Kaburu akiwaonyesha Waandishi mkataba wa Okwi na Simba |
Mkataba wa Okwi na Simba |
Soma vipengele hapo |
Kaburu akizungumza na Waandishi wa Habari |
Kaburu akiwasikiliza sauti ya Okwi waandishi |
Hapa anafunguka kwa hisia kali |
Na Prince
Akbar
WAKATI Mshambuliaji Emmanuel
Okwi amekanusha kusaini Yanga, uongozi wa klabu yake, Simba umesikitishwa na
habari zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa
kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari mchana wa leo, makamo makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam,
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo
hazina ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na
zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na
Simba.
“Gazeti kama la Spoti STAREHE
limekwenda mbali zaidi kwa hatua yake ya kutaka kuufitinisha uongozi na wapenzi
na wanachama wake kwa kudai kuwa uongozi unafikiria tu kumuuza Okwi bila ya
kuangalia mkataba wake.
Kwa
mujibu wa gazeti hilo, mkataba wa Okwi umemalizika leo na ndiyo maana ameamua
kusaini Yanga akiwa mchezaji huru,”alisema Kaburu na kuongeza;.
“Ukweli ulivyo. Emmanuel Okwi
alisaini mkataba mpya wa kuichezea Simba mnamo mwaka jana na mkataba huo
unamfanya kuwa mchezaji halali wa klabu yetu hadi mwaka 2013. Baada ya mkutano
huu, nitawaonyesha waandishi nakala ya mkataba wa Okwi na Simba. Hivyo taarifa
kwamba mchezaji huyo hana mkataba na Simba ni za uongo, uongo
mtupu,”alisema.
“Hivi ninavyozungumza nanyi,
Okwi yuko kwao nchini Uganda akishughulikia viza ya kwenda nchini Italia ambako
anatarajiwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya vilabu
vya Ligi Kuu ya Italia (Serie A),”alisema Kaburu.
Okwi |
Aidha, alisema uongozi wa
Simba SC unavitaka vyombo vya habari vilivyoripoti kuhusu Okwi kuhamia Yanga
(gazeti la Bingwa na lile la Spoti STAREHE) kuomba radhi katika kipindi cha siku
saba kuanzia leo la sivyo uongozi utachukua hatua kali za kisheria dhidi
yao.
“Tayari tumewasiliana na
mwanasheria wa klabu ambaye ameelekeza kwamba ni lazima vyombo hivyo viombe
radhi na viuambie umma kwamba vilisema uongo na vinajutia kosa hilo la kimaadili
na habari hiyo itoke katika ukurasa wa mbele katika namna ileile ambayo habari
ya leo ilitoka.
Pia, uongozi wa Simba
unaviomba vyombo vya dola vichunguze ni nani anahusika na usambazwaji wa taarifa
hizi kwenye simu na vyombo vya habari kwani zina hatari ya kuchafua hali ya
amani na utulivu nchini,”alisema.
Aidha, Kaburu alimpigia simu
Okwi na kuzungumza naye huku akiwasikilizisha Waandishi wa Habari. Katika
mazungumzo hayo, alisema hana mpango wa kusaini Yanga na kwa sasa yuko kwao
Uganda akifuatilia visa ya kwenda Italia ndani ya siku mbili hizi, ambako
anatakiwa na klabu ya Parma ya Serie A.
“Akili yangu kwa sasa ni
kucheza Ulaya, na hata kama nitakosa nafasi Italia, basi kama ni kurudi
Tanzania, basi nitaendelea kucheza Simba siyo Yanga,”alisema Okwi katika
mazungumzo yake na Kaburu kwa simu kutoka Uganda.
Mbali na Parma, Okwi pia
anatakiwa na Etoile du Sahel ya Tunisia, Mamelodi Sundown na Orlando Pirates za
Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment