Saturday, July 2, 2016

Mtwara na Lindi hatarini kukithiri kwa watoto wenye mtindio wa ubongo.


Katibu wa afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula, Jenifer Mapembe, akiongea na Juma News.



Mwakilishi kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Omary Gwao, akizungumza na Juma News baada ya ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari wa Mtwara, juu ya athari za matumizi ya chumvi yenye ukosefu wa madini joto.


Na Juma Mohamed, Mtwara.

KUKITHIRI kwa watoto wanaozaliwa na mtindio wa ubongo na kuharibika mimba kwa kina mama ni miongoni mwa athari zinazoweza kuikumba mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na kukosa matumizi ya chumvi yenye madini joto.
Hayo yameelezwa na katibu wa afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula, Jenifer Mapembe, baada ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara juu ya athari zitokanazo na matumizi ya chumvu isiyo na madini joto na namna ya kuielimisha jamii.
Alisema mikoa hiyo inaongoza katika orodha ya mikoa ambayo ina ukosefu wa chumvi ya madini joto huku na kubainisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa katika kila kaya 100 katika mikoa hiyo, ni kaya 13 pekee ndio hutumia chumvi hiyo.
“Athari zinazotokana na kutotumia chumvi yenye madini joto ziko nyingi sana mojawapo ndio hiyo kwamba tunapata watoto ambao wana mtindio wa ubongo, watoto hawakui vizuri ule udumavu wa watoto lakini pia kuna kuharibika kwa mimba, wanawake wanapata mimba zinaharibika..” alisema.

Jenifer Mapembe



Aidha, aliwataka wazalishaji wa chumvi kuhakikisha wanaweka madini joto ili kuhepuka kuwasababishia walaji madhara yaliyotajwa kwani madini hayo hutolewa bure bila gharama yoyote, pamoja na wananchi kuitumia vizuri elimu ya matumizi ya chumvi hiyo ambayo hutolewa kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari.
Mwakilishi kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamiii, jinsia, wazee na watoto Omary Gwao, alisema mikakati ya wizara katika kuwakomboa wakazi wa mikoa hiyo kutoka katika matumizi ya chumvi isiyo na madini joto ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanahabari ili waweze kujua ukubwa wa tatizo na kupanga mikakati ya kuweza kuisaidia jamii.

Afisa habari wa Ndanda Fc na mmiliki wa blog ya Bandari 44, Idrissa Bandari akitoa maoni yake.



“lakini mkakati mwingine ambao tumejiwekea kama wizara ni kuipeleka hii elimu pia kwa watu wa afya ngazi ya jamii tunaita ‘community health workers’ sasa hawa pia wameandaliwa ‘package’ yao ni tofauti kidogo wataenda kufundishwa ukubwa wa tatizo lakii pia kuwatengenezea mkakati wa namna gani watashirikiana na jamii kuhakikisha kwamba chumvi inakuwa na madini joto..” alisema.
Waandishi wa habari walitoa mapendekezo yao walipotakiwa kutoa mikakati yao kupitia taaluma yao ili kufanikisha kutoa elimu kwa jamii ihamasike na matumizi ya chumvi ya madini joto.

Mwandishi wa gazeti la Habari Leo na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) Hassan Simba akitoa maoni yake.



“Kwa mfano Jumamosi iliyopita tulikuwa tunafanya usafi kwenye makaburi pale (Makaburi Msafa), kwahiyo mnaweza mkasema kwamba siku ile ya kufanya usafi kutakuwa na elimu ya matumizi sahihi ya nanii..(Chumvi ya madini joto) mkapewa nafasi mkaielezea wakati huo sisi waandishi si tupo hapa tutakapokuwa tunaripoti kuhusu hicho kitu tutakuwa tunasema miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni pamoja na wananchi upewa elimu..” alisema Hassan Simba, ambaye ni mwandishi wa Habari Leo.


No comments: