Tuesday, June 21, 2016

Ashikiliwa na jeshi la Polisi Mtwara kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka ‘8’.




Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP-Henry Mwaibambe.


Na Juma Mohamed, Mtwara.

JESHI la polisi mkoani Mtwara linamshikilia Andrea Machael (28) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Magumchila wilayani Masasi kwa kosa la kumbaka mototo wa miaka Minane ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Magumchila, na kumsababishia maambukizi ya ugonjwa wa zinaa.
Akzungumza mkoani hapa, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP-Henry Mwaibambe, alisema hatua hiyo imetokana na mama mzazi wa mtoto huyo kuamua kwenda kituo cha polisi kutaka msaada wa kumpeleleza mtoto wake, baada ya kumwona hatembei vizuri huku akificha kueleza sababu.
“Tarehe 16 mwezi huu wa sita majira ya asubuhi mama yake mzazi alimshtukia huyu mtoto kwa mwendo wake akaona kama hatembei vizuri, sasa akawa anmbana kwanini yuko vile, yule mtoto akawa anazubaisha sasa Yule mama akamchukua mtoto na kumpeleka polisi Masasi, sasa pale polisi tuna dawati la watoto na jinsia wakaanza kumu ‘Interview’ Yule mtoto kwanini yuko vile, mtoto akakiri kuwa alikuwa akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa muda mrefu..” alisema.

Henry Mwaibambe.



Aidha, Mwaibambe alisema mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akimpa mtoto huyo fedha sh. 500 hadi 1000 katika kipindi alichokuwa anamfanyia vitendo hivyo, amemsababishia maambukizi ya ugonjwa wa Kaswende ambao umebainika baada ya kwenda kufanyiwa vipimo vya afya.
“Tukachukua jukumu la kumpeleka mtoto hospitali ya serikali ya Mkomaindo tukagundua kwamba mtoto huyo amefanyiwa vitendo hivyo sana na ameambukizwa maradhi ya zinaa ambayo ni Kaswende..mtuhumiwa akakamatwa siku hiyo hiyo ya tarehe 16 na tukampeleka hospitali kwenda kumpima na kweli akagundulika mtuhumiwa ni mwathirika wa ugonjwa wa Kaswende..” aliongeza.
Alisema, tayari upelelezi juu ya tuhuma hizo umekamilika ambapo mtuhumiwa huyo ambaye yuko rumande anatarajiwa kufikishwa mahakamani June 17 mwaka huu huku kesi yake itasikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Masasi.
Katika hatua nyingine, Mwaibambe amesema jeshi la polisi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti matukio ya wizi ambayo yalijitokeza katika manispaa ya Mtwara Mikindani yalioambatana na imani za kishirikina.

No comments: