KIUNGO mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima 'Fabregas' ameushawishi uongozi wa timu hiyo kumsainisha straika Meddy Kagere anayemaliza mkataba na timu ya Polisi ya Rwanda. Gazeti la Mwanaspoti limeandika jana kwamba Fabregas, ambaye alitamba na Yanga msimu uliopita amezungumza na viongozi wanaowezesha usajili wa Jangwani na kuwaambia kuwa Kagere ni bonge la straika na anaweza kufanya kazi kubwa msimu ujao. Kiungo huyo alizungumza na Mwanaspoti kutoka Lagos, Nigeria ambako timu yake ya Rwanda itacheza na Super Eagle leo Jumamosi na kusema; "Kagere ni straika mzuri sana nimekaa naye timu ya taifa namuona anavyocheza ni aina ya mchezaji ambaye Yanga inastahili kuwa naye." "Viongozi wa Yanga wamezungumza naye na mambo yanakwenda vizuri, nadhani tukirudi Rwanda wanaweza kumalizana naye. Ni mchezaji mwenye juhudi sana anayeweza kupunguza tatizo la mabao hapo Yanga, ana juhudi sana halafu si mtu wa kukubali kushindwa kirahisi. "Akifanya kazi kwa uwezo wake wote ninaoujua mimi, tutafika mbali na atang'ara sana na Yanga hata kwenye ligi ya Tanzania atakubalika upesi sana, ngoja akifanikiwa kuja utakubali maneno yangu," alisema Fabregas. Mmoja wa viongozi wa jopo la usajili alikiri kuwa Fabregas amewahakikishia wakimsajili mchezaji huyo wameula na atafanya kazi. Aliongeza kuwa bado wanaendelea na mazungumzo ya kupata beki wa kati kutoka kwenye timu ya taifa ya Kenya au Uganda na mkakati mwingine ni kuhakikisha wanamalizana na Kagere ambaye aliwahi kuitolea nje Gor Mahia ya Kenya. Ingawa tayari wametua Dar es Salaam, lakini Yanga imepanga kuachana na mastraika wake Davies Mwape wa Zambia na Kenneth Asamoah wa Ghana ili kusajili wapya wawili kutoka nje; Kagere akiwa miongoni. Simon Msuva wa Moro United ndiye straika pekee mzalendo ambaye Yanga imeshamsajili hadi sasa safari hii. |
MHARIRI GAZETI LA BINGWA AFARIKI DUNIA
MHARIRI wa Jamboleo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo (saa 6.30) usiku.
Taarifa ya Neville
Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, imesema kwamba Willy aliyewahi
kuwa Mhariri wa gazeti la BINGWA, pamoja na wahariri wengine walikuwa mjini
Morogoro ambako walikwenda kuhudhuria mkutano wa masuala ya sensa iliyoandaliwa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Mara baada ya semina
hiyo alikwenda kuwaona watoto wake na alikuwa huko hadi saa sita usiku
alipomwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo la kurejea katika hoteli
alikokuwa amefikia. Baada ya kutoka nje, na hatua sita hivi kabla ya kufika
pikipiki ilipokuwa, alianguka.
Ndugu zake walimkimbiza
hosipitali lakini walipofika na daktari kumpima, tayari alikuwa “amenyamaza”
yaani amefariki dunia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es
Salaam zinafanywa.
Tutamkumbuka daima kwa
upole na unyeyekevu wake. Kweli Willy ametuacha, ni pigo kwa taaluma yetu, ni
pogo katika Jukwaa la Wahariri. Poleni kwa familia ya Willy Edward Ogunde, pole
kwa wahariri wote na pole kwa tasnia nzima ya habari. Bwana alitoa na Bwana
ametwaa, jina lake lihimidiwe.
PREVIEW STARS V MAMBAS; VIJANA LAZIMA WASHINDE LEO
Kikosi cha Stars kilichoiua Gambia Jumapili Taifa. |
Na Prince
Akbar
TIMU ya soka ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars leo ina kibarua kigumu mjini Maputo, Msumbiji wakati
itakapokuwa ikimenyana na wenyeji, Mambas katika mchezo wa kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika
Kusini.
Taifa Stars, ambayo kwenye
mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 mjini Dar es Salaam, inatakiwa lazima
kushinda au japo ikikwama kabisa itoe sare ya mabao yasiyopungua 2-2 au
zaidi.
Taifa Stars inaonekana
kuimarika kwa sasa na si sawa na ile iliyomenyana na Mambas Febrauri 29, mwaka
huu na kutoka sare ya 1-1.
Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY
asubuhi ya leo kutoka Maputo kwamba, tayari Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulen ametaja kikosi chake kitakachoanza mechi ya leo na katika safu ya
ushambuliaji amewapanga pamoja washambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel
Ulimwengu.
Katika mechi hiyo
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo
kuanzia saa 9:00 kamili kwa saa za huko sawa na saa 10:00 kwa saa za kwetu,
Poulsen amemuacha benchi beki Amir Maftah na atamuanzisha Erasto Nyoni katika
beki ya kushoto.
Safu ya ulinzi ya Stars
itaongozwa na mlinda mlango na Nahodha wa timu hiyo,
Juma Kaseja, wakati Shomari
Kapombe atacheza beki ya kulia, kushoto Erasto Nyoni, waakti katikati watasimama
Mwanasoka Bora wa Tanzania, Aggrey Morris na Kelvin Yondani.
Ameweka viungo wakabaji
wawili, Shaabani Nditi atakayecheza chini na Frank Damayo atakayecheza juu
wakati huo huo Mwinyi Kazimoto atacheza kushoto na Mrisho Ngassa kulia, wakati
washambuliaji ni Ulimwengu na Samatta.
Maana yake leo, kutokana
umuhimu wa Stars kutoruhusu bao leo huku ikisaka mabao, Poulsen amemuweka Damayo
na Nditi ili wakabe sana, wakati Mwinyi na Ngassa watakuwa na kazi ya
upishi.
Ulimwengu ana sifa ya kuwa
nguvu na uwezo wa kukokota mpira, wakati Samatta anakimbiza na uwezo wa kuwatoka
mabeki kwa chenga, kuwakokota na pia ni mjanja mno.
Dhahiri Stars itatawala mchezo
leo, kwa sababu Ngassa ana uwezo mkubwa wa kushambulia- hivyo ni sawa na kucheza
na washambuliaji watatu wakati Mwinyi atakuwa akiwachezesha washambuliaji
hao.
Damayo na Nditi, wote pamoja
na kuwa wakabaji, lakini pia ni watoaji wazuri wa pasi ndefu na
fupi.
Kama ilivyokuwa kwenye mechi
na Gambia Jumapili iliyopita, kuna uwezekano kiungo ‘fundi’ Haruna Moshi ‘Boban’
akatokea benchi kipindi cha pili kwenda kuimarisha safu ya ushambuliaji na
dhahiri atachukua nafasi ya Ulimwengu.
Stars ikishinda mechi ya leo,
itapangwa kwenye Kundi kucheza mtindo wa ligi kuwania tiketi ya kucheza fainali
za AFCOn mwakani, ambazo zinakuja mapema ili kukwepa kugongana na Fainali za
Kombe la Dunia mwaka 2014.
Kila la heri Taifa Stars.
Mungu ibariki Tanzania.
POULSEN ATAJA 11 WANAOANZA LEO, ULIMWENGU NA SAMATTA KUONGOZA MASHAMBULIZI
Kim Poulsen |
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulen ametaja kikosi chake kitakachoanza mechi ya leo dhidi ya Msumbiji (The
Mambas) itakayochezwa Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto hapa Maputo. Mechi itaanza
saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo nyumbani
Tanzania itakuwa saa 10
kamili.
Stars inaundwa na;1.
Juma Kaseja, 20. Shomari Kapombe, 22. Erasto Nyoni, 6. Aggrey Morris, 5. Kevin
Yondani, 19. Shaabani Nditi, 8. Mrisho Ngasa, 16. Frank Domayo, 11. Thomas
Ulimwengu, 10. Mbwana Samata na 15. Mwinyi Kazimoto.
Wachezaji wa akiba;18.
Deogratias Munishi, 17. Amir Maftah, 13. Jonas Mkude, 3. Haruna Moshi, 12. Simon
Msuva, 9. Christopher Edward, 14. John Bocco, 7. Ramadhan Singano na 21. Nurdin
Bakari.
Benchi la
Ufundi;
Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk. Juma Mwankemwa (Daktari wa Timu), Dk. Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk. Juma Mwankemwa (Daktari wa Timu), Dk. Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Refa: Bennett Daniel (Afrika
Kusini)
Refa Msaidizi 1; Molefe Enock (Afrika Kusini)
Refa Msaidizi 2; Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini)
Refa wa Akiba; Hlungwani Tinyiko Victor (Afrika Kusini)
Kamishna wa Mechi; Mateus Joel Amdhila (Namibia)
Refa Msaidizi 1; Molefe Enock (Afrika Kusini)
Refa Msaidizi 2; Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini)
Refa wa Akiba; Hlungwani Tinyiko Victor (Afrika Kusini)
Kamishna wa Mechi; Mateus Joel Amdhila (Namibia)
ARSENAL WAKUBALI KUMUUZA VAN PERSIE BEI POA TU, WALCOTT NAYE HUYOOOOO
Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya
ARSENAL WAKUBALI KUMUUZA VAN PERSIE PAUNI MILIONI 30
HATIMAYE klabu ya Arsenal
imekubali kumuuza mshambuliaji wake Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28,
kwa dau la pauni Milioni 30 - na winga wa Washika Bunduki hao, Theo Walcott,
mwenye umri wa miaka 23, anaweza pia kumfuata Mholanzi huyo katika mlango wa
kutokea.
KOCHA
wa Arsenal, Arsene Wenger amepanga kusajili wachezaji wawili wa Ufaransa,
Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, na Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka
21.
KOCHA
Mreno, Jose Mourninho atajaribu kuinasa saini ya kiungo mchezeshaji wa kimataifa
wa Hispania, David Silva, mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa anachezea
klabu bingwa England, Manchester City ili ahamishie cheche zake Real
Madrid.
KLABU
ya Manchester United inamuwania kiungo wa klabu ya Hoffenheim, Gylfi Sigurdsson,
mwenye umri wa miaka 22, huku kocha Sir Alex Ferguson akitunisha misuli ili
kuipiku Liverpool inayomuwania pia.
KLABU
ya Manchester United inataka kutumia fursa ya kufukuzwa kazi kwa Harry Redknapp
katika klabu ya Tottenham kwa kusajili wachezaji wawili wa klabu hiyo ya London,
kiungo Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, na winga Gareth Bale, mwenye umri
wa miaka 22.
KLABU
ya Tottenham inapambana kuipiga bao Newcastle katika mbio za kuwania saini ya
winga wa Manchester United, kindaEzekiel Fryers, mwenye umri wa miaka 19, baada
ya beki huyo kugoma kuendelea kuichezea klabu hiyo mkataba wake utakapoisha
mwezi ujao.
MSHAMBULIAJI
Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, anataka kuondoka Chelsea baada ya
kukosa Euro 2012, huku Arsenal, Manchester City, Tottenham na Liverpool zote
zikiwa tayari kumsajili.
KLABU
ya QPR itakamilisha mpango wa kumsajili kipa wa West Ham, Robert Green wakati
mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32-akiwa kwenye Fainali za Kombe la
Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.
KLABU
ya West Ham ipo kwenye mazungumzo na Juventus kwa ajili ya winga Eljero Elia,
mwenye umri wa miaka 25, na wanajadili pia uhamisho wa mshambuliaji Luc
Castaignos, mwenye umri wa miaka 19, na Inter Milan.
TETESI ZA EURO 2012
MSHAMBULIAJI
wa Hispania, Alvaro Negredo amesema kwamba mabingwa hao wa dunia na Ulaya ni
bora wakutane kuliko Ufaransa katika Robo Fainali.
GWIJI
wa Denmark, Jan Molby amesema kwamba kiwango kibovu cha Christian Eriksen katika
Euro 2012 kinadhihirisha mwanasoka huyo wa kimataifa wa Denmark hayuko tayari
kuhamia klabu kubwa Ulaya.
BEKI
wa Croatia, Vedran Corluka, mwenye umri wa miaka 26, bado anataka kuondoka
Tottenham licha ya kuondoka kwa kocha Harry Redknapp.
AVB
APEWA MIAKA MIWILI SPURS
KOCHA
wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas ameripotiwa kupewa mkataba wa miaka
mitatu na Tottenham akarithi mikoba ya Harry Redknapp.
KOCHA
wa Ufaransa, Laurent Blanc naye anatajwa kuwa mbioni kumpiga bao Villas-Boas
katika kuwania kurithi mikoba ya Harry Redknapp kama kocha wa Spurs. Habari kamili: Sunday Mirror
NDOTO
za Tottenham kumnasa David Moyes zimeingia dalili za kuyeyuka baada ya kocha
huyo kuwa katika mpango wa kusaini mkataba mpya na Everton.
KLABU
ya Tottenham ilijiandaa kumtupia virago Harry Redknapp tangu miezi sita
iliyopita.
MCHEZAJI
anayewaniwa na Arsenal, Alan Dzagoev, mwenye umri wa miaka 21, mshambuliaji wa
kimataifa wa Urusi, amesema kwamba yuko tayari kwa dili hilo la kumtoa CSKA
Moscow ya nyumbani kwao.
KIUNGO
wa Manchester United, Luis Nani, mwenye umri wa miaka 25, anahofia anaweza
kulazimika kuondoka Manchester United kutokana na klabu hiyo kusuasua kumpa
mkataba mpya.
HAPPY BIRTH DAY MY DEAR FRIEND JIDEEEE
Zawadi
ilikuwa ni kutoka kwa Swahiba wangu Peter
Tulikuwa
wa nne ilipogonga saa 6 kamili usiku
Ni
siku yangu kubwa sina budi kujidai
"IT'S
MY BIRTHDAY"
Ndio
New Year kwangu
MUNGU
ndio alieamua niwepo tena, namshukuru sana
Me, Ibra and Khadija "GOBOS United"
Mazuri
machache ya kuwahusia ni haya:
Msivunjwe
mioyo na waliokwisha vunjika mioyo
Maana
hawana matumaini na hawatakuwa na busara za kuwashauri.
Msikatishwe
tamaa na waliokwisha kata tamaa, maana hawakumbuki nyuma na mbele wanaona
giza.
Mawazo
na maneno yao yatakuwa ni ya kusitisha safari yako isifikie mafanikio
RESPECT
TO MY MAMA "MARTHA MBIBO"
NI zaidi ya mwanamke.
Party
itakuwa Nyumbani Lounge karibuni tujumuike
Chuma
hakiunguzwi na moto wa Kiberiti
Ila
kinapata moto tu
MUCH
LOVE
JIDE
No comments:
Post a Comment