Wednesday, April 11, 2012


Reactions: 

Tumejifunza nini kutokana na mafanikio ya Simba dhidi ya Setif.

Katika hali ya kawaida kabisa Simba walipoteza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Es Setif , tena kwa matokeo mabaya sana ya kuruhusu mabao matatu ambayo hayawezi kumfurahisha kocha au mchezaji au hata shabiki yoyote yule ambaye anahusika na klabu yake .
Hata hivyo lazima tukiri ukweli kuwa katika michezo miwili Simba ilipata matokeo mazuri na ndio maana wamefanikiwa kufuzu kuingia raundi inayofuata ya michuano hii. Kwa sababu hii hatuna budi kutoa sifa pale sifa inapostahili na kiukweli kabisa Simba wanastaili pongezi kwa kuwatoa Setif.
Pamoja na sifa hizo lazima turudi nyuma na kujiuliza nini siri ya mafanikio ya Simba  na baada ya kujiuliza huko lazima tujifunze kutokana na mafanikio ya Simba hasa kwenye mchezo wao mwisho dhidi ya Setif.
Kikubwa kilichowasaidia Simba ni matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza ambao kwa Simba ulikuwa mchezo wa nyumbani. Kwenye mchezo wa kwanza Simba walishinda kwa mabao mawili bila na ndio maana pamoja na kupoteza mchezo wa marudiano , bao moja la ugenini lilitosha kuwapa matokeo ya kuwatoa Setif pamoja na ukweli kuwa matokeo ya jumla yalikuwa sare .
Moja ya vitu ambavyo vimekuwa vikizitatiza timu za Tanzania ni kutofanya vizuri hasa kwenye mchezo wa nyumbani. Ukirudi nyuma na kutazama mchezo wa Yanga dhidi ya Zamalek wiki chache zilizopita utagundua ukweli wa hoja hii . Hebu jiulize kama Yanga wangeshinda mchezo ule ambao uliisha kwa sare ya 1-1 labda kwa matokeo kama ya 2-0 au 3-0 au 3-1 ? Jibu ni moja tu kuwa hunda yanga wangekuwemo kwenye mashindano hii leo kwa kuwa Nyumbani Zamalek walishinda kwa bao moja  pekee. Hata timu ya taifa imekuwa na tatizo hilo hilo la kufanya vibaya nyumbani . Mfano angalia mara ya mwisho kwenye mchezo wa hatua za awali kufuzu kwa kombe la mataifaya afrika dhidi ya Msumbiji , sina lengo la kusema kuwa Taifa Stars itatolewa lakini siku zote unapotoka sare ya 1-1 au unaporuhusu bao la ugenini unajiweka kwenye mazingira magumu sana ya kusonga kwenye raundi inayofuata .
Kikubwa kilichowapa simba faida ni mchezo wa nyumbani ambao endapo time za kitanzania zitajifunza kuuchukuliakwa umakini matokeo kama ya Simba yataendelea kuwepo , hata kwenye mchezo unaofuata ambao Simba  watacheza na Al Aly Shandy wanapaswa kurudia kile walichokifanya kwenye mchezo dhidi ya Setif ambao siri ya ushindi ilikuwa mchezo wa nyumbani.
Zaidi ya hapo lazima usifu moyo wa kishujaa ulioonyeshwa na wachezaji wa Simba . Tunaweza kuzungumzia ushindi wa nyumbani tunavyotaka lakini bado bao moja la ugenini lililofungwa na Emmanuel Okwi limechangia asilimia hamsini ya ushindi wa Simba . Bao hili limekuja kutokana na juhudi binafsi za Okwi ambaye mara nyingi hufunga mabao ya aina ile , lakini zaidi ya hapo bao lile lilikuja kutokana na moyo wa kuendelea kupambana waliokuwa nao wachezaji wa simba . Mazingira yalikuwa magumu sana hasa ukizingatia hali ya hewa , na jins ambavyo mchezo ulikuwa unaelekea . Kwa mtu mwingine angeweza kukata tamaa na kuomba tu mechi iishe haraka apunguziwe mateso lakini Simba walipambana kiume na ndio maana wakapata matokeo kama yale. Hili ni fundisho muhimu kuwa mchezo ni dakika tisini na kabla ya filimbi ya mwisho kama mchezaji unapaswa kupambana kufa na kupona .

TAARIFA KUTOKA TFF!

Release No. 054
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 10, 2012

NGORONGORO HEROES YAINGIA KAMBINI
Kocha Kim Poulsen, leo (Aprili 10 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa umri huo.

Kikosi hicho kimeingia kambini leo (Aprili 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni Saleh Ally Malande (Simba), Aishi Salum Manula (Azam), Hassan Khamis Kessy (Mtibwa Sugar), Said Ruhava Samir (Falcon, Pemba), Carlos Protus Kilenge (TSC Mwanza), Dizzana Issa Yarouk (Azam), Amani Peter Kyata (African Lyon) na Issa Rashid Issa (Mtibwa Sugar).

Emily Mgeta Josiah (TSC Mwanza), Khamis Jamal Mroki (Mtibwa Sugar), Ramadhan Suzana Singano (Simba), Frank James Sekule (Simba), Frank Domayo Raymond (JKT Ruvu), Omega Sunday Seme (Yanga), Abdallah Kilala Hussein (Falcon, Pemba) na Ibrahim Rajab Juma (Villa Squad).

Hassan Saleh Dilunga (Ruvu Shooting), Alhaje Said Zege (JKT Ruvu), Jerome Lambele Reuben (Moro United), Atupele Green Jackson (Yanga), Simon Msuvan Happygod (Moro United) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo).

Mechi ya marudiano dhidi ya Sudan itachezwa jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.

Fainali za Afrika kwa vijana zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria. Timu nne za juu kwenye fainali hizo zitacheza Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu.

KAMATI YA NIDHAMU KUKAA J’MOSI
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana Jumamosi (Aprili 14 mwaka huu) kujadili rufani ya Yanga inayopinga kunyang’anywa pointi tatu.

Kamati ya Ligi ya TFF iliinyang’anya Yanga pointi tatu ilizopata kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union kwa kumchezesha beki Nadir Haroub anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

AZIM DEWJI KUWAUNGAISHA TENA SIMBA NA MBWANA SAMATA PAMOJA NA PATRICK OCHAN

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta na Patrick Ochan watakutana tena na wachezaji wenzao wa zamani, viongozi wao- kwa ujumla na timu ya zamani, Simba SC.
Katika kuhakikisha Simba inazidi kuimarika kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mfanyabiashara maarufu na mwanamichezo Azim Dewji anakusudia kuileta nchini timu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa ajili ya kuipa makali Simba kabla ya wawakilishi hao wa Tanzania hawajaivaa Al Ahly Shandy ya Sudan.
Dewji aliyeifadhili Simba kwa miaka mingi, alisema jana Dar es Salaam kuwa ziara inaratibiwa na kampuni yake ya Simba Trailers na kwamba ameshazungumza na kuafikiana na Rais wa Mazembe, bilionea Moise Katumbi Chapwe na pia uongozi wa Simba.
 “Pamoja na kuwazawadia pesa wachezaji wa Simba, nimeona nitoe mchango zaidi kwa kuwaletea mechi ya kujipima nguvu na timu bora ya Mazembe ya
Kongo,” alisema Dewji aliyetoa sh milioni 15 kwa Simba baada ya kuitoa ES Setif ya Algeria.
Kwa mujibu wa Dewji, mchezo baina ya Mazembe na Simba unatarajiwa kufanyika Aprili 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni wiki moja kabla ya `Wekundu wa Msimbazi’ kuumana na Al Ahly.
Alisisitiza kuwa, Mazembe itakuwa kipimo sahihi kwa Simba kutokana na kuwa na kikosi chenye hadhi ya juu.

WABUNGE HALIMA MDEE WA CHADEMA NA ESTER BULAYA WA CCM - WAANZISHA KAMPENI YA KUMSAIDIA LULU NA FAMILIA YAKE.

Mbunge wa kawe/Chadema Halima mdee yeye pamoja Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya (CCM) jana walienda kumuona Lulu, na kwa wakati huu Mh Halima Mdee kupitia mtandao wa Tweeter anaendesha kampeni ya Kuchangisha Pesa za malazi kwa ajili ya familia ya Lulu (mama yake).
Mh.Halima mdee amesema kwamba lulu anahitaji mwanasheria makini wa kuweza kumnasua kwenye kesi hiyo, lakini pia anahitaji mwana saikolojia (psychological support) wa kuzungumza nae ili aweze kuwa fresh kiakili.


kwa wakati huu Lulu anashikiliwa katika kituo cha polisi Oysterbay


SOMA TWEETS ZA @HALIMA MDEE

Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Watz wenzangu. Leo mimi na mhe. Bulaya tulikwenda kumuona Lulu oysterbay polisi. She really needs our support. Kwanza she is only 17..


Halima J Mdee ‏ @halimamdee



Pili anahitaji sana psychological support. Nawaomba watu wenye taaluma hiyo wasisite kwenda kumuona. wasiliana na 0714282527steve nyerere.


Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Tatu anahitaji wanasheria makini wa kumsaidia. Kwa yeyote ambaye yuko tayari naomba awasiliane nami 0759569823..


Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Nne,at that tender age ndio alikuwa anategemewa na familia yake. Now yuko ndani matatizo yamezidi kuwa makubwa.


Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Kwa yeyote anayeguswa,naomba atume chochote kwenye namba hii 0754878890 ni namba ya m pesa ya mama yake Tumsaidie huyu mtoto!


Again ..Namba ya M -PESA kwa wanaotaka msaidia Binti yetu Lulu+255754878890.Ni namba ya mama yake!

No comments: