Kaburu kulia akimkabidhi Mama Zainab Sh. 500,000 |
MABINGWA wa
soka Tanzania Bara, Simba SC leo wamehitimisha Wiki ya Simba na Jamii, kwa kutoa
misaada yenye jumla ya thamani ya Sh. Milioni 1.5 katika kituo cha kulelea
watoto yatima, Maunga Orphanage Center, kilichopo Kinondoni Hananasif, Dar es
Salaam.
Baadhi ya
wachezaji wa Simba, Emanuel Okwi, Juma Nyosso, Uhuru Suleiman, Meneja Nico
Nyagawa, Daktari Cossmas Kapinga, Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga, Katibu Evodius
Mtawala na Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ walijumuika na watoto wa
kituo hicho kuwafariji.
Akizungumza
baada ya kukabidhi fedha taslimu Sh. 500,000 mbali na unga, mchele, sabuni na
bidhaa nyingine, Kaburu alisema kwamba huo ni mwanzo tu na watakuwa wakiendelea
kusaidia kituo hicho.
“Simba SC ni
taasisi kubwa, tunasema tumeguswa na kilio chenu, nasi tunaahidi kuendelea
kusaidia kadiri ambavyo tutakuwa tukipokea maombi kutoka kwenu,”alisema
Kaburu.
Akitoa
shukrani baada ya kupokea misaada hiyo, Katibu wa kituo hicho, Rashid Mpinda
aliwashukuru Simba SC na kuwatakia kila heri katika msimu ujao, kuanzia kwenye
Ligi Kuu na michuano ya Afrika.
Maunga
Orphanage Center kilianzishwa mwaka 2008 kikiwa na watoto wanne, chini ya
mmiliki wake, Mama Zainab Bakari na sasa kina watoto zaidi ya 60, kati ya hao 30
wakiwa wanaishi moja kwa moja kituoni hapo na 30 wengine wanashinda kituoni na
kwenda kulala kwa walezi wao.
Mama Zainab
alisema kwamba changamoto zinazowakabili mbali na kukosa eneo la kutosha kwa
malazi ya watoto na hata eneo la kufanyia michezo, lakini pia gharama za
kuwasomesha watoto hao pia ni baadhi ya changamoto nyingine
zinazowakabili.
Alisema
watoto wote waliofikisha umri wa kwenda shule, wanawasomesha katika shule za
Hananasif na Mkunguni na kinachowasumbua ni ada za watoto na michango mingine ya
shule.
Mama Zainab
alisema kituo chao hadi sasa hakina wafadhili, zaidi ya kutegemea michango ya
wadau kama ambayo Simba SC wametoa leo na pia misaada ya Diwani wao, Abbas
Tarimba.
Alisema
wanahitaji eneo lingine kubwa kwa ajili ya kujenga kituo kikubwa kitakachopokea
na kuhudumia watoto wengi zaidi, hivyo anaomba wajitokeze wafadhili wa
kuwasaidia.
Emmnauel
Okwi, Uhuru na Nyosso kama ilivyokuwa kwa viongozi wao, walionyesha kuguswa na
matatizo ya watoto hao na kuahidi binafsi kutembelea tena katika kituo hicho
kuwasaidia.
Katika
ratiba ya Wiki ya Simba SC na Jamii, mambo mawili tu yameshindikana kufanyika,
kutembelea shule ya Msingi Mgulani na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), ambao ni
wadhamini wa klabu hiyo kupitia bia ya Kilimanjaro Premeum Lager.
Katika
mfululizo wa Wiki ya Simba na Jamii, jana timu hiyo ilicheza mechi ya kirafiki
na Nairobi City Stars ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kufungwa mabao
3-1 katika Simba Day.
Lakini
kufungwa huko kwa Simba kulitokana na kocha Milovan Cirkovick kubadilisha karibu
kikosi kizima kilichoanza na kuingiza wachezaji wapya kipindi cha pili, ambao
waliitoa City Stars ya Nairobi nyuma kwa 1-0 na kuipa ushindi wa
3-1.
Simba
ilitangulia kupata bao kupitia kwa Felix Sunzu dakika ya 15, pasi ya Mwinyi
Kazimot na ilikwenda kupiumzika ikiwa mbele kwa bao hilo.
Lakini
kipindi cha pili, kipa aliyempokea Juma Kaseja, Hamadi Waziri alitunguliwa mabao
matatu katika dakika 57 na Duncan Owiti, dakika ya 64 na Bruno Okullu na dakika
ya 79 na Boniphace Onyango.
Mapema
katika tamasha hilo, Simba ilitoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa sasa na wa
zamani kwa mchango wao kwenye klabu hiyo, pamoja na baadhi ya wadau
wake.
Waliopewa
tuzo kwa wachezaji wa sasa, ni Shomary Kapombe (Nidhamu), Emmanuel Okwi
(Mchezaji bora wa msimu) na marehemu Patrick Mfisango (Heshima).
Wa zamani ni
Haidari Abeid ‘Muchacho’ (Mchezaji Bora miaka ya 1970), Hamisi Kilomoni
(Mchezaji Bora Miaka ya 1960), Ally Sykes (Heshima, Udhamini), Profesa Philemon
Sarungi (Mchango wa muda mrefu klabuni) na Gaorge Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro
Beer, Wadhamini wa sasa wa Simba SC.
Katika mechi
ya kwanza, timu na wanawake ya Simba, Simba Queens mchana, iliifunga Ever Green
ya Temeke mabao 5-3 katika mchezo wa Ligi ya Wanawake, Dar es Salaam uliokwenda
sambamba na tamasha la Simba Day, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shujaa wa
Simba alikuwa ni Maimuna Hamisi ‘Ronaldo’ aliyefunga mabao matatu, katika dakika
za tano, 62 na 64, wakati mabao mengine ya Malkia wa Msimbazi, walio chini ya
kocha Anthony Makunja, yalifungwa na Grace Tony dakika ya 48 na Neema Kuga
dakika ya 59.
Mabao ya
Ever Green yalifungwa na Sherida Boniface dakika ya 53, Vumilia Maarifa dakika
ya 55 na Amina Siraj dakika ya 61.
Viongozi, wachezaji Simba na watoto wa Maunga |
WIKI YA
SIMBA NA JAMII ILIVYOKUWA:
Agosti 5,
2012: Mkutano Mkuu wa mwaka Simba SC (Polisi Oystrebay)
Agosti 7,
2012: Kutembelea wagonjwa Mwananyamala hospitali
Agosti 8,
2012: Simba 1-3 Nairobi City Stars (Simba Day Uwanja wa Taifa)
Agosti 9,
2012: Kutembelea watoto yatima Maungu Orphanage Center
Uhuru na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Nyosso na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Nyagawa na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Kaburu na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Baadhi ya watoto wa kituo hicho |
BIN ZUBEIRY na baadhi ya watoto wa kituo hicho |
Mkwabi na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Pamba na mmoja wa watoto wa kituo hicho |
Nyagawa akikabidhi sembe, ngano na mchele |
Nyosso a Uhuru tayari kuondoka baada ya zoezi |
Kamwaga na Matari |
Baadhi ya watoto wa kituo hicho |
Uhuru akikabidhi sabuni |
Okwi akikabidhi dawa za kupigia mswaki |
Nyosso akikabidhi mafuta |
Wachezaji wa Simba na watoto wa kituo hicho |
Kaburu akimsikiliza Mama Zainab, mwenye kituo hicho |
Dk Kapinga kushoto, kulia Okwi na katikati Nyosso |
Mtawala akiwa na Katibu wa kituo hicho kulia na Mama Zainab kushoto |
No comments:
Post a Comment