Monday, June 4, 2018
PS3 YAWAJENGEA UWEZO WA KIMIFUMO WAHASIBU NA WAWEKAHAZINA WA HALMASHAURI MTWARA NA LINDI
Uzinduzi wa Mfumo wa Uhasibu Ulioimarishwa kwa Ajili ya Kuboresha Uwazi, Usimamizi na Utoaji wa Huduma kwa Wananchi wa Tanzania.
Tarehe 1 Julai 2018, Serikali ya Tanzania itaanza kutumia mfumo mpya wa uhasibu kwa Mamlaka za
Serikali za Mitaa185 za Tanzania bara, kwa msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Kwa mara ya kwanza, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa
nchini Tanzania zitatumia mfumo mmoja wa uhasibu ujilikanao kama Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za
Umma, tolea la 10.2 (Epicor10.2), utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu, utoaji taarifa
na usimamizi wa fedha.
Uzinduzi wa mfumo huu mpya utafuatiwa na mafunzo ya kina ya wiki tatu kwa watumishi 950 na wale wa
kada za uhasibu kutoka katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa 185 za Tanzania bara kuanzia Juni 4,
2018. Mafunzo haya yataendeshwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) pamoja na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). Mafunzo
yatafanyika katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mtwara, Mbeya, Kagera na Mwanza.
Moja kati ya maboresha makubwa katika mfumo mpya wa usimamizi wa fedha za umma ni kushushwa
kwa mfumo hadi kwenye ngazi ya mtoa huduma. Kwa sasa matumizi yote yanayofanywa na Mamlaka
za Serikali za Mitaa kwa vituo vyake vya afya na shule yatahifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya
kutolea huduma pamoja na jamii wanayoitumikia.
Maboresho mengine katika mfumo wa usimamizi wa fedha za umma katika tolea la 10.2 (Epicor 10.2) ni
kwamba mifumo yote ya msingi ya usimamizi wa fedha katika sekta za umma kwa sasa itaweza
kuwasiliana na kushirikishana taarifa. Hapo awali, uongozi na maafisa katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa walilazimika kupitia mipango na bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumo mwingine na
matumizi kwenye mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika kudhihirisha uwajibikaji, ufanisi na
thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za Serikali.
Mfumo wa Epicor 10.2 utaunganishwa na mfumo unaowezesha mabenki kulipana Tanzania (TISS)
ambao utaruhusu malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki. Mfumo pia unahusisha Muundo mpya
wa uhasibu (New Chart of Account) pamoja na Kasma Mpya ya 2014 (GFS) kama ilivyoelekezwa na
Wizara ya Fedha na Mipango. Matoleo yaliyopita ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma
yalijumisha hitilafu za kiufundi ambazo zilididimiza mbinu bora za uhasibu na taratibu za usimamizi wa
fedha, na kusababisha kuwepo kwa hati chafu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali.
Kwa ufupi, mfumo wa usimamizi wa fedha za umma wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao unashuka
hadi katika ngazi ya kutolea huduma, mfumo unaoweza kuongea na mifumo mingine ili kuboresha
usimamizi na kupunguza lawama, utafanikisha kuwepo kwa usimamizi bora wa kifedha na uboreshaji wa
utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa
katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili
kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye
uhitaji.
I'm a Blogger, and News Reporter at East Africa Radio and Nipashe-News Paper. Available in Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment