Mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo akifurahi pamoja na wananchi wa vijiji vya Mnali na Mapinduzi wilayani humo waliosota kwa miaka 12 bila kupata maji safi na salama. |
JUMA
MOHAMED, MTWARA.
Baada ya
kusota kwa muda wa miaka 12 bila kupata huduma ya maji safi na salama, wananchi
wa vijiji vya Mnali na Mapinduzi tarafa ya Kitangali halmashauri ya wilaya ya
Newala, sasa wameondokana na kero hiyo kwa jitihada za mkuu wa wilaya ya Newala
Aziza Mangosongo.
Wananchi hao
ambao awali walilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji, wameamua kuandaa
hafla ya mapokezi na kumpongeza mkuu wa wilaya huyo pamoja na kumkabidhi zawadi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mbuzi na Korosho, kwa kufanikisha kupatikana kwa
huduma hiyo katika vijiji hivyo.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mnali, Salehe Masoud, amesema wananchi wa vijiji hivyo waliamua
kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya kuwasilisha kero hiyo ndipo mkuu wa wilaya alipoamua
kwenda kuweka kambi ya siku Tatu akiwa na timu yake mpaka walipofanikisha
kutatua changamoto hiyo.
Wananchi wa
vijiji hivyo wamemuahidi kumpatia chumba mkuu huyo wa wilaya ili apumzike na
kupata Baraka za wazee, pindi akiwatembelea katika shughuli zake za kiutendaji.
No comments:
Post a Comment