Sunday, October 2, 2016

Zaidi ya wakazi 5,000 Rufiji wanufaika na Mradi wa elimu ya uzazi



Mmoja wa Watoa elimu jumuishi(WAJA) Jumanne Mbondele,akielezea jambo kuhusiana na mwitikio na kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo,wakati  Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo pamoja na Taasisi ya  Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya  kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani.




Baadhi ya wakina mama wakisuburi huduma za afya katika  kituo cha Afya Mohoro,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani kituo hicho kinafadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi wa Afya ya baba mama na mtoto na kuendeshwa na Taasisi ya  Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya  kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani.


NA MWANDISHI WETU, RUFIJI
 Zaidi ya wakazi 5,000/=wa vijiji sita vya vya kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani wamenufaika na mradi wa elimu kuhusu  afya ya uzazi na mtoto iliyotolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana naTaasisi ya  uzazi na malezi bora (UMATI).
Takwimu hizo zilitolewa jana na  Razia Mamboleo Ofisa wa Programu wa mradi huo Wilayani hapa ambao umehusisha  vijiji vya Shela,Mohoro Mashariki,Mohoro Magharibi,Ndundutawa,King'ong'o  pamoja na Kwaijia.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za mradi huo Radhia alisema mradi huo umeleta mafanikio makubwa  ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto,akina mama kupata mwamko wa kuhudhuria Kliniki kwa wakati mwafaka kipindi cha ujauzito sambamba na kuboreshwa kwa huduma za uzazi  katika vijiji hivyo.

Aidha Radhia alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia mradi huo umefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi  sambamba na kuwapatia wanawake chanjo kwa wakati tofauti na awali .

 Baadhi ya watoa elimu jumuishi ya  afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo, (WAJA) wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo pamoja na Taasisi ya  Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya  kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani.

Alijinasibu kuwa mradi huo umefanikiwa kutoa elimu kwa watoa huduma jumuishi (WAJA) ambao walipatiwa mafunzo kwaajili ya kuelimisha jamii jambo ambalo limeongeza uelewa wa masuala ya afya ya mama na mtoto katika jamii ya watu wa Rufiji.
Akizungumzia kuhusu changamoto za mradi huo ambao unafikia tamati Oktoba mwaka huu, Razia  alieleza kuwa  kikwazo kukibwa ni  ya kieneo na kijiografia ambayo ufikaji wake ni wa kusua sua.

"Changamoto kubwa ni ya kieneo, maeneo mengine hayafikiki kutokana na miundo mbinu mibovu ambayo imesababisha magari kutofika"alisisitiza Razia.

Kwa upande wake mmoja wa Watoa elimu jumuishi (WAJA) Jumanne Mbondele alisema mradi huo umepata mwitikio chanya  kwa wakazi wa Kata hiyo lakini changamoto kubwa ni ya kijiografia.

"Mwitikio ni mzuri sana na imesaidia sana Kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo lakini mradi ni wa muda mfupi na ndiyo kama hivyo uanelekea ukingoni,tuanaomba mradi uongezewe muda angalau uwe wa miaka mitatau ili uweze kufikia maeneo mengine"alihitimisha Mbondele.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mohoro,Tegemei Mtambo(kushoto)akielezea jinsi watoa elimu jumuishi(WAJA) pichani  walivyochangia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa elimu ya afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo,wakati  Uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation ambao ni wadhamini wa mradi huo na kuendeshwa na  Taasisi ya  Uzazi na Malezi bora (UMATI) walipowatembelea kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi huo uliowanufaisha zaidi ya wakazi elfu 5/- wa vijiji sita vya  kata ya Mohoro ,Wilayani  Rufiji mkoani Pwani.

Naye Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kuwa  mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa  hasa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, afya ya mama na mtoto sambamba na matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanaume na wanawake.
"Vodacom Tanzania Foundation itaendelea kusaidia jamii hasa katika masuala mazima ya afya  ili kutimiza malengo ya milenia kuhakikisha sera ya afya ya kupunguza vifo vya mama na mtoto sambamba na uboreshwaji wa afya ya uzazi "alihitimisha Rwehikiza.

No comments: