Na Juma Mohamed, Mtwara.
MSAFARA wa
kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ulioambatana na naibu waziri wa wizara
hiyo, Dkt. Medad Kalemani, ulizuiwa na wananchi wa kata ya Msimbati halmashauri
ya wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kuwasilisha kero zao kwa naibu waziri ikiwamo
gharama za umeme, kushuka kwa thamani ya ardhi na ubovu wa barabara.
Akizungumza
kwa niaba yaw engine, Mohamed Shaban, alisema mwananchi analazimika kulipia
hadi sh. 300,0000 pindi anapohitaji kupata nguzo ya kuvuta umeme nyumbani kwake
na kudai kuwa kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na hali ya maisha yao ilivyo
na kwamba hawaoni faida ya kuwa na mradi wa gesi asilia ambao mitambo yake
imejengwa huko.
Alisema,
licha ya kuwa gesi asilia imeanza kutumika kuzalisha umeme lakni bado kumekuwa
na tatizo la kukatika kwa huduma hiyo mara kwa mara jambo ambalo linayumbisha
shughuli mbalimbali zinazohitaji umeme.
“Vilevile
hata kama kuna mradi fuani kama wa uchimbaji visima au utafiti, fidia zile
hazieleweki haziko wazi, kuna wakati mita moja ya ardhi ni sh. 80 kuna wakati
sh. 1,170 kwa miaka ya nyuma ndio walilipa hivyo..lakini kadiri tunavyoenda
thamani inashuka baadala ya kupanda, siamini kama kuna kokote duniani ardhi
itashuka baadala ya kupanda..” alisema Shabani.
Wananchi |
Aidha,
walilalamikia ukosefu wa ajira kwa vijana wa eneo hilo ambao waliamini
kuondokana na tatizo kutokana na kuwapo kwa mradi wa bomba la gesi uliotoa
matumaini makubwa kwao na kudai kuwa wakihoji kwa wahusika wanaambiwa kuwa
shughuli nyingine zinahitaji wataalamu zaidi.
Walisema
walivyofanya uchunguzi waligundua kuwa shughuli hizo wanao uwezo wakuzifanya
huku wakichagizwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali
wakisisitiza kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozungukwa kwa miradi ya
uwekezaji wapewe kipaumbele cha ajira.
“Yani
tunachotoka tujue ni masilahi ya mradi kuwepo katika eneo lenu, sisi hapa hatujajua,
yani mradi upo hapa tulivyoambiwa tushirikiane tunashirikiana nao lakini lakini
hatujui masilahi yake..leo hii tukishaghairi tukasema afadhali wafanye tu sisi
hatuoni masilahi yake sawa..” alisema Salum Makanzu.
Kuhusu ubovu
wa barabara inayotoka Mtwara mjini kwenda Msimbati, alisema ilianza kufanyiwa
ukarabati wakati wa ujio wa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Mhe. Kassim Majaliwa, lakini kabla ya hapo hali ilikuwa mbaya zaidi.
Naye, Ismail
Msuti, alilalamikia Marine Park kuwa imekuwa ikizuia maeneo mengine ambayo
hayawahusu kwasababu awali walipewa kuhifadhi eneo la bahari ambalo ndilo
waliloomba.
“Shida kubwa
wamekuja kutuhifadhi na sisi wenyewe, kwamba mtu ukiwa na shamba kama unataka
kuliuza, huwezi kuuza mpaka Marie Park wakubali..kuna shamba la mzee mmoja
ilibidi ujengwe mnara wa voda na walisaini mkataba tayari, wakaja Marine Park wakazuia
wakidai ni eneo la hifadhi.. kwahiyo kwa kifupi sisi Marine Park hatuna faida
nayo na ni kero sisi wananchi..” alisema.
Akijibu hoja
za wananchi hao, naibu waziri, alisema hoja zao ni za msingi na kumtaka meneja
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara, Azizi Salum kutolea
maelezo ambapo alidai kuwa tatizo la kukatika kwa umeme ni kutokana na kuzidiwa
kwasababu laini inayopeleka umeme Msimbati ndio hiyo inayopeleka Tandahimba,
Newala, Masasi, Nachingwea na Ruangwa.
Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani. |
Kufuatia
tatiz hilo, naibu waziri alimwagiza meneja huyo kuwajengea kituo kidogo cha
kufua umeme (Sub Station) katani hapo ili umeme ukikatika Mtwara usikatike na
huko, na kwamba utekelezaji wa agizo hilo uanze kuanzia wiki jayo.
Kuhusu suala
la vijiji vinavyokosa umeme, alisema suala hilo lipo kwenye mpango wa
utekelezaji kupitia mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA) awamu ya pili ambao
unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
“Lakini
suala la gharama za umeme ni kweli ni kubwa sana kwa Mtwara, tulitarajia watu
wa Mtwara kwasababu gesi inagundulika huku munufaike wakwanza, lakini mnajua
kilichofanyika, gharama ya kuunganisha umeme kwa nchi nzima ni sh. 177,000
lakini kwa Mtwara tuliwaunganishia kwa sh. 99,000 tu mnalijua hilo?..kwahiyo tulishaanza
kufanya hivyo, lakini kweli itabidi tuanze kufanya uchunguzi wa kina tuone
namna gani nyie mnaweza kunufaika zaidi lakini kwasasa tumeshaanza kuchukua
hatua..” alisema.
No comments:
Post a Comment