ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI TUZO ZA TASWA
RAIS
mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
hafla ya ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011 zinazotolewa na Chama
cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) zitakazofanyika kesho kwenye
ukumbi wa Diamond Jubillee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taswa Juma Pinto alisema jana
kwamba, chama chake kimeualika Mwinyi kutokana na mchango wake mkubwa katika
maendeleo ya michezo hapa nchini.
Alisema
maandalizi kwa ajili ya hafla hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya bia ya
Serengeti Breweries, yanaendelea vema ambapo kituo cha televisheni cha ITV
kitarusha Live tukio hilo.
Mshindi
wa jumla atazawadiwa kitita cha shilingi milioni 12.5 ambapo wanaowania katika
mpira wa kikapu kwa upande wa wanawake ni pamoja na Doritha Mbunda, Evodia
Kazinja (JKT Queens), Faraja Malaki (Jeshi Stars), huku kwa upande wa wanaume ni
Alpha Kisusi, (Vijana), Filbert Mwaipungu, Gilbert Batungi (ABC), wakati Liliam
Sylidion na Doritha Mbunda
watachuana katika Netiboli.
Kwa
upande wa gofu wanaowania ni Madina Iddi ,Hawa Wanyeche ,Ayne
Magombe kwa upande wa wanawake,wakati kwa wanaume ni Frank Roman,Nuru Mollel na
Issac Anania kwa upande wa Wabaume, huku gofu ya kulipwa ni Fadhili Saidi Nkya,
Yasini Salehe na Hassani Kadio.
Ahmada
Bakar,Amina Daud Simba (kisahani na tufe),Othman Ally Othman (mkuki, kisahani na
tufe) wanawania kwa upande wa Olimpki maalum, huku katika Paralimki ni Zaharani
Mwenemti, Joseph Nziku, Yohana Mwila kwa upande wa Wanawake, wakati Faudhia
Chafumbwe, Siwema Kilyenyi na Janeth Madise watachuana kwa upande wa
wanawake.
Katika
ngumi za ridhaa mchuano utakuwa kati ya Suleiman Kidunda,Victor Njaiti na
Abdalah Kassim,huku kwa upande wa waogeleaji (Wanawake) ni Magdalena Moshi,
Gouri Kotecha, na Mariam Foum na kwa wanaume ni Amaar Ghadiyali na Omary Abdallah.Judo
itawaniowa na Mbarouk Seleman Mbarouk, Mohammed Khamis Jumana Azzan Hussein
Khamis.
Wavu
(Wanawake) itawaniwa na Zuhura Hassan, Theresia Ojode (JESHI STARS
DAR)na Everlyne Albert wa magereza, huku kwa upande wa Wanaume ni Mbwana Ally, (
MZINGA CORPORATION – MOROGORO),Kevin Peter (MAGEREZA – DAR),Farhan Abubakar (
MAFUNZO ZNZ) na katika ngumi za kulipwa ni Benson Mwakyembe,Nasibu
Ramadhan,Francis Cheka,Nassib Ramadhan na Fadhil Majia.
Watakaowani
Tenisi kwa upande wa Wanaume ni Waziri Salum, Omary Abdallah,Hassan Kassim,
wakati Wanawake ni Rehema Athuman, Mkunde Iddy na Violet Peter.Baiskeli ni
Sophia Hussein,Sophia Anderson kwa upande wa Wanawake, huku Richard Laizer
naHamisi
Hussein watachuna kwa upande wa wanaume.
Tuzo
ya wachezaji wanaocheza nje itawaniwa na Henry Joseph,Mbwana
Samatta-Soka, Sophia
Mwasikili (Soka), huku ile ya mchezaji bora chipukizi itwaniwa na Theresia
Ojode- wavu (Jeshi Stars),Shomari Kapombe (soka) SIMBA na Salum Abubakari-Azam
(soka), wakati mchezaji wan je anayecheza Tanzania ni Haruna
Niyonzima-Yanga,Kipre Tchetche-Azam,Emmanuel Okwi-Simba (soka).
Aidha,
tuzo ya mwanasoka kwa wanawake itawaniwa na Asha Rashid,Mwanahamisi Omary
(Mburahati Queens),Fatuma Mustapha (Sayari),Eto Mlenzi (JKT), wakati kwa upande
wa wanaume ni John Bocco,Aggrey Morris-Azam na Juma Kaseja-Simba, huku katika
Riadha Wanawake ni pamoja na Zakia Mrisho,Mary Naali na Jaqueline Sakila wakati
kwa upande wa Wanaume ni Dickson Marwa na Alphonce Felix.
Mikono
Wanawake ni Abinery Kusencha (JKT Ruvu),Kazad Mtong (Magereza Kiwira) na Faraji
Shaibu Khamis (Nyuki Zbar), huku kwa upande wa Wanaume ni Doris
Mangara-(Magereza Kiwira),Zakia Seif (Ngome Dar),Mary Kimiti (Magereza Kiwira)
na .Kriketi
Wanawake itawaniwa na MoniCa Pascal,Asha Daudi na Esther Wallace, huku Wanaume
ni Kassimu Nassoro,Benson Mwita na Riziki Kiseto.
