Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe. |
Juma Mohamed, Mtwara.
Jeshi la
polisi mkoani Mtwara limewataka wananchi mkoani humo kusheherekea sikuu ya
Pasaka kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri
kuhakikisha ulinzi unahimarika katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na kumbi za
starehe na fukwe za bahari.
Akizungumza
na Juma News, kamanda wa polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alisema
wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao hawaendi kuogelea baharini
kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuwasababishia kuzama kwenye majini na kupoteza
maisha.
Aidha,
amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wakuendesha
vyombo vyao na kuhepuka kuendesha wakiwa wamelewa jambo ambalo linaweza
kumfanya akose umakini na kusababisha ajali.
No comments:
Post a Comment