Friday, April 22, 2016

Madaktari nchini watakiwa kuacha kufoji vyeti kwa walimu.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akitoa hotuba kwa wahitimu katika chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara




Wahitimu wa katika chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara.



Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu mmoja wa wahitimu wa chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara.


Na Juma Mohamed, Mtwara.

MADAKTARI nchini wametakiwa kuacha tabia za kufoji vyeti vinavyothibitisha magonjwa hatari kwa baadhi ya walimu wanaokwepa kwenda kufanya kazi vijijini kwa kisingizio cha kuugua, na kutaka wapangiwe kufundisha katika shule za mijini.
Akizungumza katika maafali ya chuo cha Uwalimu cha Montessori mkoani hapa, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, alisema walimu wengi wanaopangia ajira vijijini wamekuwa na visingizio vingi ambavyo vinalenga kukwepa kwenda kufundisha huko na kupelekea mahitaji ya walimu katika shule za vijijini kuwa makubwa.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally


“Unaweza ukapokea cheti cha kuonesha kwamba huyu mtu anaugonjwa wa hatari, tujue pia kuna mungu, unaweza ukawa unajiombea maana kama unafoji cheti unasema mimi naumwa kitu fulani siwezi kukaa sehemu ya mbali na hospitali Mungu anasikia unaweza ukajikuta unajiombea dua mbaya mwenyewe..” alisema.
Aliongeza kuwa, waajiriwa wengi walioko mijini walianzia huko huko vijijini na wakati mwingine hata teknolojia ya mawasiliano inakuwa ngumu lakini ni uvumilivu na moyo wa kujito kufanya kazi kwa bidii ambapo baadae wameweza kuhamishiwa katika vituo vya mijini.

Burudani ya aina yake


Kuhusu suala la kuchelewa kwa ajira za walimu ambalo liliwasilishwa na wahitumu kupitia risala yao, mkuu wa wilaya aliwaomba kuwa wavumilivu na kusema kuwa mambo mazuri hayataki haraka na kuwahakikishia kuwa sekta ya elimu ajira zipo hata kama zinachelewa.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya chuo, Francis Kasoyaga, alisisitiza juu ya nidhamu kwa wahitimu hao ambao jumla yao ni 33 kwa daraja la 3 A, ambayo wamedumu nayo kwa kipindi chote walichokaa katika chuo hicho kilicho chini ya shirika la kidini la Mkombozi.

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara, Francis Kasoyaga, akiwahusia wahitimu wa chuo hicho juu ya namna ya kwenda kuishi waendako.


“Mumehitimu katika chuo ambacho kinaendeshwa maadili ya kiroho lazima tuoneshe tabia zetu kuwa ni tofauti na za wale ambao wametoka katika vyuo vingine, kila mtu akikuona ajue kabisa kwamba huyu ametoka katika chuo cha Montessori kwa matendo yako..” alisema Kasoyaga.
Chiku Jamuhuri, ambaye ni miongoni mwa waliohitimu chuoni hapo, aliahidi kwenda kupambana na changamoto zozote zinazowakabili walimu na kwenda kuyafania kazi yale yaliyosisitizwa na mkuu wa wilaya katika hotuba yake.

Aidha, aliishauri serikali kuona umuhimu wa kuboresha masilahi ya walimu hasa mishahara pamoja na kuboresha miundombinu ya kuwawezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupata mahitaji mbalimbali.

No comments: