Sunday, October 18, 2015

CHAUMMA kuleta kilimo cha helkopta..

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Runwe, akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara juzi katika mkutano wa hadhara wa kunadi sera za chama na kuomba kura, uliofanyika katika eneo la Mti wa Miba.


Hashim Rungwe

 Na Juma Mohamed.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amesema iwapo atachaguliwa na kuingia madarakani ataanzisha kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia Helkopta.

Akihutubia wananchi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika mkutano wa hadhara wa kunadi sera na kuomba kura, alisema kilimo ndio tegemeo la wananchi walio wengi hapa nchini, hivyo lazima kuwe na mikakati kabambe ya kuboresha sekta hiyo.

Hashim Rungwe

“Mkinichagua nikawa Rais nitahakikisha tunakuwa na mashamba na kulima mwaka mzima na sio kwa misimu kama ilivyo sasa..hawa jamaa hawa (CCM) ‘wamechemsha’ betri zao hazina chaji, nchi hii kila kitu kinawezekana..” alisema.

Mogombea Mwenza wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Issa Abasi Hussein, akinadi sera za chama na kumuobea kura Mgombea Urais wa chama hicho, HashimRungwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi wilayani Masasi mkoani Mtwara.

 Awali, mgombea mwenza wa chama hicho, Issa Abasi Hussein, aliwataka wananchi hasa akina mama kuto shawishika na pesa kidogo kutoka kwa baadhi ya makada wa CCM ili kuwapa madaraka ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano huku wao wakitaabika na hali ngumu ya maisha.

Issa Abasi Hussein


No comments: