Mbunge wa Cherengany, Wesley Korir. (PICHA: MTANDAO) |
Na
Mack Kemoli, Nairobi.
ALIYEKUWA bingwa wa boston marathon Wesley Korir ambaye ni mbunge wa eneo bunge la
Cherengany, magharibi mwa kenya ameteuliwa katika timu ya marathon ya Kenya
itakayowakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Olympic huko Rio De Janeiro
nchini Brazil, baadae mwaka huu.
Akiongea
baada ya uteuzi huo, Korir mwenye umri wa miaka 32 alisema,
“Lengo lango
ni kufanya mazoezi kwa juhudi zangu zote, niombe niwe mzima ili nitwae medali
kwenye mashindano hayo”.
Aliongezea
kwamba yeye na wenzake watafanya bidii watwae nafasi za kwanza tatu katika
mashindano hayo.
“
nina furaha kuwa mbunge wa kwanza popote duniani kushiriki katika
mashindano ya Olympic kama mwanariadha na sio mwana siasa”, aliongeza Korir. Akiongea na waandishi
wa habari, Korir alisema,
“sikuamini ningewakilisha nchi yangu kwenye
mashindano ya Rio, lakini licha ya majukumu ya kisiasa, nimeendelea kufanya
mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali, nawaahidi ushindi, mimi na wenzangu
tutakaowakilisha kenya kwenye mashindano ya Olympic”
Wesley Korir |
Wengine
watakaowakilisha Kenya kwenye mashindano hayo ya Rio kwa mbio za marathon ni
pamoja na bingwa wa marathon duniani msimu huu Eliud Kipchoge ambaye alishinda
mashindano ya London marathon mwaka huu pamoja na Stanley Biwott
aliyemaliza katika nafasi ya pili na ambaye pia alikuwa mshindi wa new York
marathon mwaka jana.
Katika
hatua nyingine,timu ya wanawake kwenye kitengo hicho inajumuisha washindi wa
mashindano ya riadha ya Dunia (IAAF) yaliyofanyika Beijing mwaka jana, ambao ni
Helah Kiprop, Jemima Sumgong na Visiline Jepkesho .
Waliokosa
kupata nafasi katika timu hiyo ni pamoja na bingwa wa dunia wa mbio za
marathon, Dennis Kimetto na mshindi wa tatu wa mbio za marathon za Olympic huko
London Wilson Kipsang .
Uteuzi
wa timu ya Kenya ya olympic unafanyika katika uwanja Kipchoge Keino mjini
eldoret. Uteuzi huo ulianza jana na unaendelea leo huku nafasi zikishindaniwa
kwenye vitengo mbalimbali.
Timu
hiyo itapiga kambi hapo hapo kabla ya mashindano hayo ya Rio.
Eneo
hilo la Eldoret ni zuri kwani ni ukanda wa juu zaidi na hutoa fursa kwa
wanariadaha kujinoa kabla ya mashindano. Zaidi ya wanariadha 1,000 kutoka
nchi mbalimbali wamepiga kambi mjini Eldoret kwa maandalizi hayo.
No comments:
Post a Comment