MTWARA
Wahamiaji
haramu 23 ambao ni raia wa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi na
Rwanda wamekamatwa mkoani Mtwara wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba za kulala
wageni.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mtwara Lukas Mkondya, alisema baada ya kuahoji watuhumiwa hao,
wote wamekiri kusafirishwa na mfanyabiashara raia wa jijini Dar es Salaam
ambaye bado hajakamatwa aliyedhamiria kuwapeleka nchini Ufaransa.
“Baada ya
kupata taarifa hizo askari walikwenda kufanya upekuzi katika nyumba za wageni,
na kufanikiwa kuwakamata hao wahamiaji 23 ambao wameingia nchini kwetu kinyume
cha sheria..katika mahojiano hayo, wahamiaji hao wametoka katika nchi
zifuatazo..kuna wahamiaji wametoka nchi ya Kongo au Zaire, kuna wengine
wametoka nchi ya Rwanda na wengine ni raia wa Burundi.” Alisema Mkondya.
Katika tukio
lingine, jeshi hilo limewakamata watu 13 kutoka katika kijiji cha Chikongo
wilayani Tandahimba kwa tuhuma za kuhusika na wizi sugu wa pikipiki katika maeneo
mbalimbali ya nchi.
Aidha, jeshi
hilo linawashikilia wanafunzi Tisa wa chuo kikuu kishiriki cha Stella Maries
mkoani Mtwara ambao wanatuhumiwa kuhamasisha maandamano pamoja na kuchapisha
lugha za kumkashifu Rais.
No comments:
Post a Comment