Wachezaji wa Azam (Picha kutoka maktaba) |
MABAO mawili ya mshambujliaji
wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche, jioni hii yametosha kuivusha
Azam FC hadi fainali ya Kombe la Urafiki, baada ya kuwafunga mabingwa wa
Zanzibar, Super Falcon 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Tcheche alifunga bao la kwanza
dakika ya 67, akiunganisha krosi ya Hamisi Mcha wakati bao la pili, alifunga kwa
penalti, dakika ya 77, baada ya Samir Haji Nuhu kuangushwa kwenye eneo kla
hatari na Samir Said dakika ya 77.
Kwa matokeo hayo, Azam
inasubiri mshindi wa mechi kati ya Simba SC na Zanzibar All Stars, mechi
inayoanza saa 2:00 usiku huu Uwanja wa Amaan kucheza naye fainali
keshokutwa.
Katika mechi hiyo, Azam
ilipata pigo dakika ya 54, baada ya mshambuliaji wake Gaudence Exavery Mwakimba
kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 54 kwa kumpiga kiwiko Abdul
Ally.
Katika mechi yake ya mwisho ya
Kundi A, Simba iliifunga kwa taabu Karume Boys 1-0, bao pekee la mshambuliaji
wake Mzambia, Felix Mumba Sunzu Jr, wakati Azam iliifunga Mafunzo
3-2.
Kuna uwezekano mkubwa Simba na
Azam zikakutana katika Fainali Jumatano, kwani Wekundu wa Msimbazi, ambao ni
mabingwa wa Tanzania Bara, wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi yao hiyo,
ingawa pia haitarajiwi kuwa kazi nyepesi kwani hata nyota wa Zanzibar nao ni
wazuri.
Kikosi cha Azam, inayonolewa
na Muingereza Stewart Hall, kilikuwa: Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu,
Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph Owino, George Odhiambo ‘Blackberry’,
Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao Mkami, Kipre Herman Tcheche/Hamisi Mcha, Kipre
Michael Balou/Abdulhalim Humud, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na
George Odhiambo ‘Blackberry’/Zahor Pazi.
Katika mchezo wa baadaye leo,
huenda kocha wa Simba Profesa Milovan Cirkovick akapanga kikosi hiki; Juma
Kaseja, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri
Kiemba/Edward Chirtopher, Mwinyi Kazimoto/Salim Kinje, Mussa Mudde/Jonas Mkude,
Felix Sunzu/Abdallah Juma, Kanu Mbivayanga/ Uhuru Suleiman na Danny
Mrwanda/Abdallah Seseme.
No comments:
Post a Comment