SHUJAA WA SIMBA; Christopher Edward |
SIMBA SC
jioni imepata ushindi wa kwanza katika michuano ya BancABC Sup8r kwenye Uwanja
wa Ushirika mjini Moshi, baada ya kuifunga Mtende FC ya Zanzibar mabao
2-0.
Simba,
ambayo kwenye mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 na Jamhuri ya Zanzibar
pia, mabao yake katika mchezo wa leo yalifungwa na Christopher Edward dakika ya
11 na 26 kwa penalti.
Mtende
walilazimika kumaliza pungufu mechi hiyo, baada ya mchezaji wake, Rajab Mzee
kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 86 kwa kumtolea lugha chafu refa wa
kike, Judith Gamba.
Simba
inatumia kikosi chake cha pili kwenye mashindano haya, ambacho kipo chini ya
kocha Suleiman Abdallah Matola, Nahodha wa zamani wa Simba SC.
Katika
mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam walifungwa
mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mabao yote
ya Mtibwa yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa ni Shaaban Kisiga
‘Malone’ na Hussein Javu.
Mtibwa
iliyoifunga Polisi Moro 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, sasa inaongoza kundi hilo
kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi tatu, ambayo katika mchezo
wake wa kwanza, iliifunga Super Falcon 2-0.
MUAMBA ANAHITAJI UPASUAJI ZAIDI WA MOYO KUPATA MATUMANI YA KUCHEZA TENA
KIUNGO
Fabrice Muamba ameambiwa anahitaji upasuaji zaidi wa moyo, kama anataka
matumaini ya kucheza tena soka.
Kiungo huyo
wa Bolton yupo Ubelgiji kwa mtaalmu wa tiba za moyo, miezi mitano baada ya
'kufariki dunia kwa dakika 78' kwenye Uwanja wa White Hart Lane katika mechi ya
Kombe la FA dhidi ya Spurs.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24, amemtembelea mtaalamu Pedro Brugada kwa matumaini
ya kutimiza ndoto zake za kurejea uwanjani siku moja kucheza tena
soka.
Fabrice
Muamba
Muamba alipofariki kwa
dakika 78
No comments:
Post a Comment