Na
Mwandishi Wetu, Juma News
Taasisi
ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ina dhamana kubwa ya hatma
ya Elimu ya Ufundi nchini Tanzania, jambo linafanya elimu ya
Ufundi kuwa ya umuhimu hususan katika kipindi hiki ambacho agenda kuu ya
Taifa ni kujenga Uchumi wa Viwanda kwakujenga elimu ya ufundi
imara.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknlolojia, Dk
Leonard Akwilapo wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa NACTE jijini Dar es
Salaam leo Oktoba 4,2014.
Dk
Akwilapo alisema kuwa agenda hiyo inabidi ichukuliwe na Baraza hili kama
kigezo cha kupima utendaji wa kazi wa NACTE. “ Ni matumaini yangu kuwa wajumbe
wote wa Barza hili tunalolizindua leo watatambua hili na kutoa mchango
maridhawa katika Maendeleo ya Taifa na kufanikisha agenda ya Taifa ya “Uchumi
wa Viwanda”.alisema naibu katibu mkuu huyo
Alisemama
kwa sasa i uchumi wa dunia unaendeshwa katika misingi ya soko huria na Sekta
yetu ya Elimu haijaachwa nyuma katika hilo. Hata hivyo kwa kiasi kikubwa utoaji
wa Elimu nchini kwetu bado ni huduma. Hivyo basi NACTE lazima iwe makini katika
kusimamia uendeshaji wa Sekta hii, kwa kuzingatia maadili ili kuondoa huo
utata. Endeleeni na usimamiaji madhubuti wa Elimu ya Ufundi, msiyumbishwe na
wafanyabiashara wanaotaka kuharibu mfumo wetu wa elimu. Matarajio yenu
yaendelee kuwa ni utoaji wa elimu yenye ubora wa kiwango cha juu cha
mafunzo.
“Ni
RAI yangu kwa Baraza la Wafanyakazi kusimamia hili kwa nguvu zenu
zote. Msiposimama imara mtakuta mna vyuo batili, vyuo vinavyoendesha
mafunzo kiholela bila kufuata taratibu, na vitatoa wataalamu wasio na uwezo
unaolingana na kiwango cha vyeti wanavyotunukiwa. Baraza la Wafanyakazi
hamtakwepa lawama katika hali kama hiyo” alisema Dk Akwilapo
Alisema kuwa
uzinduzi wa baraza hilo lilikuwa ni muhimu sana katika historia ya Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), hii ni kwa sababu kama taasisi mmekuwa
hamna Baraza la Wafanyakazi kwa kipindi kirefu sana. Natambua kwamba kwa
kipindi chote cha uhai wa taasisi tangu ilipoanza shughuli zake takribani miaka
kumi na tano (15) iliyopita, mmekuwa mkiendesha shughuli zenu bila kuwa na
chombo hiki. Na hiyo ni kinyume kabisa na taratibu za utawala bora. Sina budi
kuwapongeza kwa kutambua hilo na kuamua sasa kuanza kutekeleza majukumu yenu
kulingana taratibu.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa alifahamu kuwa nia na juhudi za kutaka kuunda
Baraza la Wafanyakazi la Taasisi hii zilianza muda mrefu yapata miaka nane
(8) iliyopita. Changamoto iliyokuwepo na kukwamisha uundwaji wa Baraza hili
muhimu ilikuwa ni kutokuwepo kwa tawi la chama cha Wafanyakazi katika Taasisi
hii. Utaratibu wa kuundwa kwa Baraza la Wafanyakazi unahitaji kuwepo na
makubaliano ya pande mbili, upande wa Mwajiri kwa upande mmoja na Chama cha
Wafanyakazi mahali pa kazi kwa upande mwingine. Kwa sasa hali ni tofauti kwa
kuwa “TUGHE” moja ya chama cha Wafanyakazi nchini kimefanikiwa kuanzisha tawi
lake hapa na hatimaye kuwezesha kuundwa kwa Baraza hili la Wafanyakazi.
“Kwa
kutambua hili napenda nichukue fursa hii kulipongeza Bar
aza la Uongozi wa NACTE
na Menejimenti yake kwa jitihada mlizozifanya kuhakikisha kuwa tawi la chama
cha Wafanyakazi “TUGHE” linafunguliwa hapa na kisha kuunda Baraza hili la
Wafanyakazi. Baraza ambalo kuanzia leo linakuwa rasmi”, alisema Dk Akwilapo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi wa NACTE, Mhandisi, Stephen Mlote alitaja
majukumu ya baraza la wafanyakazi kuwa ni pamoja na kuwashirikisha wafanyakazi
wa NACTE katiak utekelezaji wa shughuli za NACTE kwa kushirikiana na uongozi.
Majukumu
mengine ni kushauri NACTE juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa
kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa huduma zitolewazo na NACTE ni za
kuridhisha na zimo katika lengo la kujenga Taifa.
Mwenyekiti
huyo alitaja majukumu mengine ya baraza hilo ni kushauri NACTE juu
ya mambo mengine muhimu yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment