Taifa Stars wakipasha |
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA | ||
KALENDA YA MATUKIO 2012-13 | ||
TUKIO | TAREHE | |
KIPINDI CHA KWANZA CHA MATAYARISHO YA MSIMU | 01 JUNI HADI 20 AGOSTI 2012 | |
KIPINDI KIKUU CHA MAPUMZIKO KWA WACHEZAJI | 01 JUNI HADI 30 JUNI 2012 | |
KIPINDI CHA KWANZA CHA UHAMISHO | 15 JUNI HADI 30 JULAI 2012 | |
KUTANGAZA WACHEZAJI WA KUACHWA (SIO WA LIGI KUU) | 15 JUNI HADI 30 JUNI 2012 | |
KUTANGAZA WACHEZAJI WATAKAOSITISHA MIKATABA | 15 JUNI HADI 30 JUNI 2012 | |
USAJILI WA KWANZA | 15 JUNI HADI 10 AGOSTI 2012 | |
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI | 11 AGOSTI HADI 18 AGOSTI 2012 | |
KUTHIBITISHA USAJILI HATUA YA AWALI | 19 AGOSTI HADI 20 AGOSTI 2012 | |
USAJILI HATUA YA PILI | 21 AGOSTI HADI 4 SEPTEMBA 2012 | |
KUTHIBITISHA USAJILI HATUA YA PILI | 5 SEPTEMBA HADI 6 SEPTEMBA 2012 | |
KUTAYARISHA TIMU KIPINDI CHA KWANZA | 01 JULAI HADI 20 AGOSTI 2012 | |
MECHI ZA KIRAFIKI ZIARA NDANI NA NJE YA NCHI | 01 JULAI HADI 20 AGOSTI 2012 | |
KUTOA RATIBA YA LIGI KUU | 23 JULAI 2012 | |
KIPINDI CHA KWANZA CHA MASHINDANO 25 AGOSTI HADI 04 NOVEMBA 2011 | ||
NGAO YA HISANI KUCHEZWA MIKOA YOTE KUFUNGUA MSIMU | 25 AGOSTI 2012 | |
LIGI KUU YA VODACOM MZUNGUKO WA KWANZA KUANZA | 01 SEPTEMBA 2012 | |
LIGI DARAJA LA KWANZA -NYUMBANI NA UGENINI KUANZA | 15 SEPTEMBA HADI 04 NOVEMBA 2012 | |
LIGI YA TAIFA | ||
NGAZI YA WILAYA KUANZA - MIKOA YOTE | 08 SEPTEMBA HADI 31 OKTOBA 2012 | |
LIGI YA WANAWAKE | ||
NGAZI YA WILAYA KUANZA - MIKOA YOTE | 08 SEPTEMBA HADI 31 OKTOBA 2012 | |
KOMBE LA FA | ||
HATUA YA AWALI - NGAZI YA WILAYA NA MKOA | 24 SEPTEMBA 2012 HADI 12 MEI 2013 | |
MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA VILABU | ||
KAGAME CUP | JULY 2012. | |
MASHINDANO YA CAF YA LIGI YA MABINGWA | JUL, AUG, SEPT, OCT, NOV,DEC, 2012 | |
MASHINDANO YA KOMBE LA CAF | JUL, AUG, SEPT, OCT, NOV, DEC, 2012 | |
MICHEZO YA KIRAFIKI NA MASHINDANO YA TIMU ZA TAIFA | ||
MCHEZO WA KIRAFIKI (TAREHE YA FIFA) | AUG, NOV, 2012 | |
MASHINDANO YA CAF/FIFA (TAIFA STARS) | JUNI, SEP, OKT,2012 | |
MASHINDANO YA KUFUZU FAINALI ZA CHAN | SEPT, OKT, 2012 | |
MASHINDANO CAF YA KUFUZU FAINALI ZA WANAWAKE | JUNI, 2012 | |
MASHINDANO YA KUFUZU FAINALI ZA AFCON | JUNI, AOG, SEPT, OKT, 2012 | |
MASHINDANO YA CAF KUFUZU FAINALI ZA U.20 | JUNI, JULAI, SEPT, 2012 | |
MASHINDANO YA CAF KUFUZU FAINALI ZA U.17 | SEPT, OKT, 2012 | |
CECAFA KARUME CUP U.20 | ||
CECAFA CUP U.17 | AGUSTI, 2012 | |
CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP | NOVEMBA, DESEMBA 2012 -KENYA | |
FAINALI ZA WANAWAKE | SEPTEMBA 2012 - EQUATORIAL GUINE | |
MASHINDANO MENGINE | ||
KOMBE LA KILIMANJARO LAGER (TBL) | 23 JULAI HADI 06 AUGOSTI 2012 | |
KOMBE LA BANK ABC | 01 AGOSTI HADI 19 AGOSTI 2012 | |
SHIMUTA | NOVEMBA 2012 | |
SHIMIWI | OKTOBA 2012 | |
MASHINDANO YA VIJANA - U.14 | ||
NGAZI YA WILAYA NA MKOA - MIKOA YOTE | NOVEMBA NA DESEMBA 2012 | |
MSHINDANO YA TAYSA | ||
MASHINDANO KUFANYIKA | NOVEMBA -DESEMBA 2012 | |
MASHINDANO YA SHULE - VYUO | ||
MASHINDANO YA UMISHUMTA | ||
MASHINDANO YA UMISETA | JUNI, 2012 | |
MASHINDANO YA SHIMIVUTA | DESEMBA 2012 | |
LIGI YA VIJANA WA LIGI KUU YA VODACOM U.20 | ||
LIGI YA VIJANA KUCHEZWA | 10 NOVEMBA HADI 25 NOVEMBA 2012 | |
KIPINDI KIFUPI CHA MAPUMZIKO | 15 NOVEMBA HADI 15 NOVEMBA 2012 | |
TUKIO | TAREHE | |
KIPINDI CHA PILI CHA MATAYARISHO YA MSIMU- 01 DESEMBA 2012 HADI 10 JANUARI 2013 | ||
KIPINDI CHA PILI CHA UHAMISHO | 15 NOVEMBA HADI 30 NOVEMBA 2012 | |
KIPINDI CHA PILI CHA USAJILI | 15 NOVEMBA HADI 15 DESEMBA 2012 | |
KUTANGAZA WACHEZAJI WA KUACHWA (SIO WA LIGI KUU) | 15 NOVEMBA HADI 22 NOVEMBA 2012 | |
KUTANGAZA WACHEZAJI WATAKAOSITISHA MIKATABA | 15 NOVEMBA HADI 22 NOVEMBA 2012 | |
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI | 16 DESEMBA HADI 23 DESEMBA 2012 | |
KUTHIBITISHA USAJILI | 27 DESEMBA HADI 28 DESEMBA 2012 | |
KUTAYARISHA TIMU KIPINDI CHA PILI | 01 DESEMBA 2012 HADI 31 DESEMBA 2012 | |
MECHI ZA KIRAFIKI ZIARA NDANI NA NJE YA NCHI | 01 DESEMBA 2012 HADI 12 JANUARI 2012 | |
KIPINDI CHA PILI CHA MASHINDANO - 01 JAUNARI HADI 31 MEI 2013 | ||
KOMBE LA MAPINDUZI | 05 JANUARI HADI 12 JANUARI 2013 | |
LIGI KUU YA VODACOM MZUNGUKO WA PILI KUANZA | 19 JANUARI HADI 28 APRILI 2013 | |
LIGI DARAJA LA KWANZA (FAINALI) KUCHEZWA | 26 JANUARY HADI 16 MARCH 2013 | |
LIGI YA TAIFA | ||
NGAZI YA MKOA KUCHEZWA | 05 JANUARI HADI 20 FEBRUARI 2013 | |
NGAZI YA KANDA KUCHEZWA | 01 MACHI HADI 25 MACHI 2013 | |
LIGI YA WANAWAKE | ||
NGAZI YA MKOA KWA MIKOA YOTE KUCHEZWA | 15 NOVEMBA HADI 20 DESEMBA 2012 | |
NGAZI YA TAIFA KUCHEZWA | 26 JANUARI HADI 24 FEBRUARY 2013 | |
COPA COCACOLA | ||
USAMBAZAJI WA FOMU NA USAJILI | 01 JANUARI HADI 30 JANUARI 2013 | |
MASHINDANO NGAZI YA WILAYA KUCHEZWA | 05 FEBRUARI HADI 30 MACHI 2013 | |
MASHINDANO NGAZI YA MKOA KUCHEZWA | 15 APRIL HADI 30 APRIL 2013 | |
KUANDAA TIMU KWA AJILI YA FAINALI YA TAIFA | 05 MEI HADI 30 MEI 2013 | |
KOMBE LA FA | ||
FAINALI ZA KOMBE LA FA | 12 MEI 2013 | |
MASHINDANO MENGINE | ||
MASHINDANO YA MAJESHI | MACHI 2013 | |
MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA VILABU | ||
MASHINDANO YA KOMBE LA CAF | FEB, MARCH, APRIL 2013 | |
MASHINDANO YA CAF YA LIGI YA MABINGWA | FEB, MARCH, APRIL 2013 | |
CECAFA KAGAME CUP | JULY, 2013 | |
KOMBE LA TAIFA | ||
MASHINDANO NGAZI YA MKOA KUCHEZWA | 05 APRILI HADI 20 APRILI 2013 | |
MATAYARISHO YA KWANZA YA TIMU YA MKOA | 22 APRILI HADI 04 MEI 2013 | |
KUWASILISHA USAJILI WA TIMU YA MKOA-TFF | 27 APRILI 2013 | |
KUPITIA MAJINA NA KUTANGAZA PINGAMIZI | 29 APRILI HADI 05 MEI 2013 | |
KUPITISHA USAJILI | 05 MEI 2013 | |
MASHINDANO NGAZI YA TAIFA- MAKUNDI | 05 MEI HADI 12 MEI 2013 | |
MATAYARISHO YA PILI YA TIMU YA MKOA | 13 MEI HADI 18 MEI 2013 | |
FAINALI NGAZI YA TAIFA | 21 MEI HADI 27 MEI 2013 | |
MICHEZO YA KIRAFIKI NA MASHINDANO YA TIMU ZA TAIFA | ||
MCHEZO WA KIRAFIKI (TAREHE YA FIFA) | FEB, 2013 | |
MASHINDANO YA CAF/FIFA (TAIFA STARS) | MARCH, 2013 | |
TFF YATOA ANGALIZO, MWONGOZO, UFAFANUZI UCHAGUZI YANGA
<!--[endif]--><!--[if
!mso]-->
|
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KUHUSU UCHAGUZI
WA KUJAZA NAFASI ZA UONGOZI WA KLABU YA YANGA
10 JULAI
2012
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa
kuzingatia majukumu yake ya kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF kama
ilivyoanishwa kwenye Katiba ya TFF, Ibara ya 49 (1), na Kanuni za Uchaguzi za
wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu uchaguzi wa
kuziba nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga:
<!--[if !supportLists]-->1.
<!--[endif]-->Wanachama
wote wa TFF, ikiwa ni pamoja na Klabu ya Yanga, wanatakiwa kuzingatia kikamilifu
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF katika kuendesha shughuli zote za
uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->2.
<!--[endif]-->Wagombea
uongozi wote wa wanachama wa TFF wanapaswa kutimiza masharti ya uongozi
yaliyoanishwa katika Katiba za vyama vyao na Kanuni za
Uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->3.
<!--[endif]-->Kamati
za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinapaswa kutimiza kikamilifu majukumu yao ya
kulinda Katiba za wanachama wa TFF na kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama
wa TFF katika michakato ya uchaguzi. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilishaelekezwa
kufanya hivyo na inakumbushwa kuendelea kuzingatia wajibu
huo.
<!--[if !supportLists]-->4.
<!--[endif]-->Wagombea
uongozi wa wanachama wa TFF wanao wajibu wa kuzifahamu Katiba zao na Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kuomba uongozi kwa kutimiza matakwa ya Katiba na
Kanuni za Uchaguzi.
<!--[if !supportLists]-->5.
<!--[endif]-->Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imepokea maombi ya marejeo (review) dhidi ya uamuzi wake wa
kuwaondoa waombaji uongozi wanne (4) wa Klabu ya Yanga. Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inatoa uamuzi ufuatao:
<!--[if !supportLists]-->i)
<!--[endif]-->Marejeo
yaliyoombwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga yanakiuka Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF, hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeyakataa. Kamati inafafanua
kuwa hata kama Kanuni zingekuwa zinaruhusu
kufanya marejeo, bado maombi hayo yasingepaswa kuwasilishwa na Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga, bali waombaji uongozi wenyewe. Pamoja na hayo, sababu za
kuomba marejeo si za msingi kwa kuwa waombaji uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya
Yanga walipewa mwongozo wa kutosha kurekebisha upungufu uliojitokeza katika
mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi za uongozi kwenye Klabu ya
Yanga.
<!--[if !supportLists]-->ii)
<!--[endif]-->Sara
Ramadhani
hakutimiza masharti ya kuomba uongozi kwa mujibu wa Ibara ya 10(4) na (5) ya
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kama ilivyoanishwa kwenye Fomu namba 1
kwa kutojaza fomu na kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za kugombea. Kwa
hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga kuliondoa jina lake katika orodha ya wagombea uenyekikiti wa
Klabu ya Yanga.
<!--[if !supportLists]-->iii)
<!--[endif]-->Shaaban
R. Katwila
na Ahmed Waziri Gao wameshindwa kutimiza masharti ya uombaji uongozi kwa
kutowasilisha vyeti halisi kwa ajili ya uhakiki kama ilivyotakiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania
(NECTA) baada ya nakala za vyeti vyao kubainika na NECTA kuwa vina utata. Kamati
ya Uchaguzi ya TFF inaitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutekeleza uamuzi wa
kuondoa majina yao kwenye orodha ya wagombea uongozi wa
Yanga.
<!--[if !supportLists]-->iv)
<!--[endif]-->Ramadhan
Mzimba Kampira
ameshindwa kutimiza masharti ya kugombea uongozi kama yalivyo kwenye Ibara ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi
za Wanachama wa TFF kwa kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za mgombea. Kwa
hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga kuondoa jina lake katika orodha ya wagombea
uongozi.
<!--[if !supportLists]-->v)
<!--[endif]-->Kamati
ya Uchaguzi ya TFF inaridhia uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga
kuwaondoa wafuatao kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi:
<!--[if !supportLists]-->(a)
<!--[endif]-->Ally Mayay
Tembele
<!--[if !supportLists]-->(b)
<!--[endif]-->Abdallah
Sharia Ameir
<!--[if !supportLists]-->(c)
<!--[endif]-->Jamal Hamisi
Kisongo
<!--[if !supportLists]-->(d)
<!--[endif]-->Mohamed R
Mbaraka
<!--[if !supportLists]-->vi)
<!--[endif]-->Wagombea
uongozi ambao hawakutajwa hapo juu na ambao walipitishwa na Kamati ya Uchaguzi
ya Yanga, wametimiza matakwa ya awali ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF
na hatua za mwisho za uhakiki wa vyeti vya elimu yao , zinaendelea.
Angetile
Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
TFF YAPATA MSIBA MWINGINE
Na Prince
Akbar
SHIRIKISHO la Soka Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha Soka
Mara (FAM), Fabian Samo kilichotokea leo asubuhi (Julai 10 mwaka
huu).
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace
Wambura Mgoyo, ameaimbia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, Samo ambaye Novemba 13
mwaka jana alichaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa FAM
katika uchaguzi uliofanyika wilayani Rorya alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya
figo.
Wambura amesema taratibu za
mazishi ya Samo ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu (Internal
Audit Committee) ya TFF ikiwemo siku atakayozikwa bado zinafanywa na familia
yake.
Amesema Samo alitoa mchango
mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Mara na Tanzania kwa ujumla, vitu ambavyo
vilichangia kuchaguliwa kwake tena kuiongoza FAM.
Amesema msiba huo ni pigo kwa
familia ya Samo, FAM, TFF na mchezo wa mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana
na mchango na mawazo aliyotoa kwa kipindi chote alichokuwa
kiongozi.
Amesema TFF inatoa pole kwa
familia ya marehemu Samo, FAM, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu
katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa
familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu
Samo mahali pema peponi. Amina
Wakati huo huo: Wambura
amesema kwamba, wakati wa mechi za Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu, screen kubwa iliyoko uwanjani itatumika
kwa matangazo ya biashara na ujumbe mbalimbali kwa washabiki watakaoshuhudia
mechi hizo.
Amesema TFF inakaribisha
kampuni na wadau mbalimbali wanaotaka kuweka matangazo yao wakati wa michuano
hiyo itakayoshirikisha klabu kumi na moja kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki
na Kati.
Amesema muda wa kurushwa
matangazo hayo yanayotakiwa kuwa kwenye mfumo wa DVD ni kabla ya mechi kuanza,
wakati wa mapumziko na baada ya mechi. Matangazo hayo yanatakiwa kuwa ya sekunde
60 (dakika moja) au sekunde 30 (nusu dakika).
Aidha, Wambura amesema kwamba
Kozi ya makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu
(wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza leo (Julai 10
mwaka huu) kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es
Salaam.
Amesema Wakufunzi kutoka
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ndiyo wanaoendesha kozi hiyo
iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile
Osiah.
Amesema Kozi hiyo
itakayomalizika Julai 15 mwaka huu inashirikisha washiriki 35, na mwendelezo wa
ile ya awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka jana jijini Dar es
Salaam.
Amemtaja Gouinden Thandoo
kutoka Mauritius ni mmoja wa wakufunzi wa FIFA wanaoendesha kozi hiyo
No comments:
Post a Comment