Nikusaidiaje' akiigiza kama binti kutoka kijijini.

Mwanadada huyo anasema kuwa ana mpango wa kuwa mtayarishaji na kuigiza ili kujipatia kipato zaidi badala ya kuigiza filamu zinazoandaliwa na watayarishaji wengine.

WASANII WAGOMBEA KAMPUNI YA KANUMBA


Hisani Muya Tino
MWIGIZAJI Nyota wa filamu na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Hisani Muya Tino, amemshukia mchekeshaji na mwigizaji wa filamu Steven Mangere Steve Nyerere kwa kusema kuwa ni tatizo na mgombanishi wa wasanii wakubwa.

�Huyu Steve Nyerere ni mtu mbaya sana kwa sasa katika tasnia ya filamu, siku za nyuma wasanii walikuwa na ushirikiano wa kweli bila kuwa na makundi ambayo yapo sasa, na kila tatizo ukifuatilia utaambiwa Steve.

"Nimeshangaa sana hata msiba wa Kanumba haujakwisha tayari ameshatengeneza zengwe akidai kuwa mimi nimekaa na mama wa marehemu eti kumponda mdogo wake Seth asipewe kampuni ya Kanumba, hawezi kuongoza nipewe mimi,� anasema Tino.

Tino alisema kuwa Steve Nyerere alimpigia simu kwa kumlaumu kuwa Bongo Movie wapo Leaders wakiwa katika kikao cha kumjadili yeye kwa kuingilia suala la marehemu wakati wao walikuwa wanataka kuisimamia kampuni hiyo kwa kumtumia Seth, lakini Tino anakuwa kikwazo jambo ambalo linawakera, lakini pia alisema anashangaa Steve kujiweka mbele wakati marehemu alijitoa katika kundi hilo.

�Huyu anatakiwa kujua kuwa mimi sijajuana na marehemu juzi, nimekuwa nikifanya naye kazi mbalimbali hata kabla ya kufariki aliniita akaniambia anahitaji tuendeleze mradi wa kuinua vipaji vya wasanii wachanga na kusema nizifuate (tape) mikanda tuliyorekodi kwa ajili ya usaili wa wasanii tuliowafanyia siku za nyuma,� alisema Tino.

Mwanaspoti ilimpigia simu Steve Nyerere ambaye alisema kuwa mambo hayo yalishapita na Tino waliongea naye yakaisha, sasa anashangaa kuyasikia tena yakiendelea bila sababu za msingi wakati yeye anaamini kuwa hayana faida yoyote.

�Jamani hayo mambo yamepita, tumwache marehemu apumzike kwa amani hakuna sababu ya kuendelea na malumbano yasiyotuingizia fedha na tusitafute umaarufu kupitia marehemu, tufanye kazi maisha yaendelee, kama kuna kosa kila mtu kajifunza kwa wakati wake,� alisema Steve.

Kufuatia kifo cha Steven Kanumba kumekuwa na maneno yanayoashiria shari na kuibuka makundi kwa wasanii na kuzua vikao kila kukicha, huku wakishindwa kupanga mikakati imara ya maendeleo yao.



GAZETI LA MWANASPOTI LEO:

KOCHA WA YANGA AWAPA SIMBA SIRI ZA AL AHLY SHANDY



SREDOJEVIC MILUTIN MICHO
AL-AHLY Shandy ya Sudan itakayokutana na Simba kwenye raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho inashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya klabu barani Afrika.

Makao makuu ya timu hiyo yapo katika Mji wa Shandy, ambao upo kilometa 100 kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Si timu ya kubeza licha ya kutokuwa na ukubwa wa timu vigogo za Sudan za Al-Hilal na Al-Merreikh.

Hii inatokana na ukweli kuwa, imedhihirisha makali yake baada ya kuitoa Ferroviaro ya Msumbiji kwenye raundi ya kwanza ya mashindano haya.

Ferroviaro ina uzoefu mkubwa katika mashindano haya kwani imewahi kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itakabiliana Al-Ahly Shandy, Aprili 29 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limeteua waamuzi kutoka Swaziland, Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.

CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishina wa mechi hiyo.

Al Ahly imepata nguvu kutokana na jeuri ya fedha ya tajiri wa Sudan, Salah Idris, ambaye aliwahi kuongoza timu kigogo ya Al-Hilal kwa miaka nane.

Salah anatokea katika Mji wa Shandi na aliisaidia timu hiyo kupanda daraja mwaka jana, na iliposhiriki tu kwa mara ya kwanza ikakata tiketi ya kushiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Alipokuwa Al-Hilal aliisaidia kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka ya 2007 na 2009.

Tajiri huyo aliamua kuachana na Al-Hilal na kugombea uongozi wa Shirikisho la Soka la Sudan, ingawa alishindwa kwenye uchaguzi wake.

Salah amemwajiri kocha kutoka Tunisia, Kuki na nyota wa kigeni kutoka nchi za Nigeria, Mali na Saudi Arabia katika kikosi cha Al-Ahly Shandy.

Al Ahly ina raia wawili wa Nigeria, beki wa kati, Malik Isaac na Ike Francis, ambaye ni mfungaji hatari.
Kuna kiungo kutoka Mali, Bashiru na kipa Abdulraham Ali Daya, ambaye kwao ni Saudi Arabia.

Tajiri huyo wa Al Ahly pia aliwasajili wachezaji waliotemwa na Al-Hilal, ambao ni mabeki Osama Tawoon, Sadam Abdutalib, Samu Abdalla na wachezaji wa kiungo, Hamooda Bashir na mshambuliaji Nadir Al Taib, ambaye ndio alifunga mabao mawili wakati timu hiyo ilipoitoa Ferroviaro ya Msumbiji kwenye raundi ya kwanza.

Wachezaji hawa wa kigeni ukijumlisha na wachezaji wa zamani wa Al-Hilal, ambao wana uzoefu mkubwa na mashindano ya Afrika kunaifanya timu hiyo kuwa tishio kwa Simba.

Al-Ahly, ambayo inashika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu Sudan inajivunia vitu vikubwa vitatu.

Jamaa wanajiamini na hawaiogopi Simba kwani wanajivunia fedha nyingi na wanawalipa wachezaji wao vizuri, pia wana wachezaji wenye vipaji na kikosi chao kimesheheni wazoefu.
Pia wamepania kumdhibiti mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu kwani wanafahamu kutokana na kuwahi kuchezea Al-Hilal ya Sudan.

Kutokana na mazingira haya kunafanya Al-Ahly kuingia huku ikijiamini kwenye mechi hizi dhidi ya Simba.
Simba sasa watapaswa kujipanga kwa mbinu zote ndani na nje ya ili kuing'oa Al-Ahly kama ilivyofanya kwa Entente Setif ya Algeria.

Mwandishi wa makala hii ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, na amewahi kuifundisha Yanga.

No comments: