Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
KUTOKANA
baadhi ya maeneo hapa nchini kukumbwa na matukio ya ujambazi, jeshi la polisi
mkoani hapa limewataka wananchi kutoa taarifa haraka iwapo watabaini kuwapo kwa
watu wakigeni wanaowatilia mashaka ili waweze kuchunguzwa na vyombo vya
usalama.
Akizungumza
na Juma News ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi
wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe, alisema vilevile wananchi wanapaswa
kuchunguzana wenyewe kwanza kwasababu hata wahalifu wa kigeni hawawezi
kutekeleza uhalifu bila kushirikiana na wenyeji.
“Na vilevile
ni ngumu sana mtu kutoka mbali huko na eneo lako kufanya uhalifu bila
kushirikiana na mwenyeji wake, kwahiyo naomba sana tuchunguzane mienendo
yetu..wiki iliyopita nilikaa na watu wa bodaboda na niliongea nao kwa kirefu
sana juu ya namna gani tunaweza kushirikiana juu ya kukomesha makosa ya wizi wa
pikipiki na makosa mengine..” alisema.
Alisema
aliwaeleza mambo mengi yanayowahusu na kusema kuwa matukio mawili kati ya
matatu yaliyoripotiwa polisi siku za nyuma yamewahusisha wanawake wanaokodi
pikipiki kwa ajili ya kupelekwa sehemu fulani alafu baadae anaomba akajisaidie
haja ndogo ndipo wanatokea vijana na kupora pikipiki.
“Ni mtu tu
anakodi pikipiki nipeleke Naliendele njiani anasimamisha ili akajisaidie kidogo
haja ndogo, wanajitokeza vijana wanapora pikipiki..sasa ni vyema unapochukua
hiyo pikipiki kwenye kundi la watu mufahamiane vizuri, sio rahisi mtu akapora
pikipiki yako bila kujua mwenendo wako, sasa hata mienendo yetu inabidi
tuiangalie vizuri nawaombeni sana..” aliongeza Mwaibambe.
No comments:
Post a Comment