Katibu wa afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula, Jenifer Mapembe, akiongea na Juma News. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
KUKITHIRI
kwa watoto wanaozaliwa na mtindio wa ubongo na kuharibika mimba kwa kina mama
ni miongoni mwa athari zinazoweza kuikumba mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na
kukosa matumizi ya chumvi yenye madini joto.
Hayo yameelezwa
na katibu wa afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula,
Jenifer Mapembe, baada ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara juu ya athari zitokanazo na matumizi ya
chumvu isiyo na madini joto na namna ya kuielimisha jamii.
Alisema mikoa
hiyo inaongoza katika orodha ya mikoa ambayo ina ukosefu wa chumvi ya madini
joto huku na kubainisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa katika kila kaya 100
katika mikoa hiyo, ni kaya 13 pekee ndio hutumia chumvi hiyo.
“Athari
zinazotokana na kutotumia chumvi yenye madini joto ziko nyingi sana mojawapo
ndio hiyo kwamba tunapata watoto ambao wana mtindio wa ubongo, watoto hawakui
vizuri ule udumavu wa watoto lakini pia kuna kuharibika kwa mimba, wanawake
wanapata mimba zinaharibika..” alisema.
Jenifer Mapembe |
Aidha,
aliwataka wazalishaji wa chumvi kuhakikisha wanaweka madini joto ili kuhepuka
kuwasababishia walaji madhara yaliyotajwa kwani madini hayo hutolewa bure bila
gharama yoyote, pamoja na wananchi kuitumia vizuri elimu ya matumizi ya chumvi
hiyo ambayo hutolewa kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya
habari.
Mwakilishi
kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamiii, jinsia, wazee na watoto Omary Gwao,
alisema mikakati ya wizara katika kuwakomboa wakazi wa mikoa hiyo kutoka katika
matumizi ya chumvi isiyo na madini joto ni pamoja na kutoa mafunzo kwa
wanahabari ili waweze kujua ukubwa wa tatizo na kupanga mikakati ya kuweza
kuisaidia jamii.
Afisa habari wa Ndanda Fc na mmiliki wa blog ya Bandari 44, Idrissa Bandari akitoa maoni yake. |
“lakini
mkakati mwingine ambao tumejiwekea kama wizara ni kuipeleka hii elimu pia kwa
watu wa afya ngazi ya jamii tunaita ‘community health workers’ sasa hawa pia
wameandaliwa ‘package’ yao ni tofauti kidogo wataenda kufundishwa ukubwa wa
tatizo lakii pia kuwatengenezea mkakati wa namna gani watashirikiana na jamii
kuhakikisha kwamba chumvi inakuwa na madini joto..” alisema.
Waandishi wa
habari walitoa mapendekezo yao walipotakiwa kutoa mikakati yao kupitia taaluma
yao ili kufanikisha kutoa elimu kwa jamii ihamasike na matumizi ya chumvi ya
madini joto.
Mwandishi wa gazeti la Habari Leo na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) Hassan Simba akitoa maoni yake. |
“Kwa mfano
Jumamosi iliyopita tulikuwa tunafanya usafi kwenye makaburi pale (Makaburi
Msafa), kwahiyo mnaweza mkasema kwamba siku ile ya kufanya usafi kutakuwa na
elimu ya matumizi sahihi ya nanii..(Chumvi ya madini joto) mkapewa nafasi
mkaielezea wakati huo sisi waandishi si tupo hapa tutakapokuwa tunaripoti
kuhusu hicho kitu tutakuwa tunasema miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni
pamoja na wananchi upewa elimu..” alisema Hassan Simba, ambaye ni mwandishi wa
Habari Leo.
No comments:
Post a Comment