TAIFA STARS YAJIPANGA KUIKABILI MSUMBIJI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen amesema ili kuitoa Msumbiji ‘Mambas’ kwenye michuano ya Afrika ni lazima
timu yake ishinde mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 17 mwaka huu jijini
Maputo.
Mechi ya marudiano kusaka tiketi
ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani
nchini Afrika Kusini itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo
ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9 mchana kwa saa za huko.
Kim amewaambia Waandishi wa
Habari leo (Juni 13 mwaka huu) kuwa maandalizi ya kikosi chake yanakwenda vizuri
ingawa ana wachezaji watatu ambao ni majeruhi; kipa Mwadini Ali, na mabeki
Nassoro Masoud Cholo na Waziri Salum.
Amesema wachezaji hao
hawatakuwemo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoondoka Juni 15 mwaka huu saa 11
alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.
Kocha huyo amesema baada ya
mechi tatu maendeleo kiuchezaji kwa timu yake inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager ni mazuri ingawa bado anafanyia kazi kwa nguvu safu ya
ushambuliaji. Mechi iliyopita Taifa Stars iliifunga Gambia 2-1 huku mabao yote
yakifungwa na mabeki.
Iwapo Taifa Stars itaitoa
Msumbiji katika raundi ya mwisho itapangiwa moja kati ya timu 16 zilizocheza
Fainali za AFCON zilizofanyika Januari mwaka huu katika nchi za Gabon na
Equatorial Guinea. Katika mechi ya kwanza dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Dar es
Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Taifa
Stars ambayo msafara wake utakuwa na wachezaji 20 itaagwa kesho (Juni 14 mwaka
huu) saa 6 mchana kambini kwao- hoteli ya Accommondia (Tansoma) jijini Dar es
Salaam. Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa
miguu.
WAAMUZI KOZI YA FIFA KUPIMWA UFAHAMU WA ALAMA
Waamuzi 54 wanaoshiriki kozi ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyoanza Juni 11 mwaka huu,
kesho (Juni 14 mwaka huu) watahamia Uwanja wa Karume kwa ajili ya mazoezi ya
alama (signals). Mazoezi hayo yatafanyika kuanzia saa 1-4 asubuhi.
Kozi hiyo itakayomalizika kesho
(Juni 14 mwaka huu) inaendeshwa na wakufunzi Carlos Henriques na Mark Mizengo
kutoka FIFA wakisaidiwa na wakufunzi wengine wanne wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Wakufunzi wa TFF ni Kapteni
mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Waamuzi wanaoshiriki ni 14 wa
Tanzania wenye beji za FIFA ambao ni Erasmo Jesse, Ferdinand Chacha, Hamis
Changwalu, Hamis Maswa, Israel Mujuni, John Kanyenye, Josephat Bulali, Judith
Gamba, Mwanahija Makame, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Saada Tibabimale, Samuel
Mpenzu na Sheha Waziri.
Washiriki
wengine ni 20 wa daraja la kwanza (class one), kati ya hao watano wanatoka
Zanzibar. Lakini vilevile wapo waamuzi chipukizi (watoto) 20 ambao mwaka jana
walitumika katika michuano ya Kombe la Uhai na Copa
Coca-Cola.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J'MOSI
Na Mwandishi
Wetu
WAREMBO
wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 jumamosi hii
wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika
katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi
wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Mratibu wa
shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara
hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati
zao za kielimu.
Alisema
Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na
kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne
zilizopita.
“Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu
la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya
kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza
kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo
washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE),
uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya
The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao
ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na
Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda,
Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo,
Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo
limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s
Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada
Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa
Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na
Full Shangwe.
KUONA TWIGA STARS, ETHIOPIA 2,000/-
Kiingilio
cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya
Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia itakayochezwa Jumamosi (Juni 17 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 2,000.
Kiwango
hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani na rangi ya chungwa. Viti hivyo
kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 48,590 kwenye uwanja huo wenye uwezo
wa kuchukua washabiki 60,000.
Viingilio
vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000 kwa VIP B na
C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi
kuanzia saa 3 asubuhi.
Mechi
hiyo itachezeshwa na waamuzi Grace Msiska atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi
wake ni Bernadettar Kwimbira, Happiness Mbandambanda na Linda Chikuni, wote
kutoka Malawi. Kamishna ambaye anatoka Kenya ni Maqulate Atieno. Waamuzi hao
wanawasili leo.
JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA SIKU YA SABA SABA
Mabondia,
Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa
utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa
saba katika uwanja mpya wa taifa .Picha na Maktaba ya www.superdboxingcosach.blogspot.com)
Ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
Ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment