ZAWADI DAKIKA |
Friday, June 8, 2018
MAAFISA UTUMISHI NA WATAALAMU WA AFYA RUVUMA NA DAR WAJENGEWA UWEZO MFUMO WA WISN PLUS POA MTWARA
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Wednesday, June 6, 2018
WAHASIBU NA WAWEKA HAZINA WA HALMASHAURI MTWARA NA LINDI WAIVA KIMABADILIKO YA MFUMO WA EPICOR 10.2
Siku Nne za
kuwajengea uwezo Wahasibu na Waweka hazina wa halmashauri za mikoa ya Mtwara na
Lindi, juu ya mabadiliko ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2)
hatimae zinakamilika leo huku watumishi hao wakiwa wameiva kwa masomo
waliyopewa na wawezeshaji kutoka TAMISEMI.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Tuesday, June 5, 2018
MAAFISA UTUMISHI NA WATAALAMU WA AFYA MTWARA WANOLEWA JUU YA UPANGAJI WA WATUMISHI KATIKA VITUO
Kutokana
na kuwapo kwa changamoto ya uhaba wa watumishi katika halmashauri mbalimbali
mkoani Mtwara ambayo inadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na mrundikano wa
watumishi kwa baadhi ya maeneo, Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, ikaamua kuendesha mafunzo kwa
maafisa utumishi na wataalamu wa afya, kuwajengea
uwezo juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa
kuzingatia mahitaji.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Monday, June 4, 2018
PS3 YAWAJENGEA UWEZO WA KIMIFUMO WAHASIBU NA WAWEKAHAZINA WA HALMASHAURI MTWARA NA LINDI
Uzinduzi wa Mfumo wa Uhasibu Ulioimarishwa kwa Ajili ya Kuboresha Uwazi, Usimamizi na Utoaji wa Huduma kwa Wananchi wa Tanzania.
Tarehe 1 Julai 2018, Serikali ya Tanzania itaanza kutumia mfumo mpya wa uhasibu kwa Mamlaka za
Serikali za Mitaa185 za Tanzania bara, kwa msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Kwa mara ya kwanza, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa
nchini Tanzania zitatumia mfumo mmoja wa uhasibu ujilikanao kama Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za
Umma, tolea la 10.2 (Epicor10.2), utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu, utoaji taarifa
na usimamizi wa fedha.
Uzinduzi wa mfumo huu mpya utafuatiwa na mafunzo ya kina ya wiki tatu kwa watumishi 950 na wale wa
kada za uhasibu kutoka katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa 185 za Tanzania bara kuanzia Juni 4,
2018. Mafunzo haya yataendeshwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) pamoja na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). Mafunzo
yatafanyika katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mtwara, Mbeya, Kagera na Mwanza.
Moja kati ya maboresha makubwa katika mfumo mpya wa usimamizi wa fedha za umma ni kushushwa
kwa mfumo hadi kwenye ngazi ya mtoa huduma. Kwa sasa matumizi yote yanayofanywa na Mamlaka
za Serikali za Mitaa kwa vituo vyake vya afya na shule yatahifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya
kutolea huduma pamoja na jamii wanayoitumikia.
Maboresho mengine katika mfumo wa usimamizi wa fedha za umma katika tolea la 10.2 (Epicor 10.2) ni
kwamba mifumo yote ya msingi ya usimamizi wa fedha katika sekta za umma kwa sasa itaweza
kuwasiliana na kushirikishana taarifa. Hapo awali, uongozi na maafisa katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa walilazimika kupitia mipango na bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumo mwingine na
matumizi kwenye mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika kudhihirisha uwajibikaji, ufanisi na
thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za Serikali.
Mfumo wa Epicor 10.2 utaunganishwa na mfumo unaowezesha mabenki kulipana Tanzania (TISS)
ambao utaruhusu malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki. Mfumo pia unahusisha Muundo mpya
wa uhasibu (New Chart of Account) pamoja na Kasma Mpya ya 2014 (GFS) kama ilivyoelekezwa na
Wizara ya Fedha na Mipango. Matoleo yaliyopita ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma
yalijumisha hitilafu za kiufundi ambazo zilididimiza mbinu bora za uhasibu na taratibu za usimamizi wa
fedha, na kusababisha kuwepo kwa hati chafu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali.
Kwa ufupi, mfumo wa usimamizi wa fedha za umma wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao unashuka
hadi katika ngazi ya kutolea huduma, mfumo unaoweza kuongea na mifumo mingine ili kuboresha
usimamizi na kupunguza lawama, utafanikisha kuwepo kwa usimamizi bora wa kifedha na uboreshaji wa
utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa
katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili
kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye
uhitaji.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Thursday, April 12, 2018
PS3 YAENDELEA KUWANOA WANAHABARI NA WANATEHAMA WA SERIKALI
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
WAHAMIAJI HARAMU 23 WAKAMATWA KATIKA NYUMBA ZA WAGENI MTWARA
MTWARA
Wahamiaji
haramu 23 ambao ni raia wa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi na
Rwanda wamekamatwa mkoani Mtwara wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba za kulala
wageni.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mtwara Lukas Mkondya, alisema baada ya kuahoji watuhumiwa hao,
wote wamekiri kusafirishwa na mfanyabiashara raia wa jijini Dar es Salaam
ambaye bado hajakamatwa aliyedhamiria kuwapeleka nchini Ufaransa.
“Baada ya
kupata taarifa hizo askari walikwenda kufanya upekuzi katika nyumba za wageni,
na kufanikiwa kuwakamata hao wahamiaji 23 ambao wameingia nchini kwetu kinyume
cha sheria..katika mahojiano hayo, wahamiaji hao wametoka katika nchi
zifuatazo..kuna wahamiaji wametoka nchi ya Kongo au Zaire, kuna wengine
wametoka nchi ya Rwanda na wengine ni raia wa Burundi.” Alisema Mkondya.
Katika tukio
lingine, jeshi hilo limewakamata watu 13 kutoka katika kijiji cha Chikongo
wilayani Tandahimba kwa tuhuma za kuhusika na wizi sugu wa pikipiki katika maeneo
mbalimbali ya nchi.
Aidha, jeshi
hilo linawashikilia wanafunzi Tisa wa chuo kikuu kishiriki cha Stella Maries
mkoani Mtwara ambao wanatuhumiwa kuhamasisha maandamano pamoja na kuchapisha
lugha za kumkashifu Rais.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Wednesday, April 11, 2018
MAAFISA HABARI WA MIKOA NA HALMASHAURI WATAKIWA KUBADILIKA KIUANDISHI
MTWARA
Maafisa habari wa serikali za
mikoa na halmashauri nchini wametakiwa kubadilika katika uandishi kwa kuacha
kuandika habari za viongozi pekee na baadala yake wajikite katika kuandika
habari zinazowagusa wananchi.
Akizungumza jana mkoani Mtwara katika mafunzo ya kuwajengea uweo
maafisa habari na maafisa TEHAMA wa mikoa Minne nchini, afisa habari wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atley Kuni, alisema kitendo cha kuandika habari
za viongozi peke katika tovuti zao kinawafanya wananchi wajione kama wametengwa
na kutoona umuhimu wa kutembelea tovuti hizo.
“Kubwa tunalosisitiza
kwasababu hii ipo sehemu ya kipengele kimoja katika masuala ya utawala bora,
kwa maana ya kuwashirikisha wananchi..wananchi wanashirikishwaje ni kuhakikisha
habari ambazo zinaandikwa sasa zina sawidi ya kile ambacho wanakifanya kwenye
maeneo yao..” alisema Atley.
Faith Shimba ni Mshauri wa
mifumo ya TEHAMA katika Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3,
ambaye alieleza lengo la kuendesha mafnzo hayo kwa maafisa habari na maafisa
TEHAMA kuwa ni baada ya tathmini iliyofanywa na TAMISEMI pamoja na PS3 na kubaini
mapungufu yakiutendaji kwa maafisa hao.
Baadhi ya washiriki wa
mafunzo hayo akiwamo afisa habari wa mkoa wa Mtwara Evaristy Masuha na afisa
habari wa manispaa ya Kinondoni, Martha Kawishe, walieleza kuwa mafunzo hayo
ytawasaidia kuwajenga kitaaluma sambamba na kuahidi kubadilika katika uandishi
wa Tovuti zao.
Mafunzo hayo ya siku Nne
yanayoendeshwa na Mradi wa Uimarshaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3,
yamejumuisha maafisa habari na maafisa TEHAMA wa halmashauri na mikoa Minne ya
Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Ruvuma.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Subscribe to:
Posts (Atom)