TUKUYU STARS
FAMILY
P.O.BOX
61989
DAR ES
SALAAM
05/JULY/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
NIA NA MKAKATI WA KUIFUFUA NA
KUIREJESHA TUKUYU STARS (BANYAMBALA) LIGI KUU TANZANIA
BARA
Tukuyu stars ni timu pekee yenye historia ya aina yake nchini Tanzania. Ilipanda
daraja mwaka 1985, ikachukua ubingwa mwaka 1986, ikashuka daraja mwaka 1987,
ikapanda tena daraja mwaka 1988 na baada ya misimu kadhaa ikashuka daraja na
kupotea katika ramani ya mpira nchini. Hii ni historia ya pekee , lakini cha
kukumbukwa zaidi ilikuwa ni uwezo wa kusakata soka la nguvu, kasi, akili na
ubunifu wa wachezaji chini ya mwalimu Athuman Juma (
marehemu).
Kutokana na mwenendo na uwezo wa Tukuyu stars, timu hii ilivuta mashabiki wengi
kila kona ya nchi na Duniani. Hivyo wadau, wapenzi na watu wengine walioguswa
na kupotea kwa Tukuyu stars kwenye ramani ya soka nchini wameanzisha mkakati wa
kuifufua na kuirejesha Tukuyu stars kwenye ramani ili tuendelee kupata ladha
tuliyoikosa, yaani zile burudani za akina Selemani Mathew, Karabi Mrisho,
Stephen Mussa ( marehemu), Salum Kabunda Ninja (marehemu), Ally Kimwaga, John
Alex, Richard Lumumba, Aston Pardon na wengineo. Hivyo lengo ni kuifufua na
kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa timu uwe wa kisasa hasa kampuni ili iwe
endelevu, shindani na inayojitegemea kiuchumi na kimaamuzi. Kwa maana hiyo
wadau, wapenzi na wengine wote wanaoguswa na kutokuwepo kwa Tukuyu stars
mnaalikwa kujumuika kwenye mpango huu.
Katika kufikia malengo yaliyowekwa wadau wameanza utekelezaji wa mpango huu
katika ngazi mbalimbali ikihusisha wadau waliopo Dar es salaam na wale waliopo
Mbeya.
<!--[if !supportLists]-->i)
<!--[endif]-->Vikao vya wadau waishio Dar es salaam
vimeanza na vinaendelea kila ijumaa kuanzia saa kumi na nusu jioni Kinondoni
Mkwajuni, Katumba bar. Mada kuu ikiwa ni namna bora ya kuifufua na kuirejesha
Tukuyu stars.
<!--[if !supportLists]-->ii)
<!--[endif]-->Wadau wa Tukuyu stars waliopo Mbeya
wanaendelea na vikao vya kufanikisha siku rasmi ya kongamano la kufufuka kwa
Tukuyu stars.
<!--[if !supportLists]-->iii)
<!--[endif]-->Ili kuleta hamasa na kuibua vipaji
vitakavyounda Tukuyu stars ijayo ligi ndogo imeanzishwa Wilayani Rungwe mahali
ilipozaliwa timu hii. Ligi hii inategemea kukamilika yaani Fainali zake kuwa
tarehe 04/08/2012
Siku ya fainali yaani tarehe 04/08/2012 inatarajiwa kuwa siku ya kujadili na
kufufuka rasmi kwa Tukuyu stars, hii ni siku muhimu na inatarajiwa kuwa na
matukio mengi na ya kusisimua. Kutakuwa na michezo mitatu ya utangulizi kabla
ya mchezo wa fainali, pia kutakuwa na ngoma za asili maarufu kama Ing’oma.
Michezo itakuwa kama ifuatavyo:-
<!--[if !supportLists]-->i)
<!--[endif]-->Mechi ya awali ya vijana chini ya
miaka 14 ( under 14) walioalikwa wakishindana na wenyeji
<!--[if !supportLists]-->ii)
<!--[endif]-->Mechi ya vijana chini ya miaka 17 (
under 17) itafuatia, pia ikihusisha timu waalikwa watakaoshindana na
wenyeji.
<!--[if !supportLists]-->iii)
<!--[endif]-->Baada ya mechi hizo zitafuatia ngoma
za asili
(Mang’oma)
<!--[if !supportLists]-->iv)
<!--[endif]-->Itafuatia mechi ya kukata na shoka ya
wakongwe (veterans )waliochezea Tukuyu stars na timu zingine waliopo Dar es
salaam chini ya mwalimu Kennedy Mwaisabula ‘’mzazi’’ wakishindana na wakongwe
wenzao (veterans) waliopo Mbeya wakiongozwa na Jimmy Mored na Alex
Mwambipile
<!--[if !supportLists]-->v)
<!--[endif]-->Baada ya mechi ya Veterans itafuatia
fainali ya ligi inayoendelea, ili kumpata bingwa wa mashindano yaliyoanza
June.
Kilele cha shughuli hii kitahitimishwa kwa kongamano kubwa la kuifufua rasmi
Tukuyu stars, mjadala huu utahusisha kuona namna bora ya kuendesha timu, na kama
ni kampuni basi uuzaji wa hisa utaanza siku hiyo kwa kuorodhesha majina ya wote
wanaopenda kununua hisa za kampuni na kujadili namna ya upatikanaji wa Bodi ya
timu na watendaji wa timu. Katika kongamano hili zitatolewa tuzo rasmi kwa
waanzilishi na viongozi wa Tukuyu stars, wanaotegemewa kupewa tuzo ni kama
Ramnik Patel Kaka (muasisi), mzee Kasyupa (katibu mkuu wa kwanza), mzee
Malakasuka, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Major General (mstaafu) Rashid
Nalihinga Makame , mzee Mwakasala na wale wote waliojitoa kwa hali na mali
kuifanya Tukuyu stars ing’are katika medani ya soka.
Pia vitakabidhiwa vifaa vya awali kwa
ajili ya kuanza rasmi kambi ya timu ya Tukuyu stars.
Maandalizi ya timu ya veterans waliopo Dar es salaam yanatarajia kuanza siku ya
jumamosi na kusimamiwa na mwalimu Kennedy Mwaisabula katika viwanja vya Harbours
Pub kurasini kuanzia saa mbili asubuhi. Wachezaji wanaotarajiwa kucheza mechi
hiyo na kuanza mazoezi ni:-
<!--[if !supportLists]-->i.
<!--[endif]-->Godwin Aswile ‘’Mlimba’’ ‘’Scania’’ (
Baba Subi).
<!--[if !supportLists]-->ii.
<!--[endif]-->Seleman
Mathew
<!--[if !supportLists]-->iii.
<!--[endif]-->Karabi Mrisho
<!--[if !supportLists]-->iv.
<!--[endif]-->Salum Kussi
<!--[if !supportLists]-->v.
<!--[endif]-->Asanga Aswile
<!--[if !supportLists]-->vi.
<!--[endif]-->Mbwana
Makata
<!--[if !supportLists]-->vii.
<!--[endif]-->Peter
Mwakibibi
<!--[if !supportLists]-->viii.
<!--[endif]-->Sekilojo
Chambua
<!--[if !supportLists]-->ix.
<!--[endif]-->Nsajigwa
Mwaisaka
<!--[if !supportLists]-->x.
<!--[endif]-->Geofrey
Amanyisye
<!--[if !supportLists]-->xi.
<!--[endif]-->Ezekiel (
Masatu)
<!--[if !supportLists]-->xii.
<!--[endif]-->Shedrack Nsajigwa
Fusso
<!--[if !supportLists]-->xiii.
<!--[endif]-->Christopher
Michael
<!--[if !supportLists]-->xiv.
<!--[endif]-->Lawrence
Mwalusako
<!--[if !supportLists]-->xv.
<!--[endif]-->John Mwansasu
<!--[if !supportLists]-->xvi.
<!--[endif]-->Deo Philip
Masanja
<!--[if !supportLists]-->xvii.
<!--[endif]-->Michael
Mbaruku
<!--[if !supportLists]-->xviii.
<!--[endif]-->Ally Kassimu
<!--[if !supportLists]-->xix.
<!--[endif]-->Nsangalufu
Joseph
Kupitia
taarifa hii tunawaalika wachezaji na wadau wote wanaopenda kushiriki kwenye
mazoezi na kucheza mechi hii wafike jumamosi asubuhi saa mbili katika viwanja
vya Harbours pub.
Vikao vya mikakati ya kufufua Tukuyu stars vinaendelea kila ijumaa saa kumi na
nusu jioni kinondoni Mkwajuni Katumba bar hivyo wapenzi na wadau wote mnaalikwa
ili tuweze kupanga kwa pamoja, pia tujadili namna ya kusafiri kwenda Tukuyu
Mbeya kwa ajili ya hiyo siku rasmi.
Michezo inaburudisha, inatoa ajira, inajenga undugu na zaidi ya hapo inawafanya
wanajamii wasahau tofauti zao na kuungana kusonga mbele katika maendeleo yao.
Tunawaombeni wadau wote wenye mapenzi mema na Tukuyu stars tuungane ili
turudishe heshima ya miaka ya 1980 wakati Tukuyu stars ikipambana na Simba ya
Dsm, Yanga ya Dsm, Pamba ya Mwanza, Ushirika ya Moshi, Mecco ya Mbeya, Coastal
Union ya Tanga, Nyota Nyekundu ya Dsm, Sigara ya Dsm, Pilsner ya Dsm, Lipuli ya
Iringa na timu nyingine. Tujumuike ili tuzalishe wachezaji mahiri kama Justin
Nicodemus Mtekele ( marehemu), Aston Pardon, Sekilojo Chambua, Hussein Zito,
Stephen Mussa ( marehemu), Jabir Mohamed ( marehemu), Peter Mwakibibi na
wengine wengi.
No comments:
Post a Comment