Saturday, December 26, 2015

Homa yazidi kupanda pambano la Ndanda Sc Vs JKT Ruvu..Ushirikina wachukua nafasi yake.

Sehemu ya Lango Kuu la kuingilia uwanja wa Nangwanda Sijaona-Mtwara, kukiwa na vipande vya Chungu, Nazi na Mayai ambavyo vimevunjwa na watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa JKT Ruvu.


Vipande vya Chungu, Nazi na Mayai.


Ushirikina katikati ya Lango la kuingilia ndani ya uwanja wa Nangwanda-Mtwara



Gari ambalo walipanda wafuasi wanaoaminika kuwa ni wa JKT Ruvu ambao walifanya vitendo vinavyoashiria ushirikina katikati ya lango kuu la kuingilia uwanja wa Nangwanda Sijaona-Mtwara.


Gari likiondoka baada ya kukamilisha shughuli


Mmoja wa wafuasi wa timu ya Ndanda Sc ya Mtwara, akijaribu kukojolea mkojo sehemu iliyofanyiwa kitendo kinachoashiria ushirikina katika lango kuu la kuingilia uwanja wa Nangwanda Sijaona-Mtwara, kwa kuamini kufanya hivyo ni kuondoa makali ya ushirikina.



Mfuasi wa Ndanda Sc akifanya yake.



Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia kitendo kinachoashiria ushirikina kinachoaminika kufanywa na watu wa JKT Ruvu katika lango kuu la kuingilia uwanja wa Ngwanda Sijaona-Mtwara.


Mashuhuda.


Picha zote kwa hisani ya Fatuma Maumba.


No comments: