Thursday, April 5, 2018

WATENDAJI WA SEKTA YA AFYA KUTOKA MIKOA MITANO NCHINI WANOLEWA MTWARA

Kiongozi wa timu ya mifumo ya fedha katika mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, Dokta Gemini Metei, akitoa somo kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.



Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi, Dokta Genchwele Makenge (kushoto) akiwa na mhasibu wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi (Sokoine), Nurdin Mchinjo, wakifuatilia kwa makini masomo kutoka kwa wakufunzi  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.


Mratibu wa Mpago wa Malipo kwa Utumishi RBF kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dokta Athumani Pembe, akitoa somo kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.


Mhasibu kutoka taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu wizara ya afya, Polycarp Mareba, akitoa somo kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.


Mhasibu wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, Finna Maziku akiratibu taarifa mbalimbali za washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.


Baadhi ya watendaji wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini masomo kutoka kwa wakufunzi  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya hiyo kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.



Watendaji wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini masomo kutoka kwa wakufunzi  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam.

 Mtwara

MAFUNZO yanayolenga kuimarisha uelewa wa pamoja  katika kuboresha huduma za afya kwa kuwashirikisha wananchi  yamefunguliwa mjini Mtwara juzi.
Mafunzo hayo yanataka kuwawezesha watendaji katika ngazi ya mkoa, halmashauri  na vituo vya kutolea huduma kupanga na kutekeleza mipango ya serikali inayozingatia bajeti.
Akifungua mafunzo hayo yanayoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mitano nchini kaimu katibu tawala mkoa wa Mtwara, Elias Nyabusani aliwataka washiriki kujikita na kuelewa maana ya mpango huo ili kuboresha afya za wananchi.
“Lengo mahususi ya mafunzo haya ni kuelewa kwa upana maana ya ugatuaji wa mipango ya afya na bajeti kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma (dhff)” alisema na kuwasisitiza kujikita katika mafunzo na kukidhi matarajio ya mafunzo ya kuboresha huduma.

Alisema mafunzo hayo yamelenga kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa  kuimarisha uwajibikaji na uboreshaji wa  uandaaji wa mipango, bajeti na matumizi  yanayolenga kuboresha huduma za afya.
Mafunzo hayo yamwezeshwa yamefadhiliwa na wadau wa mfuko wa afya wa pamoja (health basket fund) ikiwamo Shirika la Misaada la kimataifa la Marekani (usaid) kupitia mradi wake wa uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (ps3) 
Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma(ps3) unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano katika mikoa 13 nchini inaangalia sekta mbalimbali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano,utawala bora,fedha,rasilimali watu hususan kwa jamii zenye uhitaji
Mafunzo yanayotolewa timu za uendeshaji huduma za afya za wilaya, watumishi wa vituo vya kutolea huduma za afya na wajumbe wa kamati za usimamizi za vituo.
“Lengo letu mkimaliza mafunzo  muweze kusimamia fedha na utendaji wenye matokeo kupitia viashiria vya utendaji (performance indicators) ambavyo ndiyo kigezo cha upatikanaji wa fedha za mfuko wa afya wa pamoja. “ alisema kaimu katibu tawala huyo.
Aidha mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watendaji wa ngazi za mikoa ambao pia watahusika kutoa mafunzo katika ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa, vituo vya kutolea huduma za afya na watendaji wa ngazi ya jamii, kwa lengo la kutekeleza afua za kuboresha huduma za afya kupitia utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo (dhff),  utekelezaji wa chf iliyoboreshwa pamoja na mfumo wa kutumia mshitiri /jazia (prime vendor-pvs) kwa ajili ya manunuzi ya dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pale vinapokosekana kutoka katika bohari kuu ya dawa (msd).

Alisema kuna changamoto mbali mbali katika uendeshaji na utoaji wa huduma katika maeneo mengi nchini hivyo kuifanya serikali kuchukua hatua na kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiundeshaji ili kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande wake mkuu wa mifumo ya fedha wa mradi wa uimarishaji sekta za umma(ps3)Dk Gemini Mtei amesema kwamba lengo la kuendesha mafunzo ni kusaidia jamii kupata huduma bora za afya.
Serikali kupitia mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya uliofanyika Desemba 7, 2016 iliamua kuanzisha utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  ili kuzipa nguvu zaidi kamati za usimamizi wa huduma za afya (hfgc) katika kupanga na kusimamia huduma za afya katika ngazi ya jamii.
Utekelezaji wa utaratibu huo  uliamuliwa  kuanza mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa nne wa sekta ya afya (hssp iv, 2015-2020). Hadi sasa kiasi cha shilingi billion 34 za robo 2 (julai 2017- desemba 2017) zimetoka moja kwa moja wizara ya fedha na mipango na kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma 5,125.

No comments: