Monday, December 5, 2016

Simu feki zaidi ya 500 kutoka kwa wateja wa Vodacom kuteketezwa

Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Samson Mwongela(kushoto)akisaidiwa na Meneja Uhusiano kampuni hiyo,Matina Nkurlu (katikati), kuonyesha simu feki zaidi ya 500 zilizokusanywa kutoka kwa wateja wao kwa ajili ya kuteketeza kama ilivyoagizwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wakati  wa mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Gideon Chilambo ambaye ni  Mkurugenzi wa  kampuni ya Chilambo General Trade Company inayoteketeza bidhaa feki.


Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akionyesha simu halisi aina ya Smart Prime 7 yenye ubora na kiwango inayopatikana kwa Tsh 250,000/- kwa maduka yote ya kampuni hiyo, wakati akizungumza  na  waandishi wa habari juu ya simu feki zaidi ya 500 zilizokusanywa na kampuni yake kutoka kwa wateja kwa ajili ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni a Mkuu wa Bidhaa wa kampuni hiyo,Samson Mwongela na kulia ni Gideon Chilambo ambaye ni  Mkurugenzi wa  kampuni ya Chilambo General Trade Company inayoteketeza bidhaa feki.


No comments: