Wednesday, March 16, 2016

Wananchi washauriwa kudai risiti za bidhaa zinazodhibitiwa.


Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, akihutubia katika kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Mtwara.




Baadhi ya wadau kutoka katika taasisi mbalimbali mkoani Mtwara walioshiriki katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji yaliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara.





Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, akihutubia katika kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Mtwara.


Na Juma Mohamed, Mtwara.

WATUMIAJI wa bidhaa mbalimbali zinazodhibitiwa nchini wameshauriwa kudai risiti za manunuzi au huduma, ambazo zitawasaidia kudai wajibu wao pindi inapotokea tatizo wakati wa matumizi ya bidhaa au huduma alizopatiwa.
Wito huo ulitolewa mkani hapa juzi na katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, wakati wa kuhitimisha siku ya Kimataifa ya maadhimisho ya haki za mtumiaji, yaliyofanyika Kitaifa mkoani hapa katika ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo katika Chuo cha Uwalimu Mtwara (TTC).
Alisema mtumiaji anayefahamu haki na wajibu wake ana nafasi kubwa ya kuhakikisha hadhurumiwi anapofanya manunuzi ya bidhaa sokoni na maeneo mengine ukilinganisha na yule ambaye hafahamu wajibu wake.
“Mtumiaji atakaefahamu umuhimu wa kudai risiti na akafanya hivyo kwa kila manunuzi anauwezekano mkubwa wa kuanzisha malalamika endapo atatendewa visivyo katika shughuli zake za kununua bidhaa katika soko..” alisema na kuongeza:
“Mtumiaji atakaetumia taarifa za upakiaji salama wa mizigo katika vyombo vya usafirishaji atakua na uhakika wa mizigo yake kufika salama kuliko asiye na taarifa hizo..” aliongeza.
Aliwataka watumiaji kuwa na utaratibu wa kujisimamia wakati akifanya manunuzi kwani kwa kufanya hivyo watakuwa makini katika kuhakikisha wanapata wajibu wao kuliko yule ambaye anasubiri serikali imsimamie.
Kwa upande wake, katibu mtendaji wa baraza la ushauri la Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA), Dkt. Oscar Kikoyo, alisema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, kulikuwa na kazi za uelimishaji kwa watumiaji iliyokuwa ikifanywa na mabaraza yanayounda Jukwaa la Watumiaji.

Kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji Tanzania (TCF), Thomas Mnunguli akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji.

Alisema, miongoni mwa changamoto walizozipokea kutoka kwa watumiaji ni maswali juu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, miundombinu mibovu ya maji na makato ya kila mwezi katika huduma za maji na umeme (Service Charge) na kudai kuwa hakuna taarifa zinazotolewa kwa watumiaji juu ya changamoto hizo.
Alisema, kupitia mabaraza hayo, waliweza kutoa elimu kwa watumiaji juu ya namna ya kudai haki zao za kupata taarifa kwa huduma wanazopewa kutoka katika kampuni au mashirika mbalimbali.
“Kazi kubwa tunayoifanya ni kutoa elimu kwa mtumiaji kwamba yeye mwenyewe aweze kudai haki yake, mojawapo ya haki anayoweza kudai ni haki ya kupewa taarifa, kwamba ok kuna huduma hii, je mtumiaji ana taarifa za kutosha kuhusu huduma Fulani..” alisema Kikoyo.



No comments: