Thursday, May 24, 2012

JUMA KASEJA BOSI WA WACHEZAJI STARS


Kaseja

NDOTO za mlinda mlango namba moja Tanzania, Juma Kaseja kuwa Nahodha wa timu ya taifa, zimetimia baada ya benchi la ufundi la Taifa Stars, kumteua kipa huyo wa Simba SC kushika wadhifa huo.
Maofisa wa benchi la ufundi la Stars, chini ya kocha Kim Poulsen, Wasaidizi wake, Sylvester Marsh na Juma Pondamali kwa pamoja na Meneja Leopold Mukebezi, baada ya kikao chao wamemteua rasmi Kaseja kuwa Nahodha wa timu hiyo, akirithi mikoba ya beki wa kulia, Nsajigwa Shadrack ambaye ameachwa kwenye kikosi hicho.
Hata hivyo, haijafahamika kama Kaseja atakuwa Nahodha wa kudumu wau muda wa Stars, kwa sababu chini ya Jan Poulsen, aliyekuwa kocha wa Taifa Stars kabla ya Kim, Shaaban Nditi ndiye aliyekuwa anapewa mikoba ya Unahodha Nsajigwa anapokuwa nje ya kikosi.
Hata mbele ya wachezaji wenzao, Nditi anakubalika zaidi kuliko Kaseja ambaye pia ni Nahodha wa Simba na wengi wanaamini uteuzi huo ungeshirikisha wachezaji- basi hiyo ingekuwa nafasi ya kiungo mkabaji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro.
“Kama tungepiga kura za siri, mimi nakuambia Nditi angekuwa Nahodha, ila hata Kaseja kwetu si tatizo, timu ina umoja na tutampa ushirikiano,”alisema kiungo mmoja wa Stars, akizungumza na BIN ZUBEIRY asubuhi hii, ambaye hakupenda kutajwa jina lake.

AMINI USIAMINI CHELSEA YAWATEMA BOSINGWA, KALOU


Jose Bosingwa and Salomon Kalou
24 May 2012Last updated at 05:20 GMT

Wachezaji wanaotemwa wote kutangazwa leo Stamford Bridge

KLABU ya Chelsea inajiandaa kuwatema Salomon Kalou na Jose Bosingwa mwishoni mwa msimu mikataka yao itakapomalizika.
Klabu hiyo itatangaza wachezaji inayowabakiza leo na majina yote ya wanaotemwa yatakuwa kwenye orodha moja na Didier Drogba.
Nyota huyo Ivory Coast tayari amekwishasema ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka minane, ili akakabiliane na changamoto mpya.
Bosingwa ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi Stamford Bridge, lakini klabu imeamua kumtema.
Kalou, ambaye pia anatokea Ivory Coast kama Drogba, alisajiliwa mwaka 2006 kutoka Feyenoord kwa dau la pauni Milioni 8.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amecheza mechi zaidi ya 250, ikiwemo ile aliyoanza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Chelsea na Bayern Munichon Jumamosi, na amewafungia mabao 60 The Blues.
Bosingwa, mwenye umri wa miaka 29, alisajiliwa na klabu hiyo baada ya kung'ara kwenye kikosi cha Ureno kwenye Euro 2008 baada ya Luiz Felipe Scolari, aliyekuwa kocha wa timu hiyo ya taifa kuchukuliwa kuikochi The Blues.
Beki huyo alitua kutokea Porto kwa dau la pauni Milioni 16.2, na amecheza mechi 127 katika kipindi chake cha miaka minne ya kuwa na klabu hiyo.

Wednesday, May 23, 2012

TORRES APEWA MKATABA WA MSHAMBULIAJI MKUU CHESLEA


Drogba anaondoka Chelsea, Torres anakuwa mshambuliaji mkuu

Gossip logo
23 May 2012Last updated at 22:58 GMT

Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

NEWCASTLE KUMPOTEZA DEMBA BA

KLABU ya Newcastle United itajitoa mhanga kumpoteza mshambuliaji wake mkali, Demba Ba mwenye umri wa miaka 26,msimu huu kwa kugoma kujadili naye marekebisho ya mkataba wake kuondoa kipengele cha kumruhusu kwa dau la pauni Milioni 7.
KLABU ya Chelsea ilikuwa ina dau la pauni Milioni 32.4 kwa ajili ya kumnunua kiungo chipukizi wa Brazil, Lucas Moura ambalo hata hivyo lilikataliwa na rais wa klabu yake, Sao Paulo, Juvenal Juvenico. "Lucas ni mchezaji babu kubwa mwenye ubora wa hali ya juu anayeisaidia sana timu ," Juvenico alisema kuhusu kinda huyo wa umri wa miaka 19, aliyeichezea mechi 11 timu yake ya taifa.
Newcastle striker Demba Ba
Demba Ba .
KLABU ya Manchester United inaandaa mamilioni ya kutosha kwa ajili ya mpachika mabao wa Montpellier, Olivier Giroud. Sir Alex Ferguson anataka kuanza majadiliano na washindi hao wa Ligue 1 kabla ya Euro 2012, kuangali uwezekano wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amezitupilia mbali tetesi kwamba klabu hiyo iko tayari kuwatoa washambuliaji wake Carlos Tevez au Mario Balotelli kama sehemu ya mpango wa kumpata mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27 wa AC Milan, Thiago Silva.
MSHAMBULIAJI wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 25, anataka kuchukua nafasi ya Didier Drogba katika mshambuliaji wa akiba katika kikosi cha Chelsea. Porto imetaka kiasi kisichopungua pauni Milioni 38 kwa ajili ya mshambuliaji wao huyo, lakini Chelsea haiwezi kutoa zaidi ya pauni Milioni 30.
KLABU ya Everton tayari imempata mbadala wa Leighton Baines, beki wa kushoto ambaye anaweza kutimkia Manchester United msimu ujao. Kocha Manager David Moyes amemtambulisha beki Mfaransa, Aly Cissokho, mwenye umri wa miaka 24, kama mbadala wake, ambaye wanaweza kumnunua kwa pauni Milioni 6.
NAHODHA wa Uholanzi, Mark van Bommel amemtaka mchezaji mwenzake wa kimataifa wa timu hiyo, Arjen Robben mwenye umri wa miaka 28, kufikiria kwa uzito wa juu kuhama Bayern Munich msimu huu, baada ya kuzomewa na mashabiki wa Munich katika mechi ya kirafiki baina ya timu hizo, Bayern na Ujerumani.. Winga huyo wa zamani wa Chelsea, anaweza kuvutiwa na klabu za Manchester United na Liverpool.
KOCHA wa AC Milan amepanga kuzungumza na Liverpool Juni kuhusu kiungo wa mkopo Alberto Aquilani. Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia, mwenye umri wa miaka 27, ameshindwa kucheza mechi kamili 25 akiwa na The Rossoneri, kiwango ambacho kinaweza kumfanya anunuliwe moja kwa moja kutoka Wekundu wa Anfield.
KLABU ya Manchester United inataka kumsajili Ezequiel Lavezzi, mshambuliaji wa Napoli kutoka Argentine mwenye umri wa miaka 27, kwa dau la pauni Milioni 25.
Habari kamili: Journal of Naples
KLABU ya Bolton ina matumaini ya kuendelea kuwa na kinda la Arsenal, Ryo Miyaichi kwa msimu mwingine katika Uwanja wa Reebok wakiwa na matumaini ya kurejea Ligi Kuu msimu ujao. Kiungo huyo wa The Gunners, mwenye umri wa miaka 19, amekuwa na msimu mzuri licha ya kwamba The Trotters wa meshuka daraja.

TORRES APEWA MKATABA WA MSHAMBULIAJI MKUU CHESLEA

BAADA ya kutishia anataka kuondoka Chelsea msimu huu, mshambuliaji wa Kispanyola, Fernando Torres amepokea fomu ya kuhakikishiwa na klabu hiyo kwamba atakuwa atakuwa mshambuliaji mkuu Stamford Bridge msimu ujao.
KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello, ambaye aliacha madaraka hayo February, hayumo kwenye orodha ya wamiliki wa klabu ya Liverpool katika makocha wanaotakiwa kuziba nafasi ya hiyo iliyo wazi Anfeld.
Chelsea striker Fernando Torres
Fernando Torres.

MAN CITY YAPATA HASARA BALAA


KLABU ya Manchester City imepoteza pauni Milioni 197 msimu uliopita, hasara kubwa mno ndani ya mwaka mmoja katika historia ya klabu hiyo. Klabu zote 20 za Ligi Kuu kwa ujumla zimepoteza pauni Milioni 361 mwaka jana, baada ya kutumia na kuvuka kiwango cha rekodi ya faida yao, pauni Bilioni 2.3.
KIUNGO wa zamani wa Bolton, Jay Jay Okocha anakumbuka enzi zake katika klabu hiyo, aliisaidia kuifanya Trotters kuwa moja ya timju imara katika Ligi Kuu, ingawa hiyo sasa imepotea. "Jitihada zetu zetu zimetupwa. inafikiriwa kama vile kazi yetu yote ilikuwa bure," alisema.



MTUKUTU BARTON ATUPWA JELA MECHI 12


EPL: Carlos Tevez - Joey Barton, Manchester City v QPR
Barton kulia akizunguana na Tevez anayeamuliwa na wachezaji wenzake wa Man City

Getty

NAHODHA wa QPR, Joey Barton amefungiwa mechi 12 na Chama cha Soka England kwa vurugu alizofanya kwenye mechi dhidi ya Manchester City katika siku ya mwisho ya msimu huu wa Ligi Kuu.
Barton ameongezewa adhabu ya mechi nane katika mechi nne za awali sambamba na kutozwa faini ya pauni 75,000.
Aligombana na Sergio Aguero na Vincent Kompany, lakini baada ya kupewa kadi nyekundu akamuanzishia na Carlos Tevez, na baadaye akawazingua marefa.
Pamoja na hayo hajaadhibiwa kwa kwa kumsukumia kichwa Kompany, Tume Kanuni imesema katika taarifa kwa kitendo alichomfanyia Sergio Aguero anastahili adhabu hiyo.

PIGO LINGINE TAIFA STARS, ULI MABAO AUMIA KIFUNDO CHA MGUU


Ulimwengu katika uzi wa Brazil

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu naye kuumia kifundo cha mguu.
Kuumia kwa Ulimwengu anayekipga katika klabu ya TP Mazembe ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunafa timu hiyo kufikisha majeruhi wawili ambapo jana, kiungo wake Nurdin Bakari alichanika nyama za paja hali itakayomlazimu kukaa nje ya dimba kwa siku saba.
Daktari wa Stars, Mwanandi Mwankemwa ameiambia mamapipiro blog Ulimwengu alipata maumivu hayo wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na maumivu hayo, Ulimwengu naye ataukjosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen akisaidiwa na Mzalendo Sylvestre Marsh imepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ikijiandaa mechi yake ya mchujo kufuzu Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa Abidjan Juni 2 mwaka huu.

SOURCE: DINA ISMAIL (http/mamapipiro.blogspot.com)

DROGBA AVUTIA MAELFU AKIKIMBIZA MWENGE WA OLIMPIKI LEO LONDON


Didier Drogba carrying the Olympic Flame
Didier Drogba na mwenge wa Olimpiki
Published: 34 minutes ago

NYOTA wa Chelsea, Didier Drogba aliwavutia maelfu ya mashabiki leo alipokuwa amebeba mwenge wa Olimpiki eneo la Swindon.

Drogba, ambaye alitangaza jana kubwaga manyanga Chelsea, aliwapungia mkono mashabiki wakati akiingia mjini na mwenge huo.
Wengi kati ya waliojitokeza kumuona shujaa wao wa kandanda, walikuwa wamevalia jezi za Chelsea.
Usiku huu, mwenge wa Olimpiki utamaliza mbio zake mikononi mwa Zara Phillips.
Mjukuu huyo wa kike wa Malkia,atakuwa nyuma ya farasi kubeba mwenge huo kuupeleka Cheltenham, kikomo cha mbio hizo maarufu.
Drogba, ambaye alikuwa mtu wa 84 kuushika mwenge huo leo, alipita barabara ya Commercial Road mjini Swindon katika eneo la maduka.
Barabara hiyo iligeuka kuwa bahari ya bluu, nyekundu na nyeupe kutokana na maelfu ya bendera, maputo na fulana za mashabiki wa soka.
Misururu pia ilijipanga katika mitaa ya Royal Wootton Bassett katika siku ya tano ya mbio hizo.
Courage ... Ben Fox
Ben Fox
Katikati ya Jiji sherehe zilikuwa kubwa mno na maelfu walijimwaga.
Shangwe kubwa ilikwedna kwa kijana Ben Fox, mwenye umri wa miaka 16, ambaye amepania kushiriki Olimpiki ya walemavu, maarufu kama Paralimpiki ya mwaka 2016.
Chipukizi huyo anayecheza mpira wa kikapu wa walemavu, alilazimika kubadilisha mikono mnara kadhaa wakati akiubeba mwenge huo, lakini alifanikiwa kumaliza kiwango chake cha kuukimbiza mwenge huo.

NCHUNGA AJIUZULU KUINUSURU YANGA


TANGU aondoke Mangara Tabru (sasa merehemu) katika klabu ya Yanga 1976, hapana shaka Imani Mahugila Madega ndiye Mwenyekiti pekee aliyefanikiwa kukaa madarakani hadi kumaliza muda wake, akiitisha uchaguzi na kumkabidhi madaraka kiongozi mwingine, Wakili mwenzake, Lloyd Baharagu Nchunga (pichani kushoto), Mei 18, 2010.
Kuna dalili za kutosha kabisa, Nchunga ameshindwa kuvunja rekodi ya Madega na kwa hali ilivyo wakati wowote anaweza kutangaza mwenyewe kujiuzulu, kwa nia nzuri tu ya kuinusuru Yanga.
Wanachama wanaodai idadi yao ilifika 700 wa Yanga walikutana Jumapili makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kufikia uamuzi wa kumng’oa madarakani Mwenyekiti, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga.
Mapinduzi haya yaliongozwa na Mzee Ibrahim Akilimali, ambaye kihistoria nilishasema siku nyingi ni mzee kinara wa migogoro na mvuruga amani klabuni, aliyetukuka.
Huyu alishiriki mapinduzi ya kumng’oa marehemu Rashid Ngozoma Matunda na akashiriki kumnyima amani Madega katika utawala wake, ingawa alichemsha. Mzee huyu alijaribu kugombea Uenyekiti wa Yanga dhidi ya Dk Jabir Idrisa Katundu mwaka 1993, lakini akajitoa mapema kwa sababu alikuwa hakubaliki.
Kweli, kwa sasa Nchunga ameshindwa kumudu kuongoza Yanga kwa ufanisi, na hiyo ni kwa sababu ya kukosa ushirikiano kutoka kwa Wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji na wadau wengine wa klabu, wakiwemo hao wanaojiita wazee na wafadhili.
Lakini ukirejea uchaguzi uliomuweka madarakani Nchunga Jumapili ya Mei 18, mwaka 2010, alishinda Uenyekiti baada ya kupata kura 1,437, akiwaangusha wapinzani wake wanne, Francis Kifukwe aliyepata kura 370, Mbaraka Igangula aliyepata kura 305, Abeid Falcon aliyepata kura 301 na Edgar Chibura aliyeambulia kura 65 katika kura 2,220 zilizopigwa, wakati kura 23 kati ya hizo ziliharibika.
Kura 370 za Kifukwe na 305 za Igangula kwa pamoja wakichanganya, bado hawawezi kufikia kura za Nchunga- ina maana alishinda kwa kishindo. Inakuwa rahisi kuhisi watu hawa 700 waliokutana Jumapili ni wale wale 700 waliomnyima kura Nchunga PTA Mei 18, 2010.
Lakini kwa sababu hiki ni kipindi kigumu ambacho Yanga inatakiwa kujipanga upya baada ya msimu mbovu uliopita, tena uliotokana na Nchunga kuhujumiwa na wapinzani wake, hakuna njia nzuri zaidi ya Wakili huyo kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya klabu. Wala Nchunga hataonekana mjinga- bali ataonekana jasiri na mwenye mapenzi ya kweli kwa klabu.
Alifanya kosa kubwa kuteua waliokuwa wapinzani wake kwenye uchaguzi katika Kamati zake- hao ndio waliomuumiza. Alifanya kosa kushindwa kuwa bega kwa bega na waliomsimika madarakani wamsaidie. Sasa anavuna matunda ya makosa yake. Aliwaamini sana watu wa Yanga, hakuwajua vizuri. Wengi wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi na ni wanafiki sana.
Inapofikia hapa, namkumbuka marehemu Syllersaid Salmin Kahema Mziray; aliwahi kusema Simba na Yanga zikifa na watu wengi watakufa kwa sababu maisha yao yote wanazitegemea hizo klabu- kwa Jangwani ndio hao Al Shabaab. Riziki yao inatokana na migogoro.
Kama nitapata fursa ya kukutana na Nchunga, nitamuambia ajiuzulu Yanga. Atakuwa amechukua uamuzi wa kijasiri na busara na ataheshimika daima milele. Sasa waingie hao Al Shabaab na walipe kisasi cha 5-0 za Simba. Tena wapewe miaka minne.
Siku zote nasema migogoro hii ya Simba na Yanga, serikali inaikumbatia, kwa sababu ukizama ndani ya historia ya timu hizi ni kama mali za umma tu hazina mwenyewe. Hivyo kila mwenye kadi anajifanya ana sauti na maamuzi, bila kuzingatia ana mchango gani.
Kwa misingi ya klabu hizi, ni vigumu kufa, ila migogoro haitaisha, hasa Yanga- kwa sababu kuna kigogo pale ana azma yake na inaweza kuwa nzuri, lakini njia anazotumia kutaka kuitimiza ndio shubiri kwa klabu hiyo.
Ni yule Yule aliyemnyima raha Madega katika utawala wake- sasa amepiga hatua kubwa. Kujaribu kupambana na migogoro ya Yanga kwa kupambana na akina Akilimali na Bakili Makele ni kazi bure- lazima litafutwe shina la matatizo klabuni- hawa ni matawi tu.
Sitaki kuamini eti pale alipo Leonard Thadeo, Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo au Leodegar Tenga, Mwenyekiti wa TFF hawajui kiini cha mgogoro huu wa Yanga- kama hawajui wakiniita nitawaleleza na kuwapa vielelezo au ushahidi, labda wakijua wataisaidia klabu hiyo.
Kuyumba kwa Yanga au Simba ni kuyumba kwa maendeleo ya soka ya nchi hii kwa ujumla pia- lakini pia Kilimanjaro Beer waliowekeza mamilioni yao pale Jangwani wanaupokeaje mgogoro huu?
Tazama kwa sasa kikosi cha timu ya taifa kuna mchezaji mmoja tu wa Yanga, hivi kweli kama klabu hiyo ingekuwa vizuri, leo sura ya Taifa Stars ingekuwaje? Ni kiasi gani kwa sasa mchango wa Yanga unakosekana timu ya taifa? Huu ni mfano mdogo tu.
Wanasema ni kidogo- japo mimi naona hakitoshelezi kulingana na bajeti yao wanachokipata kutoka TBL, lakini kisingekuwepo hali ingekuwaje Yanga?
Kama hakuna msaada wa serikali, au TFF ina maana Nchunga atasababisha matatizo makubwa zaidi Yanga- tu kwa kutokubali kujiuzulu katika vita ambayo tayari amekwishashindwa.
Madega alishinda vita hiyo kwa sababu kwanza alikuwa mzoefu wa siasa za Yanga na soka ya Tanzania kwa ujumla- akianzia kwenye ngazi za chini za uongozi mwaka 2000. Lakini Nchunga alikuwa mchanga katika siasa za soka za nchi na klabu hiyo kwa ujumla, nami nilijua hatafika mbali, hasa baada ya Davis Mosha kujiuzulu.
Alikubali kuhitilafiana na Mosha na akaridhia ajiuzulu, lakini hakuona athari zinazoweza kutokea mbele yake. Kama angekuwa ana Makamu wake Mwenyekiti leo na wapo kitu kimoja, angalau leo kidogo angekuwa ana nguvu.
Kile kimkutano cha nyuma ya jukwaa la Mkutano wa Uchaguzi na wagombea wenzake wa nafasi ya Mwenyekiti, leo ndio kinammaliza Nchunga. Alikubali ushauri ambao hakuufanyia kazi kwanza. Ndio, wahenga walisema mchawi mpe mwanao, lakini si katika dunia ya leo, anamuua kweli na anakuambia macho makavu; “Kazi ya Mungu”. Utafanya nini?
Madega alisimama kidete kupigana, alisimamisha wachezaji waliotumiwa na adui zake kuisaliti Yanga- alipambana na wazee, wafadhili na wanachama bila woga wala kuwatazama usoni. Ndio maana aliwaaga wana Yanga, akipigiwa makofi Mei 18, 2010 pale PTA tena akisema; “Mtanikumbuka”. Kweli, mimi ni mmoja wa wanaomkumbuka leo.
Madega hakuwa mnafiki, ukimkosea alikuwa anakuchana, na kesho mkikutana anakuwa wa kwanza kukusalimu. Ukikasirika shauri yako, ila yeye hakuwa wa kulea maradhi. Lakini naye aliwindwa kwa mikakati mizito ang’olewe, wakashindwa.
Unakumbuka alivyompa vidonge Manji? Nitakukumbusha;
“Habari hizo alizosema Manji juu ya uongozi wangu ni uongo mtupu, ukweli ni kwamba ujio wa Manji ndani ya Yanga unaonekana kama ni ukombozi wa kifedha, lakini ukweli ni kuwa amekuja kwa lengo moja tu, la kuiangamiza klabu ya Yanga kabisa na hatimaye kuunda kampuni ambayo kinadharia yeye ndio atakayekuwa mmiliki mkuu.” Kauli hii aliitoa Oktoba 11, mwaka 2007 baada ya kutokea kutoelewana kati yake na mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
Bado, kuna nyingine pia alimpa Manji, ngoja niwakumbushe;
“Kwa mawazo yangu, fedha hizo zilitolewa (na Manji) kwa lengo la kutugombanisha. Wachezaji wetu walicheza chini ya kiwango kwa kutambua kuwa wanavuja jasho, lakini fedha wanapewa wengine wasiowajibika uwanjani,”.
Kauli hii aliitoa Oktoba 26, mwaka 2007 akijibu kauli ya Yussuf Mzimba, aliyeutaka uongozi wake kueleza jinsi ulivyotumia shilingi milioni 40 zilizotolewa na mfadhili wao, Yussuf Manji kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inawafunga watani wao wa jadi, Simba Oktoba 24 mwaka huo mjini Morogoro. Manji pia aliwapa Sh. Milioni 10, wazee wa klabu hiyo chini ya Mzimba, lakini Yanga ililala 1-0, kwa bao pekee la Ulimboka Mwakingwe.
Hata Yanga waliokuwa wanaamini Yanga bila Manji haiwezekani, aliwapa kitu pia;
“Lakini pia ni vyema watu, hasa wanachama wa Yanga wakafahamu kwamba, mtoto huzaliwa na kukua, huwezi kutegemea kusaidiwa kila siku. Manji amefanya vitu vingi sana kwa klabu hii. Ametulea katika kipindi kigumu, wakati Uwanja wa Taifa ulipokuwa umefungwa, tulichezea Morogoro ambako fedha za kiingilio zilikuwa ni chache. Sasa tumehamia Dar es Salaam, timu inafanya vizuri mashindano ya ndani na nje, wanachama wanahamasika kuja kuishangilia na fedha zinapatikana. Tunaweza kusimama wenyewe,”.
Kauli hii aliitoa Februari 3, mwaka huu akizungumzia mustakabali wa klabu hiyo
Hata TBL nao pia aliwapa kitu, unakikumbuka? Nitakukumbusha;
“TBL haina uwezo wa kuiingilia Yanga kwa kututaka tuajiri Katibu Mkuu, makubaliano yetu ni kuajiri Mweka Hazina na tunatarajia kutangaza nafasi ya kazi wakati wowote kuanzia sasa, atakayetimiza vigezo tutamuajiri. Haya mambo si ya kukurupuka, nafasi kama ya Katibu Mkuu ni nyeti ambayo mshahara wake hauwezi kuwa Sh200,000, hapa tutaongelea milioni kadhaa, sasa bila kujipanga tutawezaje kumlipa?”
Kauli hii aliitoa Oktoba 3, mwaka 2008, kufuatia agizo la wadhamini wao, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kuwataka waajiri watendaji kama ambavyo mkataba baina yao unaelekeza.
Hata hawa wazee nao aliwapasha; nitakukumbusha;
“Mwisho nasema kuwa sitokuwa tayari kuiona Yanga ikiuzwa na kutawaliwa na mtu mmoja kwa nguvu ya pesa, masikini na mwanawe, tajiri na mali zake, Manji baki na mali zako au heshimu Katiba. Vinginevyo baki na mali zako au fadhili timu nyingine. Wazee na wanachama wachache waroho wa Yanga kuweni macho na msiwasaliti wazee wenzenu ambao walifanya juhudi kuifanya Yanga iwe na jina kubwa, mkiendelea kufanya hivyo kwa hakika historia itawahukumu, uongozi uko imara kutetea maslahi ya Yanga,”.
Kauli hii, Madega aliitoa Oktoba 11, mwaka 2007, kutokana na wazee na wanachama wa klabu hiyo kumuunga mkono Manji katika mgogoro wake na Madega.
Kwa staili hii Madega alikaa Yanga hadi mwisho wa muda wake wa kuwa madarakani, lakini Nchunga ameonyesha hana ubavu huo- njia nzuri kwake ni kuachia ngazi, wengi wanajua ngoma imemkalia vibaya hii na zaidi akiendelea kuleta ubishi kwa kuwa analindwa na Katiba, atazidi kuiumiza timu.
Sasa Yanga wanataka kusikia anasajiliwa mchezaji gani hodari wa kuunda kikosi imara cha kurejesha heshima msimu ujao, Nchunga bila msaada wa wafadhili ambao hivi sasa ndio wako dhidi yake, hataweza. Namshauri, aachie madaraka kuinusuru Yanga.


HAWA ISMAIL AWANOA MISS KIGAMBONI 2012

MAZOEZI kwa ajili ya kushiriki shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' yameshaanza mapema wiki hii imefahamika.
Shindano hilo limepangwa kufanyika ifikapo Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo tayari wameshaanza mazoezi kwenye ukumbi wa Break Point ulioko Posta jirani na Club Billicanas.
Alisema kuwa bado milango iko wazi kwa warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanakaribishwa kushiriki kuwania taji hilo.
Aliongeza kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
"Kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa katika kufanya mchakato wa kupata warembo wenye sifa ili waweze kwenda kuiwakilisha vyema Kigamboni katika mashindano ya Kanda," alisema Somoe.
Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen Kweka.
Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail (pichani) ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003.
"Bado tunakaribisha wadau wa sanaa ya urembo kutudhamini shindano hili, tunaamini uwepo wao ndio utafanikisha ubora na hadhi ya shindano letu mwaka huu kama tulivyodhamiria," aliongeza.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF.
Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.

SBL NMB WAIPIGA JEKI TWIGA STARS


Mafuru katikari, kocha Nasra kushoto na Kayuni kulia


Ktoka kulia Mama Yassoda, Kajula, Nasra, Kayuni na Mafuru anayekabidhi mfano wa hundi
KAMPUNI ya Bia Serengeti (SBL), kwa kushirikiana na Benki ya NBM, wameichangia timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars Sh. Milioni 30 pamoja na vifaa vya michezo, vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 5.5.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, yaliyofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru Balozi alisema kwamba wao wametoa Sh. Milioni 15 na NMB kiwango kama hicho pia.
Mafuru alisema baada ya hivi karibuni kutangaza kudhamini tuzo za wanamichezo bora za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), walifuatwa na serikali kuombwa kuisaidia Twiga Stars, ambayo haina mdhamini.
Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa kuisaidia timu hiyo, walikutana na NMB, ambao walikuwa wadhamini wenzao katika timu ya soka ya wanaume, Taifa Stars kabla ya kujitoa mwaka jana, wakakubaliana kuisaidia Twiga kwa kiwango hicho.
Mafuru pia ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuichangia timu hiyo, iliyopo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa NMB, Imani Kajula alisema kwamba wao kama wadau wakubwa wa michezo wameona umuhimu wa kuisaidia timu hiyo na pia kuanzisha kampeni ya kuitafutia misaada zaidi.
Alisema wamefungua akaunti inayoitwa; Changia Twiga Stars na amewataka wadau na makampuni mengine kuichangia timu hiyo kupitia akaunti hiyo. Kajula alisema anaamini kwa sababu benki yao inaongoza kuwa na matawi mengi nchini, itakuwa rahisi kwa wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo.
Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed aliwashukuru SBL na NMB kwa msaada huo na kuahidi matokeo mazuri katika mechi yao na Ethiopia Mei 27, mwaka huu mjini Addis Ababa.
Nasra pia aliwashukuru Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi walioitembelea timu hiyo kambini jana Ruvu na kutoa posho ya siku 16 kwa wachezaji na makocha wa timu hiyo. Nasra amewataka Watanzania kutokatishwa tamaa na matokeo ya timu hiyo kufungwa mechi mbili mfululizo za kujipima nguvun dhidi ya Zimbabwe na Afrika Kusini, kwani kupitia mechi hizo wameweza kubaini mapunfugu ya timu na kuyafanyia kazi na sasa wanaamini timu iko tayari kuleta matokeo mazuri.
Mapema katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Burton Kayuni alisema timu hiyo inakabiliwa na hali mbaya kifedha na kwa sababu hiyo, TFF ikaamua kusaka wafadhili kwa kushirikiana na serikali na akawashukuru SBL na NMB kwa kujitokeza.
Naye Ofisa wa Wizara ya Habari, Mama Juliana Yassoda, pamoja na kuwashukuru SBL na NMB, pia ametoa wito kwa makampuni mengine nchini kuiga mfano wa makampuni hayo kwa kusaidia timu hiyo, ili iweze kufuzu kwa mara ya pili mfululizo kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika, kwani ina uwezo huo ikipigwa jeki.

MAHAKAMA YAMGOMEA KAJALA HAKIMU MPYA

Kajala Masanja kuli, akiwa amejifunika usoni na kushoto katika pozi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya msanii wa filamu nchini Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo ya kutaka kesi yao ihamishiwe kwa hakimu mwingine ili iweze kuendelea kusikilizwa.
Kajala na mumewe waliwasilisha maombi hayo baada ya kupokea taarifa kuwa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yao Sundi Fimbo yupo likizo ya uzazi .
Maombi yao yalitupiliwa mbali na Hakimu Frank Moshi ambaye alisema amepokea jalada la kesi hiyo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi.
“Nimewasiliana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Ilvin Mgeta , amesema kwa kawaida shauri halifanyiwi mabadiliko iwapo hakimu yupo likizo na kwamba huo utakuwa ni usumbufu,” alisema hakimu huyo.
Baada ya uamuzi huo alipanga kesi hiyo iahirishwe hadi Juni 5, mwaka huu itakapotajwa mpaka hakimu atakapomaliza likizo yake.
Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo wanakabiliwa na mashtaka matatu kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu.

KESI YA MINTANGA JUNI 11

Mintanga
MAHAKAMA Kuu yaTanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Juni 11 mwaka huu kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Shaabani Mintanga ya kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8.
Kwa mujibu wa shajala ya Mahakama, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa siku hiyo mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib, ambaye alikuwa akiisikiliza tangu mwanzo.
Kesi hiyo iko katika hatua ya kusikilizwa mashahidi wa upande wa Jamhuri, ambapo mashahidi ambao wameshatoa ushahidi ni pamoja na Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) , Charles Ulaya na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi, Nassoro Michael.
Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2008, akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8.

JERRY SANTO, NSA JOB WATUA COASTAL UNION, MWALALA NA WASSO WATUPIWA VIRAGO

KLABU ya Coastal Union ya Tanga, ipo mbioni kumsajili kiungo Mkenya, Jerry Santo (pichani kushoto) aliyewahi kuchezea Simba SC.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Edo Kumwembe amesema mazungumzo yanaendelea juu ya mpango wa kumsajili nyota huyo, aliyecheza kwa mafanikio SImba SC.
“Tuko kwenye usajili sasa hivi, tayari tumeishawanasa wachezaji wawili na sasa tuko katika hatu ya mwisho na Jerry Santo,” alisema Edo.
Mapema jana, akizungumza na Habari Leo, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siag alisema, imewaacha wachezaji wake tisa wakiwemo Ally Ahmed ‘Shiboli’, Benard Mwalala na Ramadhani Wasso, Enock John, Laurent Mugia, Bakari Mohamed, Daudi Changula na Francis Busungu.
Katibu huyo alisema moja ya sababu za kuchukua uamuzi huo ni kutokana na kushuka kwa viwango vyao vya uchezaji na kwamba wana matumaini makubwa timu yao mwakani itakuwa moto wa kuotea mbali.
Alisema Kamati ya Usajili ya Coastal Union inaendelea na harakati za kufanya usajili wa nguvu kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi msimu ujao.
Aliwataja wachezaji ambao wamewasajili kuwa ni Nsa Job kutoka Villa Squad na kiungo Sudy Mohmed wa Toto Africans ya Mwanza.

 

WINGA WA LEOPARDS ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Image

Salim Kinje

WINGA Salim Kinje ametangaza kuondoka AFC Leopards ya Kenya na kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, timu ya Simba ya Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana kutoka Nairobi na kukaririwa kwenye mtandao wa, SuperSport.com
zimeeleza kuwa mchezaji huyo raia wa Tanzania, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuchezea timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, uamuzi huo wa Kinje kujiunga na Simba una nia ya kumuwezesha
kuonesha kiwango chake ili aweze kuchezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ambayo ndiyo ndoto yake kubwa.
Kocha Mkuu wa AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, Jan Koops amethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambaye pia humudu nafasi zote za kiungo na kusema kuwa hana muda mrefu watamkosa wakati wa kipindi cha usajili mwezi ujao.
Alisema Kinje alimjulisha jana kwamba amepata dau zuri Simba na anaondoka na kwamba amewasisitiza anahitaji kurudi nyumbani kucheza soka.
"Amenijulisha amepata ofa nzuri Simba na anaondoka, yeye ni Mtanzania anahitaji kurudi kwao kucheza soka.
“Ni mchezaji mzuri, tunapoteza mtu muhimu, alikuwa zaidi ya mchezaji, alikuwa nahodha
msaidizi na ndiyo utakapoelewa tumepoteza mchezaji wa aina gani," alisema kocha huyo.
Kinje ambaye amepata kuchezea Sofapaka ya Kenya, kuna wakati aliripotiwa kutakiwa kuitwa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars', wakiamini alikuwa Mkenya, lakini
uamuzi huo haukutekelezwa kutokana na yeye kuwa raia wa Tanzania na hakuwa tayari
kuupoteza.
 

Tuesday, May 22, 2012

MWANAMUZIKI WA ZAMANI ANAUMWA, ANAHITAJI MSAADA



Waraka huu nimetumiwa na mwanamuziki mahiri Benno Villa Anthony.................Mkuu, kwanza kabisa namwomba Mwenyezi Mungu akujalie roho ya uvumilivu ktk kufuatilia taarifa hii. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilikuwa na kipindi cha mahojiano na Manju wa muziki na mtangazaji wa TBC, komredi Masuud Masuud. Kwa vile kipindi kilirudiwarudiwa na huku Manju akitamka namba yangu ya simu, wengi waliinukuu, na kati ya hao walioinyaka ni Mzee John Mbulla, aliyekuwa mpiga sax wa Atomic Jazz. Mzee huyu kwa sasa kweli anaumwa sana. Zaidi ni maradhi ya macho, haoni. Kumbe kwao ni Mpwapwa ila kwa sasa anahifadhiwa na diwani wa Kibaigwa, Ndugu Richard Kapinye.......0717 303070. Baada ya kusikia kuwa wasanii wanachangiana ili kupata tiba, Diwani huyo alinipigia na nikazungumza nao wote wawili. Wameniomba nikupe taarifa hii ili uitoe kwenye vyombo vya habari, ikiwezekana apate msaada wa tiba. Diwani anasema kuwa John akipata operation ya macho atapona na kuanza kujitegemea maana nguvu bado anazo. KUMBUKA...Mzee John Mbulla ndiye aliyepiga Saxaphone kwenye wimbo wa "TANZANIA YETU NDIYO NCHI YA KUSIFIWA", wakati Mbaraka Mweshehe alipojiunga na Atomic Jazz kwa muda..............Mkuu Kitime, Nina uhakika kama wana Media wakimtembelea na kutoa habari zake, naamini wengi wataguswa na kumsaidia. Natanguliza shukrani zangu za awali. Asante Mkuu.

SOURCE: KIJIWE CHA KITIME
 

SAMA GOAL MAZOEZINI STARS

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars',Mbwana Samatta (wa pili kutoka kulia) akimpita beki Juma Nyoso (kushoto) na Erasto Nyoni (mbele), akiwa tayari kutoa msaada wakati wa mazoezi ya timu hiyo jana kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.Picha na Michael Matemanga.e&p

 

MAN UNTED KUSAJILI BEKI LA EVERTON


22 May 2012Last updated at 22:58 GMT

Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya

ARSENAL YATAKA KUSAINI KIUNGO BABU KUBWA

Etienne Capoue
Toulouse's captain Etienne Capoue has also been linked with Liverpool in the past
KLABU ya Arsenal imetega rada zake kwa Nahodha wa Toulouse, Etienne Capoue, mwenye umri wa miaka 23, kama chaguo mbadala la mchezaji wa Rennes, Yann M'Vila mwenye umri wa miaka 21, ikiwa ni sehemu ya jitihada za klabu hiyo kusajii kiungo mkabaji.
KLABU ya Manchester United imefungua mazungumzo na Everton ya kutoa dau la pauni Milioni 12 kumsajili beki wa pembeni, Leighton Baines.
MANCHESTER United ina matumaini ya kutumia vema nafasi ya hali hali ngumu ya kifedha inayoikabili klabu ya Rayo Vallecano kumnasa mchezaji Michu, mwenye umri wa miaka 26, kiungo aliyeongoza kwa kufunga mabao Hispania msimu uliopita, ambaye anaweza kutua Ligi Kuu kwa dau la pauni Milioni 3 msimu huu.
KLABU ya Arsenal itawauza wachezaji saba nyota akiwemo Nicklas Bendtner, Denilson, Sebastien Squillaci na Johan Djourou ili kukusanya fedha za kumsajili winga machachari wa Blackburn, Junior Hoilett mwenye umri wa miaka 21.
MSHAMBULIAJI wa England, Jermain Defoe amesema kwamba anakwenda kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 akifikiria mustakabali wake katika klabu yake, Tottenham.
KLABU ya Dynamo Kiev imeanzisha mazungumzo juu ya uhamisho wa wachezaji wawili wa Tottenham, Niko Kranjcar na Vedran Corluka, ambao unaweza kugharimu si chini ya pauni Milioni 10.
WINGA wa Wolves, Matt Jarvis mwenye umri wa miaka 25, anatakiwa na klabu ya Udinese kwa dau la pauni Milioni 5.
MSHAMBULIAJI wa Stoke, Cameron Jerome amekataa ofa ya kuhamia Wolves ili kubaki kuisaidia klabu yake kujaribu kupanda Ligi Kuu.

VAN GAAL KUTUA LIVERPOOL

Louis van Gaal
Louis van Gaal has won six domestic titles and one Champions League as manager
KOCHA Louis van Gaal anatajwa kama mshindani anayeongoza katika orodha ya watu wanaotakiwa Liverpool kwenye wadhifa wa Mkurugenzi wa Michezo. Mholanzi huyo aliyeonyesha nia ya kukubali kazi hiyo, amekuwa nje ya kazi tangu afutwe kazi Bayern Munich, Aprili, mwaka jana.
KOCHA Van Gaal anatarajia kufanya kazi na kocha mpya atakayeteuliwa kurithi mikoba ya Kenny Dalglish, aliyefukuzwa Liverpool.
KOCHA Roy Kean ameulizwa kama kocha mpya wa England na mchezaji mwenzake wa zamani Old Trafford, Gary Neville kama anastahili kazi hiyo.
MWENYEKITI mshiriki wa West Ham, David Gold amekata tamaa ya kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Joe Cole kurejea kwa mapenzi yake kwenye klabu hiyo ya Upton Park msimu huu.

No comments: