WACHEZAJI TAIFA STARS WAPEWA 'NENO' NA MKUU WA MKOA DAR
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Meckysadik amewataka wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars kuhakikisha wanadumisha viwango vyao kama wachezaji wa nchi nyingine,
badala ya desturi iliyozoeleka ya wachezaji wa nchi hii ‘kufulia’ mapema
kisoka.
‘Bosi’ huyo wa Jiji la Dar es
Salaam, ameyasema hayo mchana wa leo kwenye hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani,
Kariakoo katika hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa Taifa Stars na kuwakabidhi
bendera kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini, dhidi ya Msumbiji Jumapili mjini
Maputo.
“Nawaomba mjitahidi kudumisha
viwano vyenu kama ilivyo wachezaji wa wenzetu, wanacheza mpira kuanzia wana
miaka 18 na wanaendelea hadi wakifika miaka 30, sasa naomba na nyinyi iwe hivyo,
siyo kama ilivyo sasa, mchezaji wa Tanzania anaibuka, baada ya mwaka mmoja au
miwili anapotea,”alisema.
Pamoja na hayo, kuelekea
mchezo huo na Msumbiji Jumapili, ambao Stars inatakiwa itoke sare ya 2-2 au
zaidi ili kusonga mbele, baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 na Mambas mjini
Dar es Salaam, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Stars wakapiganie
ushindi.
“Mimi huwa sipendi haya mambo
ya kupigiana mahesabu, siyo mazuri. Kama sasa hivi kwenye Euro 2012 kuna timu
zinapigiana mahesabu, kwa sababu zimelingana kila kitu. Mimi ninataka mkashinde,
kapiganieni ushindi,”alisema Meckysadik.
Mapema, Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga aliwaambia wachezaji wa Taifa Stars
kwamba, mwanafunzi mzuri ni yule anayeendelea kujifunza kila siku kwa juhudi na
si yule anayejiona tayari amejua na kubweteka.
Kwa
sababu hiyo, Tenga akawataka Stars wakacheze kwa juhudi zaidi Msumbiji na si
kujiona wamefuzu baada ya kuifunga Gambia, mabao 2-1 Jumapili katika mchezo wa
Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka
2014.
Kwa
upande wake, kocha wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulesen amesema kwamba
wanaelekea kwenye mchezo mgumu, lakini watapigana kwa juhudi kupata ushindi, ili
kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi katika kuwania tiketi ya Afrika
Kusini 2013.
Poulsen ambaye huo, utakuwa
mchezo wake wa nne tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan
Poulsen baada ya awali kuiongoza timu hiyo katika sare ya 0-0 na Malawi Dar es
Salaam, kichapo cha 2-0 kwa Ivory Coast mjini Abidjan na ushindi wa 2-1 na
Gambia, amesema vijana wake wanaendelea kuimarika kila kukicha na ana matumaini
nao makubwa.
Anasikitika tu jana kiungo
Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ aliumia mazoezini, ingawa amesema anaendelea na
matibabu na wataenda naye Msumbiji.
Kwa
upande wake, Nahodha Juma Kaseja alisema kwamba wanatambua ugumu wa mchezo huo
kwao, lakini watakwenda kupigana ‘kufa na kupona’. Kaseja amesema kwamba soka
siyo tufe kwamba kila siku liko vile vile, bali inabadilika na sasa timu yao
imebadilika mno na Watanzania watarajie matokeo mazuri Jumapili.
STARS YAKABIDHIWA BENDERA TAYARI KUUA MAMBA
Beki Kelvin Yondan |
Kiungo mkabaji Frank Damayo |
Mabakidhiano ya bendera |
Katibu wa TFF, Angetile Osiah akkzungumza |
Rais wa TFF, Leodegar Tenga akizungumza |
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen akijadiliana na Msaidizi wake, Sylvester Marsh |
Kiungo Haruna Moshi 'Boban' akisikiliza kwa makini |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meckysaidk akizungumza kwa hisia |
Kocha wa makipa wa Taifa Stars, Juma Pondamali kushoto akiwa Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi |
MASTAA AZAM FC WAKITANUA VIFUA KATIKA GYM LA KISASA CHAMAZI
Asubuhi ya leo, BIN
ZUBEIRY ilitembelea kambi ya Azam FC, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar
es Salaam na kuwakuta wachezaji wa timu hiyo, itakayoiwakilisha Tanzania kwenye
Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani wakijifua kwa mazoezi ya kujenga
miili chini ya makocha wao, Waingereza, Stewart Hall na Msaidizi wake,
Kalimangonga Sam Daniel Ongala kwenye gym kali na ya kisasa ya klabu hiyo,
iliyopo ndani ya Uwanja wao, Chamazi. Cheki picha hizo.
|
Kocha Stewart akiinua nondo |
Add caption |
Luckson Kakolaki |
Kipre Tchetche |
Said Mourad |
Gaudence Mwaikimba |
Zahor Pazi |
Odhiambo Blackberry |
Kipre Balou |
Kutoka kushoto, Ibrahim Shikanda, Himid Mao na Ibrahim Mwaipopo |
Kutoka kulia Jabir Aziz, Ramadhan Chombo na ... |
Kali Ongala akimuelekeza Ibrahim Mwaipopo, kushoto ni Mao |
Wednesday, June 13, 2012
JUVENTUS WAANZA MAZUNGUMZO NA VAN PERSIE, MSHENGA NEDVED
Tetesi za Alhamisi magazeti
Ulaya
JUVE WAANZA MZUNGUMZO NA VAN PERSIE, MSHENGA NEDVED
KLABU ya Juventus imempeleka
Mkurugenzi wake na mchezaji wake wa zamani, Pavel Nedved akakutane mshambuliaji
wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, kujadili suala la kuhamia
kwake Turin.
KLABU
za Manchester City na Chelsea zinakabaliwa na upinzani wa mabingwa wa Serie A,
Juventus katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani, mwenye
umri wa miaka 25.
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou, mwenye umri wa miaka 26, atakuwa wazi
kwenda Liverpool kuungana na kocha wa zamani wa The Blues, Brendan Rodgers, kwa
mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.
KLABU
ya Liverpool imeambiwa kwamba mshambuliaji mwingine wanayemtaka wa Barcelona,
Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 20, atawagharimu pauni Milioni 7.
KLABU
ya Chelsea inamtaka mshambuliaji wa Malaga, Salomon Rondon, mwenye umri wa miaka
22, ili arithi mikoba ya Didier Drogba.
KLABU
ya West Ham inajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Blackburn, Yakubu, mwenye umri
wa miaka 29, ambao anaweza kuwagharimu The Hammers pauni Milioni 1.
MOYES KUMRITHI HARRY SPURS
KLABU
Ya Tottenham ina mpango wa kumchukua kolcha wa Everton, David Moyes ili mbadala
wa Harry Redknapp, aliyetupiwa virago.
KOCHA
wa zamani wa Charlton, Alan Curbishley na kocha wa zamani wa Hull na Preston,
Phil Brown wote wamo kwenye orodha ya walimu wanaotarajiwa kurithi mikoba ya
Chris Hughton katika klabu ya Birmingham City.
MKURUGENZI
wa akademi ya Crewe, Dario Gradi anaamini mchezaji mpya wa Manchester United,
Nick Powell, mwenye umri wa miaka 18, ana dalili za kutosha za kuwa kama Eric
Cantona au Wayne Rooney kwa mafanikio kwa Mashetani hao Wekundu.
No comments:
Post a Comment