Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwaibambe. |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwaibambe. |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwaibambe. |
Jeshi la
Polisi mkoani hapa limemkamata na kumfikisha mahakamani Halima Sanga au Halima
Hamadi mkazi wa jijini Dar es Salaam, kutokana na kosa la kughushi vyeti na
kujipatia ajira serikalini ya udaktari wa daraja la pili kwa njia ya
udanganyifu, akijulikana kwa jina la Dkt. Sarah Matuja.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe,
alisema mtuhumiwa huyo ambaye aliajiriwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii
kama daktari bingwa, alipangiwa kufanya kazi katika hospitali ya rufaa ya
Ligula mkoani hapa na alianza kazi Mei 29 mwaka huu.
Alisema,
uchunguzi ulianza baada ya wagonjwa wengi waliokwenda kutibiwa hospitalini hapo
wakiwemo askari polisi kutoa malalamiko yao kutokana na kutoridhishwa na huduma
zake, ambapo alikua anashindwa hata kusoma vipimo na kuandika kama madaktari
wengine.
Alisema
baada ya kupta taarifa hizo, ofisi ya mkuu wa mkoa iliamua kumuandikia barua ya
kutaka uthibitisho wa uganga wake ambapo alijibu kuwa yeye ni mganga halali na
amefuzu kufanya shughuli hiyo lakini watu wanampiga vita.
“Uchunguzi
ulipoanza, alitakiwa kuripoti polisi lakini akawa anajificha..ila alikamatwa
Agosti 2 mwaka huu akiwa ndani ya basi la Msimbati Line akiwa anataka kutoroka
kuelekea jijini Dar es Salaam..” alisema.
Alisema
kuwa, jeshi la Polisi baada ya kujiridhisha kuwa ni mdanganyifu, likaanza kumtafuta
Dkt. Sara Matuja ambaye ndio jina alilokuwa akilitumia hospitalini hapo, na
kubaini kuwa Sara Matuja ni Mganga katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza na
ni daktari halisi baada kupata uthibitisho kutoka kwa baadhi ya watu
wanaomfahamu ikiwa ni pamoja na mwalimu wake aliemfundisha.
“Mtuhumiwa
tumemuhoji wapi alivipata vyeti vilivyomfanya apate ajira hiyo lakini
alishindwa kueleza, pia hata kututajia ndugu zake, kabila lake kwao wapi
alikataa..tumechunguza tumegundua ni msichana hatari sana, mwaka 2013
aliandikwa sana katika magazeti ya Uwazi akidai mara amebakwa na Mhe. Kapuya au
amezaane..ana majina mengi, Felister, Leylate, Leyta, Halima Hamad..”
aliongeza.
Aidha,
alisema ana kesi katika ofisi ya Ustawi wa Jamii wilaya ya Ilala jiini Dar es
Salaam juu ya matunzo ya watoto na mzazi mwenzie mtumishi wa serikali ambaye
hakutaka jina lake liandikwe, ambapo huko alitumia jina la Halima Sanga.
Nipashe
ilimtafuta Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Shaibu Maarifa kutaka kujuwa
undani wa jambo hilo, ambapo alizungumza kwa wasiwasi kwa madai kuwa kesi yake
ipo mahakamani huku akisema hakuna athari zozote za kimatibabu zilizosababishwa
daktari huyo.
“Hakukuwa na
athari zozote ila tu sisi tulipoona tuna mashaka juu ya utendaji wake tukampa
taarifa katibu tawala ambaye aliamua ufikisha taarifa katika vyombo vya ulinzi
na usalama..” alisema Dkt. Maarifa.
Alipoulizwa
kama aliwahi kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya huduma zake labda
ndio ilikuwa sababu ya kutokuwa na imani naye, alisema hakukuwa na malalamiko
yoyote lakini walimtiliashaka tu kutokana na utendaji wake.
“Aliripoti
hapa mwanzoni mwa mwezi Juni na tulimpokea kutoka katika ofisi ya katibu tawala,
maana ndio utaratibu huo kwahiyo kama haturidhiki nao ndio tunampa taarifa”
aliongeza.
Alisema
Daktari huyo alikuwa amewekwa katika kitengo cha kushughulika na wagonjwa wan
je (OPD) kwasababu ndio utaratibu ulivyo kwa madaktari wageni wanaoripoti na
alikuwa anafahamika kwa jina la Dkt. Sara.
Alitoa wito
kwa serikali kuwa makini na namna wanavyotoa ajira kwa kuchunguza vizuri vyeti
na tabia za waombaji, na iwe hivyo kwa katika taasisi zote sio tu kwa
hospitali.
Jitihada za
kumpata Dkt. Sara Matuja mwenyewe ambae ni mwajiriwa katika hospitali ya
Bugando, Mwanza hazikufanikiwa kutokana na simu yake kuzuiliwa katika ofisi ya
kamanda wa Polisi mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment