Monday, July 9, 2012
CHEKA BAIBAI TPBO
Date: Monday, July 9, 2012, 9:25 AM
> NDG WAANDISHI WA
> HABARI [MICHEZO]
>
> AWALI YA YOTE NINAPENDA KUTOWA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU
> KWA JINSI AMBAVYO VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA
> VIKITUSAIDIA SANA KATIKA KUUKUZA MCHEZO HUU WA NGUMI ZA
> KULIPWA KWA KUUANDIKA VIZURI SANA NA HATIMAYE KURUDISHA
> IMANI KUBWA KWA WAPENZI WAKE AMBAO TAYARI WALIKUWA
> WAMEUKIMBIA KUTOKAN NA SABABU AMBAZO MNAZIFAHAMU FIKA ,NA
> HATA WADHAMINI KUKAA PEMBENI NA KUUTELEKEZA KABISA.
>
> LKN MIAKA ANGALAU MINNE BAADA YA KUPOTEZA MWELEKEO HATIMAYE
> MASHABIKI WAMEUPOKEA TENA KWA MIKONO MIWILI ,
>
> HIVI KARIBUNI TAYARI PEPO MBAYA AMEANZA KUJITOKEZA KWA LENGO
> LA KUUVURUGA TENA MCHEZO HUU AMBAO NI NGUVU KAZI YA VIJANA
> KTK KUJIPATIA PESA ZA KUJIKIMU KIMAISHA KUPITIA NGUMI ZA
> KULIPWA.
>
> HIVI KARIBUNI VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKIRIPOT
> TAARIFA ZA MVUTANO MKUBWA ULIOJITOKEZA KATI YA BONDIA FRNCIS
> CHEKA NA WAANDAAJI WA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI KUHUSU
> PAMBANO LAKE NA JAPHET KASEBA HUKU CHEKA AKIKANUSHA KWAMBA
> HAKUSAINI MKATABA WA KUCHEZA NA JAPHET KASEBA NA BADALA YAKE
> ALISAINISHWA KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA MISRI.HAPO TAREHE
> 07-07-2912 KTK UWANJA WA TAIFA
>
> KIMSINGI TU CHEKA ANAJARIBU KUWAFANYA VIONGOZI WA KAMISHENI
> YA NGUMI ZA KULIPWA -TPBC HAWAJUWI WAJIBU WAO KWA KUMPA
> PROMOTA KIBALI CHA KURUHUSU PAMBANO AMBALO NI FEKI WAKATI
> SIYO KWELI ,
>
> MIMI BANAFSI NILIPATA NAFASI YA KUONGEA NA CHEKA NI KWA NINI
> ALIPIMA UZITO HALI AKIJUWA HATACHEZA PAMBANO ? NA KWA NINI
> ALIFIKA UWANJANI HALI AKIJUWA HACHEZI PAMBANO ? ALISHINDWA
> KUNIJIBU .MAHOJIANO HAQYA TULIYAFANYA SIKU YA PAMBANO NDANI
> YA UWANJA WA TAIFA.
>
> TPBO INAAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA LENGO LA FRANCIS CHEKA
> LILIKUWA NI KUJARIBU KUTENGENEZA MAAFA MAKUBWA AMBAYO
> YANGESABABISHA UVUNJIFU WA AMANI KWA KWA MASHABIKI AMBAO
> WALIKUJA MAHUSUSI KUANGALIA PAMBANO LILE .
>
> NDG ZANGU WAANDISHI WOTE HEBU JIULIZENI KAMA PAMBANO HILI
> LINGEKUWA NI LA KAWAIDA NA LIMEPANGWA KUFANYIKA KATIKA
> UKUMBI WOWOTE ,NA PROMOTA AMESHAWATOZA WATU PESA NA WAMEJAA
> UKUMBINI ,NA KISHA FRANCIS CHEKA AMEINGIA UKUMBINI NA KISHA
> KUKATAA KUPIGANA JE MNADHANI MASHABIKI WANGEKUBALI ? NI
> LAZIMA WANGEFANYA VURUGU KUBWA AMBAYO INGEWEZA HATA KUPTEZA
> MAISHA YA WATU WENGI SANA NA VYMBO VYENU VYA HABARI
> VINGEKUWA NA KAZI KUBWA SANA YA KUWAHABARISHA WATANZANIA JUU
> YA MAAFA HAYO AMBAYO YANGSABABISHWA NA UJINGA WA MTU MMOJA
> TU FRANCIS CHEKA.
>
> TPBO IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO HILI AMBALO LIMEUVUNJIA
> KABISA HESHIM A MCHEZO HUU ,NA HASA UKUZINGATIA KWAMBA
> VIKUNDI MBALIMBALI VILISHIRIKI KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI A
> WASICHANA ,NA HATA WAREMBO WALIJITOLEA KUPANDA ULINGONI KWA
> LENGO LA KUCHANGIA ELIMU.
>
> TPBO INAWAPONGEZA WASANII WOTE WA BONGO MOVIE ,WANAMUZIKI WA
> AINA ZOTE ,NA WABUNGE WOTE KWA MOYO WAO WA HURUMA
> WALIOUNYESHA KUFANIKISHA LENGO LA TAMASHA HILO .PIA PONGEZI
> KWA MABONDIA WOTE WALIOKUBALI KUSHIRIKIKUCHANGIA
>
> BONDIA FRANCIS CHEKA AMESHINDWA KABISA KUWATHAMINI WANAJAMII
> AMBAO KWA MCHANGO YAO WAMWEZA KUMFANYA AJULIKANE TANZANIA
> NZIMA ,NA AMEWADHARAU SANA NA AMUVJUNJIA HESHIMA MCHEZO WA
> NGUMI ZA KULIPWA KWA UJUMLA WAKE ,NA AMEUDHALILISHA
> SANA MCHEZO HUU MBELE YA JAMII YA KITANZANIA NA AMEWAFANYA
> MAADUI WASIOUTAKIA MEMA MCHEZO HUU KWA KUTOKUUDHANINI
> WAAMINI KWAMBA HUU NI MCHEZO WA WAHUNI NA WAVUTA BANGI .
>
>
> IMANI ZA TPBO
>
> -------------
>
> KUTOKANA NA MAELEZO YOTE NILIYOYATOWA KWENU NI VIZURI PIA
> MKAJUWA IMANI ZA TPBO
>
> [1] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA INAAMINIWA NA WATANZANIA
> WOTE WAPENDAO NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA NA
> INAZINGATIA NIDHAMU NA INAPIGA VITA UTUMIAJI WA MADAWA YA
> KULEVYA MICHEOZNI ,NA HATA BIASHARA YENYEWE YA MADAWA HAYO.
> KWA WANAMICHEZO WOTE NCHINI
>
> [2] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA NI KAZI
> KAMA KAZI NYINGINE AMBAZO HUMPATIA BINAADAMU KIPATO CHA
> HALALI ILI KUJIKIMU KIMAISHA.
>
> [3]TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA HAKUNA BONDIA YEYOTE MWENYE
> AKILI TIMAMU AWEZAYE KIDHARAU JAMII IILYOMZUNGUUKA NA
> KUFANYA AWEZE KUFANYA MABO AMBAYO YATAIKERA JAMII HIYO .
>
> [4] TPBO INAAMINI KWAMBA KILA BONDIA ANAZO HAKI SAWA ZA
> KUTETEWA NA KULINDIWA HAKI ZAKE PAKE ZINAPOKUWA HATARINI
> KUPOTEA.
>
> [5] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAKUZAJI [MAPROMOTA]
> WATAPEWA MSAADA MKUBWA PALE WANAPOANDAA MAPAMBANO YAO NA
> WANAPATA USHIRIKIANO WA DHATI KUTOKA KWA MABONDIA ,IKWA NI
> PAMOJA NA KUTANGAZIWA MAPAMBANO YAO KWA USHIRIKIANO MKUBWA
> NA MABONDIA WAHUSIKA.
>
> [6] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA
> WANAZO HAKI ZA KUPATA BURDANI YA MCHEZO HUU IL WAEENDELEE
> KUUPENDA KWA FAIDA YA MABONDIA WOTE .
>
> [7] TPBO INAAMINI KILA BONDIA ANAPASWA HUHESHIMIWA NA HAKUNA
> BONDIA ALIYE JUU YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO ZIENDESHAZO
> NGUMI ZA KULIPWA.
>
> NA TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA MWENYE MAMLAKA YA
> KUBADILISHA MPINZANI WA CHEKA NI PROMOTA NA SIYO BONDIA
> ,NDIPO CHAMA HUSIKA KINATOWA KIBALI KWA AJILI YA PAMBANO
> HILO ,NA NDIYO MAANA HATA RAIS WA TPBC KUPITIA VYOMBO VYA
> HABARI ALIUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KWAMBA ANAITAMBUWA
> MKATABA /MIKATABA ALIYOISANI FRANCIS CHEKA KUPAMBANA NA
> JAPHET KASEBA.
>
>
> MAAMUZI MAGUMU YA TPBO
>
> ---------------------------
>
> \ KWA KUWA JAMII YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA
> WAMEFADHAISHWA SANA NA TUKIO LILIOFANYWA NA BONDIA FRANCIS
> CHEKA NAMI NAUNGANA NAO KTK MFADHAIKO HUO NA KUWAOMBA
> MSAMAHA KWA TUKIO HILO ,NA ILI KUHAKIKISHA KWAMBA SOTE
> TUMEFADHAISHWA NA JAMBO HILO-;
>
> TPBO INAMUONDOWA RASMI BONDIA FRANCIS
> CHEKA KATIKA ORODHA YA MABONDIA INAOWATAMBUWA NA HAITAFANYA
> NAYE KAZI YA IANA YOYOTE KTK ULIMWENGU WA MASUMBWI KTK
> KIPNDI CHOTE CHA UHAI WA TPBO. NA UHAI WANGU BINAFI.
>
> HII HAINA MAANA KWAMBA ANAKATAZWA KUCHEZA NGUMI ,LA BALI HUU
> NI MSIMAMO WA TPBO ,NA DAIMA MIMI HUIFANANISHA TPBO NA SIMBA
> DUME LENYE MENO NA AMBALO HALITAKI KULA MIZOGA , LKN KAMA
> VIKO VYAMA NINAVYODHANI KWAMBA BILA CHEKA HAVIWEZI KUIMARIKA
> NA VIMTUMIE SINA PINGAMIZI NAVYO.
>
> TPBO IPO IMARA NA ITAENDELEA KUWA IMARA KWA KUFANYA KAZI NA
> MABONDIA WENYE NIDHAMU NA KATIKA MAAMUZI YETU HATUMUOGOPI
> YEYOTE ILI MRADI TUMO NDANI YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO
>
>
>
>
> AHSANTENI SANA
>
> NB- KWA TAARIFA HII NINAUFUNGA RASMI MJADALA KUHUSU BONDI
> FRANCIS CHEKA.
>
>
> IMEANDIKWA NAMI ;-
> YASSIN ABDALLAH
> -USTAADH
> RAIS-TANZANIA PROFESSIONAL BOXING
> ORGANISATION-TPBO
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment